Ndoa za sasa zipo kwa mihemko tu ya kupendeza siku ya harusi, pete yangu ya tanzanite na whitegold, nitakavyobadilisha nguo siku ya harusi kanisani shela ukumbini gauni nimeagiza dubai, bwana harusi anavyojua kuvaa na kupangilia rangi na wale marafiki zake watakavyoingia kwa mbwembwe, mtu hawazi baada ya kuachwa hotelini unakuwa mama au baba kila kitu kinawahusu tena mkijadiliana kwa pamoja siyo baba anawaza kununua kiwanja mke anawaza kuchukua mkopo wa kununua vitz ili awaambie mashostito baada ya ndoa tu akanipa gari, kumbe gari kakopa na mgogoro kwenye ndoa ukaanzia hapo kila mara mnapishana kauli kwa kuwa mwanaume ulitaka kuoa msomi siyo mke anaamua anavyotaka, uliacha kumuoa mke mwenye heshima kisa wewe unamzidi elimu hamtaendana, haya sasa umempata huyo kama wewe yeye anajua usawa tu hamsini kwa hamsini, mwanamke ni mwanamke tu itabaki kuwa hivyo mavyeo yako ukifika home yaache mlangoni tena getini kabisa ukiingia ndani wewe ni mke mtii mumeo, wengine eti wanasema usizoee kumuaga mumeo mpe taarifa tu ndoa inakufa hiyo kwenye ndoa kuna mke zaidi ya mmoja ila siyo mume zaidi ya mmoja, na wazazi nao wanachangia siku ya send off mwanangu chumba chako hakijapangishwa ukiona anakutesa rudi tu maneno gani hayo kweli akiona mwanaume kachepuka kesho kwao, wanaume mfanye kazi mlete chakula nyumbani usitegemee sana hela ya mwanamke hawajaumbwa kutoa, ndo mana bibi na mama zetu walidumu hawakupewa majukumu makubwa ndani.