Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,802
- 71,229
Jee hizi tetesi kuwa wafanyakazi wamegoma kudai mishahara ni za kweli? Maana naona kwa siku mbili tatu matangazo hakuna ni miziki tuu bila ukomo!
Na kwa nini vyombo vingine vya habari vimefanya huu ni usiri jee hawataki kuzungumzia haki za wenzao? Au na wao hawakuwa na ushirikiano na wenzao?
Hata CCM wameshindwa kutoa msaada kwa kituo ambacho ndio msaada wao mkubwa kwa propaganda zao?
=====================
Steve Diallo, mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki Star TV, Radio Free Africa na Kiss FM amesema “Wanadai malipo ya mishahara ya miezi tofauti, wapo wa miezi mitatu na wengine zaidi, tumetoa taarifa TCRA na kwenye Ofisi ya Kamishna wa Kazi, hata Waziri Nape (Nnauye) alipiga simu kuulizia kinachoendelea.”
Ameongeza “Tunafanya vikao na wafanyakazi ili kutatua changamoto. Pesa hatuna, hatuzalishi ya kutosha ukilinganisha na mahitaji yaliyopo ya Satellite na kukatika kwa umeme. Kukatika-katika kwa umeme kumesababisha matumizi makubwa ya jenereta.”