Kulogea/kulogewa yai viza

Kulogea/kulogewa yai viza

sasa kaa mimi sina imani na hayo mtu mwingine akininuzia nitadhurika?
 
Yai viza ni kitu kisichofaa kimekufa kinanuka hakina uhai...yai viza hutumiwa sana na wachawi wenye roho mbaya kuharibu maisha ya mtu..ni mojawapo wapo ya uchawi mbaya kabisa kulogewa nao
Mara nyingi hunuizua maneno kama haya ....kama hili yai lisivyo na uhai ....kama hili yai lisivyo na faida...kama hili yai linavyonuka...

Kisha baada ya manuizi hayo hupasuliwa njia panda ili litawanyike pande nane za uso wa dunia ili kila utakapoenda utakalofanya lisifanikiwe na uchukiwe na kukimbiwa na kila mtu....hata ulikuwa una mafanikio kiasi gani ghafla hujikuta unaanguka na nuksi balaa na mikosi kukuandama

NB: Sifundishi uchawi bali najaribu kuelezea ubaya wa kitu fulani kama hiki ili siku ikitokea kuna mtu kakuudhi usimfanyie jambo baya kama hili bali mwachie Mungu kwakuwa yeye ndio mwamuzi wa haki
Na wewe kama kuna mtu kajaribu kukufanyia hivi Usijaribu kwenda kwa waganga wa kienyeji kwakuwa huko unaenda kutafuta balaa zaidi la viapo na maagano ambavyo unaweza kuja kushindwa kuvitengua
Mwachie Mungu kwakuwa hata juju liweje huwa lina kikomo cha kuishi na kufanya kazi expire date

mkuu, yai viza linazo kazi nyingi tu, kuna mkoa yanauzwa bei mbaya, linatumika kutegea kenge, linachemshwa halafu anawekewa kenge asivyo na akili yeye huwa ni kumeza na kulipasulia tumboni, hapo ndo huuingia mkenge.
 
mimi kuna watu wanapitaga kwa watu tunaoangua vifaranga na kuomba tuwauzie mayai viza kumbe ndiyo wanaenda kudungulia watu future zao... yule jamaa alinidanganya eti wanaenda kutengenezea sumu ya kuua wadudu ...
 
Kamwe hawawezi kukwambia ukweli ni kama hiyo ya kenge wanaficha ukweli kuna jinsi nyingi za kumtega kenge
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom