Kulipa kisasi kumenifikisha hapa

Kulipa kisasi kumenifikisha hapa

Usijidanganye, mwanamke wa Kiislam haolewi na mwanamme wa kikristo hata siku moja.

Wewe ni mkristo unakuja kudanganya watoto wa kike wa Kiislam waone kama kitu cha kawaida mwanamke wa Kiislam kuwa na mwanmme wa kikristo. Hakuna hiyo katika Uislam, msitutukane kistaarabu.

Watoto wa kike wa Kiislaam hizi ni porojo wala msifikiri hiki kisa ni cha kweli, hawa wenzetu usiku na mchana wanafikiri mbinu mpya za kuuharibu Uislam, wapo katika mkakati wa "mass brainwashing". Wanatumia media zote, kuanzia majarida, filamu, mpaka hii mitandao ya kijamii - Kumbukeni hilo.

Punguani wahed.

teh teh teh..kweli eeeh??labda ndoa za kiserikali
 
Habari wapendwa,

Poleni na majukumu ya maisha. Wandugu nisiwachoshe mwenzenu kuna mkasa umenipata yaani nashindwa kufanya maamuzi.

Stori inaanza hivi, mimi niliolewa na nikajaaliwa kupata watoto watatu wawili ni twins, mume wangu ni mkristo mimi muislamu.

Sasa wakati mume wangu ananioa nimemkuta na mtoto alizaa na mdada flani hivi muigizaji wa Bongo Movie.

Huyo dada hakumuoa alizaa nae tu wakaachana na mtoto huyo nimemlea mimi mpaka sasa yupo darasa la2.

Mwaka juzi nilipata mkasa mzito sintosahau, nilipakaziwa kitu ambacho sijafanya ikawa ndo sababu na nikaachika kwa talaka kabisa.

Ni kwamba kuna mtu inasemekana alipiga simu kwa wakwe zangu na kujitambulisha kwamba yeye ni rafiki yangu na tupo kwa mganga kwa lengo la kumroga mume wangu nimuue ili nirithi mali zake.

Muda wote huo me skujua kwanini mama mkwe ananichukia ghafla wakati mwanzo alinipenda kama amenizaa.

Mwisho wa siku nikapewa talaka nikarudi kwetu nikiwa na mimba ya mtoto mwingine, nimehangaika peke yangu mpaka nimejifungua.

Nikarudi chuo nimemaliza chuo mume wangu amenifuata kuniomba msamaha turudiane tulee watoto wetu.

Kibinadamu nikamsamehe lakini Mungu hamfichi mnafiki siku ikafika nikagundua aliefanya huo mchezo ni yule mwanamke aliezaa nae lengo lake arudi yeye.

Lakini kisicho riziki hakiliki pamoja na kufanya hayo bado mume wangu hakumrudia.

Akapata bwana mwingne ni askari akazaa nae mtoto mmoja, huyo bwana aliona picha yangu Instagram akanitafuta,yeye hakujua na hajui kama namjua.

So amekua mpenzi wangu kwa muda kidogo, mimi nilikua nafanya kwa kumkomoa yule mwanamke alieniharibia kwangu.

Sasa jamaa huyu ndo amenogewa anataka ndoa nampa tarehe tu kila siku yani nimedata tu hapa.

Nampenda sana na ananipenda hivi keshokutwa anataka kunipeleka kwao Usukumani kunitambulisha.

Mume wangu wa kwanza huyo ni mkristo, huyu ni mkristo but yupo tayari kubadili dini hata leo.

Nampenda ni mstaarabu, muwazi, mkweli, ana huruma, anajua mapenzi tofauti na wa mwanzo.

Sasa nawaza je, akija kujua kama mimi nilikua nalipiza kisasi atanichukuliaje?

Atanipenda? Haya nitamuachaje yule niliezaa nae watoto watatu wakati ameshaomb radhi?

Ushauri please

Duuh kisasi cha kuvua ch..piiii kibokoo hicho kisasiiii, siwezi sema wee malayaaa but mmmmhh
 
Usijidanganye, mwanamke wa Kiislam haolewi na mwanamme wa kikristo hata siku moja.

Wewe ni mkristo unakuja kudanganya watoto wa kike wa Kiislam waone kama kitu cha kawaida mwanamke wa Kiislam kuwa na mwanmme wa kikristo. Hakuna hiyo katika Uislam, msitutukane kistaarabu.

Watoto wa kike wa Kiislaam hizi ni porojo wala msifikiri hiki kisa ni cha kweli, hawa wenzetu usiku na mchana wanafikiri mbinu mpya za kuuharibu Uislam, wapo katika mkakati wa "mass brainwashing". Wanatumia media zote, kuanzia majarida, filamu, mpaka hii mitandao ya kijamii - Kumbukeni hilo.

Punguani wahed.

Nilijua uta deal na linalihusiana na dini tu kwani siyo siri wewe ni mdini 100%.

Ungempa ushauri kwa mkasa wake na siyo kumaliza na tusi.

BTW mzima wewe?
 
Yani wewe mwanamke unaonekana ni Malaya kabisa kwahiyo kama huyo jamaa ana ngoma umeamua kuifuata mwenyewe ama kweli ujielewi... unamuacha mume uliye zaa nae unachepuka kwa kulipiza kuwa mkweli unafuata pesa zake tu afu mwisho wake utabeba mimba yaani huoni kama utawapa shida watoto.ushauri wangu kwako nenda kapime afya kwanza kabla ya yote maana we maji mara moja si umejipendekeza mwenyewe kwa huyo jamaa.
 
Nilijua uta deal na linalihusiana na dini tu kwani siyo siri wewe ni mdini 100%.

Ungempa ushauri kwa mkasa wake na siyo kumaliza na tusi.

BTW mzima wewe?

Hamna ukweli katika huo mkasa, haya mambo muwadanganye misukule wenzenu.

Kusema kweli ndiyo maana yake "mdini"? nioneshe wapi kwenye Uislam inaporuhusiwa mwanamke wa Kiislam kuolewa na asiye Muislam?
 
Tatizo umesema mmeo alioa m-bongo movie kwahyo hii ni moja ya SCRIPT kutoka kwa m-bongo movie.
 
Anayetaka kulipiza kisasi ani pm, gharama za hotel na vaseline juu yangu kama atapenda.
 
Kama aliweza kukuachisha kwa MMEO atashindwa KUKUMALIZA kabisa kwa kumchukulia MMEWE:what:
 
Mwanamke wa visasi namuogopa sana anaweza kukuwekea sumu kwenye chakula akakuulia mbali

Unaonekana ni mkatili sana pamoja na mme wako kukuomba samahani bado unaenda kujitongozesha kwa bwana wa adui yako. Kwa jinsi ilivyo ulidhamilia kutenda ujinga huu eti alikuona insta acha hiyo tabia ya visasi.

Kweli kabisa ni uaji
 
Hamna ukweli katika huo mkasa, haya mambo muwadanganye misukule wenzenu.

Kusema kweli ndiyo maana yake "mdini"? nioneshe wapi kwenye Uislam inaporuhusiwa mwanamke wa Kiislam kuolewa na asiye Muislam?

we bibi acha usenge basi... mbona ni dada yangu ni muislam haswa na kaolewa na mkristo. acha kuendekezea udini,mapenzi hayaychagui dini.

fumbafuuu thaaaana
 
Ngoja nimtume mke wangu aje akuchonganishe kwa hao wanaume .............
 
Back
Top Bottom