Kumbe alifukuzwa seminari

jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Jan 23, 2013
5,321
2,000
Wakuu amani ya bwana iwe nanyi,

Juzi kati nipo katika route zangu za kusaka mkate nikapanda mwendo kasi from kimara to Gerezani,

Ile tumefika pale mapipa akaingia mzee mmoja hivi chek boob ana miwani ya jua kajitupia pensi lake mwenye na chini ana snikers kifupi yule mzee alikuwa 50's to 60'

Haraka haraka nikaukumbuka ule uzi wa cisco (RIP) wadau walivyokuwa wanamuelezea

Sasa mle ndani zikawa zinapigwa ngoma za mababu zetu yaani zilipendwa,

mimi nilikuwa nimepiga chapa ya konyagi pembeni ya yule mzee(tumesimama parallel),

Mzee na mawazom yangu kama leo usiku nitakula kwa sababu mfukoni ilikuwa inasoma buku tu ,

Mara mzee anatikisa kichwa ile kama anazielewa sana zile nyimbo,

Sasa kwa makamo yake ikabidi nimcheki wa jicho fulani hivi la ki-investigation kama vile jack bauer kamuona habibu marwan,

sasa mzee kuona nimemkata jicho lile la ki-FBI akacheka halafu akaniambia enzi zetu na akina fulani ( sitaji naogopa unuio) hizi wakati tupo secondary,

Mzee pamoja na fikra zangu za mlo wa usiku nikasema siwezi kumpotezea huyu mzee kijana,

Bas nikamuuliza lini mzee na ulikuwa wapi enzi hizo akaniambia miaka ya sabini(sikumbuki mwaka exactly).

Bas akaendelea kwamba alikuwa anasoma Lake secondary hii ipo mwanza karibu na hospital ya sekou toure.

Bas mzee nikajifanya kuhamaki eeee kumbe umesoma nae ndo mzee akaanza kutiririka vizuri kwamba mwana alifukuzwa seminary ndo akaja pale kwetu.

Bahati mbaya sana tukatia nanga pale gerezani mzee akasepa zake na mimi nikaelekea pale mtaa wa kongo kutafuta wanaohemea niwabebee mizigo yao ili siku iweze kuisha

Ila kichwani nikawa nawaza dah kumbe nyota njema huonekana asubuhi kumbe alikuwa hashikiki toka enzi za udogo wake.


Goodmorning wananchi wa danganyika kila la kheri katika siku hii mpya ya ripoti mpya ya mchanga

Mlio na luninga mtatu-updates sisi tusiokuwa nazo anyway kama kawa kama kawizi wacha nielekee mtaa wa kongo nikacheki kitu sana wabebewaji mizigo nao wanabana sana bonge ya lifurushi anataka mia 300 ukigoma anakutema

SALUTE
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom