nimeguswa na hii mada kwa maswali lukuki kuwa je ni huyu mzee kijana tu alie kimya wakati huu? je kwanini yuko kimya? yupo ofisini? busy? lakini mbona na wakubwa zake pia nao kama wamemwagiwa maji wako kimyaaa, ripoti hii imetaja mafisadi wote ofisi walipo na kiasi walichoiba, ni aibu sana kwa nchi na serikali kwa ufisadi huu wa kutisha uliofanyika na wenye ushahidi, je mahakama ya mafisadi ofisi zao ziko wazi au wapo likizo? je kwanini hawaanzi kukamata na kuwahoji wahusika wote simply kuanzia na all budget holders na signatories wa kila wizi ulioandikwa na CAG, ni aibu na kichekesho kikuu kusema serikali inapambana na ufisadi na kuwaacha mafisadi wenye ushahidi wakidunda mitaani , shime sana mahakama ya mafisadi ifanye kazi yake sasa kuwakamata mafsadi wote walioainishwa kwenye ripoti ya CAG , ni bora tutafute kauli mbiu ingine!!