Kumbe anafanya kazi ya kuuza baa.

Kumbe anafanya kazi ya kuuza baa.

Ni ajira ambayo ina vikolombwezo vingine ambavyo vinamfanya muajiriwa awe na uwezekano mkubwa wa kuambukizwa vijidudu vya HIV kuliko muajiriwa katika fani nyingine yoyote ile.

Hivi best, kuuza bar sio ajira sawa na nyingine?
 
Mpige chini piga noyo konde maisha yasonge mbele
 
Hivi best, kuuza bar sio ajira sawa na nyingine?

Tusidanganyane, hiyo ni kazi ambayo mtu anaifanya baada ya mambo mengine ya msingi yameshindikana! Hebu tuambie, kama wewe ni mwana-mme, utajivunia kuoa Bar-maid?
 
Kama mambo madogo namna yanakushinda sina hakika kama unaweza kufanya research ya Masters ukafaulu vizuri.
 
Tumia elimu yako vizuri, jibu lipo wazi unasubiri nini? Mpaka tukushauri! Aaah.
 
Ni mtu ambaye nilikua namuaandaa kua wife nilimpeleka mpaka nyumbani nae kanipeleka kwao so sio jambo la mzaha mkuu
 
Ni kweli ananafasi zingine kwani nilishawahi kumuwezeza na akawa na nashughuri zake ndogo ndogo. elimu yake ni kidato cha nne.
 
Pole sana, lakini chamsingi hapo nikuachana nae, hamtowezana huyo kwa sasa anatafuta hifadhi yakimnyookea atakua haas.
 
huna haja hata ya kuomba ushauri, mbona jibu lipo wazi?! tatizo umelewa mapenz, fikiri kwa kichwa sio Moyo!!
 
Nilikua na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke M1 kutoka kijijini ambako tulikua tukiishi huyo mpnz wangu alikua akiniaga mara kwa mara kua anenda Jijini Dar kumsalimia dada yake na pia alikua akirudi kijiji na kukaa muda wa miezi miwili au mitatu!! kisha anarejea tena DSM nikimuuliza kua anfanya kazi gani alikua ananiambia anamsaidia dada yake kuuza mgahawa. kitu cha ajabu nikihoji sana kuhusu kazi yake alikua anakasirika sana.

kwa bahati nzuri nilipata nafasi ya kuja kusoma masomo ya juu yaani shahada ya Uzamiri sikutaka kumtafuta kwani nilikua busy sana na masomo lakini kitu cha ajabu alinipigia simu na kunieleza kua amepata taarifa kua nipo DSM aliniomba tuonane tulipo onana akaniambia kua ananiomba pesa kwa ajili ya kulipia pango la nyumba nilishangaa sana kusikia hivyo nilimuuliza kwani nyumbani kwa dada yake amehama akaniambia kua shemeji yake anamtongoza ndio maana ameamua kuondoka na kujitegemea yeye. nilimshauri arudi kijijini kwani kuna nafasi kubwa ya malazi pia na fulsa nyingi za kujiajiri alikataa na kuniambia kua na mimi nimekimbia nini kule kijijini nilimweleza kua mimi nipo hapa kwa muda tu then nitarudi kijijini nikimaliza masomo yangu. nilipomweleza hivyo akaniambia tusitafutane tena na kuniambia mimi ni mshamba nikamjibu kua mi sina tatizo. ukapita muda kama wa mwezi m1 akanitumia ujumbe kua ananipenda na wala hajisikii vzuri kuachana mimi na ananiomba nionane.

Nilikubali kwasababu nilikua nampenda pia tulipoonana akanielezea jinsi maisha yanavyomsumbua hapa jiji DSM nilimuuliza anafanya kazi gani hakutaka kuniambia nilipombana kwa kushawishi aliniambia yeye ni Bar attender nilihuzunika sana kufanya kazi hiyo wakati anafursa nyingi za kujiajiri ambazo ni salama hasa kwa afya yake na lkn yeye hakuonesha wasiwasi wowote. na aliniambia hana mpango wa kurudi kijijini nilipofanya uchunguzi kumbe aliolewa na kua mke wa pili yaani nyumba ndogo. akamtibua huyo jamaa aliemuweka ndani yule jamaa akamkimbia.

sasa ananiomba turudiane wakati nikimwambia tukaishi kijijini yeye hataki anataka tuishi jijini na pia anataka kuendelea na hiyo kazi yake ambayo mimi siitaki.

kitu kingine nikimwambia tukapime yeye hataki hata kusikia suala la kwenda kupima hata wiki inaweza kuisha bila kuwasiliana nae nikimpigia hapokei.


naomba ushauri wana JF.

Tafadhari msitukane!!!!!!!!!!!!!
Kiswahili chako kibovu sana!!!
Hata kiingereza pia hujui.... 'Bar attender??'
Yaani na wewe una shahada ya Uzamili???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom