Kulikoni Watanzania? Nchi nyingi Wananchi wanaandamana Kupinga Hali Ngumu Lakini Sisi Kimyaaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni Watanzania? Nchi nyingi Wananchi wanaandamana Kupinga Hali Ngumu Lakini Sisi Kimyaaa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NdasheneMbandu, Jan 16, 2012.

 1. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Watanzania tumelogwa au ndiyo ule wimbo wa magamba wa amani na utulivu. Nchi nyingi duniani hivi sasa wananchi wanaandamana kupinga maamuzi ya serikali zao kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii lakini watanzania tupo kimyaaaaaaa kana kwamba serikali yetu inafanya vema. Mfano mzuri ni maandamano yanayoendelea nchini Uganda na Nigeria mpaka serikali zao zinaelekea kusalimu amri. Sisi hapa kwetu juzi tu EWURA wamepandisha umeme kwa wastani wa asilimia 40.29 lakini sisi tunaishia kulalamika kwenye vijiwe vyetu tu mitaani. Ifike mahali watanzania tujifunze kwa wenzetu kuwa na ujasiri. Serikali ya ccm imefanya maamuzi ya hasara mengi na makubwa kwenye mikataba ya umeme matokeo yake ni kuendelea kubebeshwa mizigo ya bei kila baada ya muda mfupi. Pamoja na hali hiyo, bado tupo kimya. Hatusikii chama chotechote kitaandaa maandamano ya kupinga ongezeko la bei. Shime watanzania tufanye maamuzi. Tutaangamizwa na maamuzi haya ya kifisadi.
   
 2. T

  TUMY JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii kauli ilikuwa na maana kubwa sana " TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU".Watu tuliichukulia poa ila ina maana yake wajameni.Mtakuja kumkumbuka.
   
 3. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Si muda mrefu utaitwa kuhojiwa na Polisi....Watz tumejaa ubinafsi,fitina na woga
   
 4. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Mi nna wasiwasi hapa tulipofikia hata tukivamiwa na nchi jirani ikahamua kuchukua mlima kilimanjaro tutabaki tunawaangalia tu. Na kulalamika vichochoroni.
   
 5. MAKOSHNELI

  MAKOSHNELI JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 474
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 80
  Wapinzan mmeanza eeh ?
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280
  Kuhamasisha maandamano ya kuipinga serikali ni "uchochezi"!.

  Watanzania ni watu wa amani!. Hatuko kama wale Wamisri, Watunisia au Walibya!.
   
 7. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nilishawahi kuandika humu ukumbini kuwa ni BORA MAISHA YAWE MAGUMU ZAIDI YA HIVI (in fact mambo yanazidi kuharibika and I am sure soon yatatimia) ili Watanzania ambao mpaka leo hii wanawaamini ccm watie akili.
   
 8. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Tatizo mi naona si wanaowaamini CCM, tatizo wasioamini kitu chochote.
  tuliona ile kampeni ya walk to work nchini Uganda napata wakati mgumu kuamini kama watanzania wako tayari kufanya hilo.
  vyama vya wafanyakazi Nigeria viliitisha mgomo, hapa kwetu kila siku ni matamko
   
 9. O

  Omr JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We njaa zako unazileta hapa kuhamasisha wenye maisha mazuri. Katafute kazi kijana
   
 10. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Ukiona hivyo ujue watsnzania wote ni wezi; yes ni wezi kama sio wa pesa basi muda wa mwaajiri ndio maana pamoja na ugumu huu bado wanaishi tu!
   
 11. S

  STIDE JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mwenzetu wewe unayo maisha mazuri nini!!?
   
 12. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  bro kizazi kilichotafuta uhuru kumeanza kuisha, kuna kizazi hapa kilichoanzia 2/5/1977. hiki ndicho kitakuja kufanya yale ya cairo. muda c mrefu utashuhudia hilo.
   
 13. grey

  grey Senior Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  tumerogwa, si umesikia viongozi wanalala makaburini au?
   
 14. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pascal,

  The time bomb is ticking tik tok tik tok

  It is a matter of time.

  Unless system ibadirike naku prempty unrest by doing things right. First and foremost wadhibiti rushwa. It doesn't cost much kudhibiti rushwa.
  This will be a good step to restore the public trust.
  Otherwise wait and see.
   
 15. MissyNana

  MissyNana Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania ni wanafiki tunalalamika tu pembeni tukiwaona viongozi kuwaambia shida zetu tunawaogopa. Haswa wakitupatia ahadi za kijinga au vitu vidogo visivyo na maana. Walio wachache haswa viongozi wa vyama vingine wameridhika na maisha yao binafsi; inaonekana kama vile wanasahau waliowachagua. Na CCM ndio kabisa hawajali chochote as long as familia zao zinaishi maisha mazuri na wala hawajui shida nini. Tuliobaki akina kapuku tunakubali chochote kile; hakuna umeme, maji upandishwaji wa bei za vitu sie kimya. Kuandamana ni kudai haki na wala si uchochezi; kwani ikiwa kama raia tunahitaji mahitaji yote muhimu kama binadamu wengine. Inatubidi tuamke sasa kwani tumelala sana...
   
 16. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  either TUMERIDHIKA KUTESEKA or TUWAOGA KUPINDUKIA
   
 17. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mbuzi yake kamba,akikubali hilo ataendelea kula majani ya eneo ambapo kamba inaishia.WaTZ tubadilike.
   
 18. N

  Nguto JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,652
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Mh! We mie sitaki kufa afadhali nilipe tu!!!
   
 19. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  vilaza ni wengi hii nchi na ujamaa bado una nafasi kwenye vichwa vya watu.
   
 20. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Hali ngumu ipi?, hauli?. We jali kama laifu lako linasonga tu. Maandamano mtafanya nyie tu ila impakiti yake mtaisoma.
   
Loading...