Kulikoni ndoa za siku hizi?

Kulikoni ndoa za siku hizi?

nani anataka kuishi na Malaya aje aletewe miwaya ndani!! wacha waachane tu.

na usiseme wanawake wanalipiza, sema wanaenda kutafuta furaha yao. unafikiri ni maboksi hawana hisia au wana mioyo ya chuma? aishi maisha yake kumlilia MTU ambaye hamjali? acha tu watafute furaha nao.

ukisema tu ndoa ina miaka thelathini wala hunivutii, hadi nijue ni ndoa kweli ama vepee! sio sifa kusema tu ndoa INA muda mrefu wakati wahusika hawafurahii, mnafurahia nyie watazamaji!
Dah! Kuna kaukweli fulani lakini hapa
 
Tatizo kubwa nikuwa watu wanajua mambo ya ndoa sn kabla hata ya kuingia kwenye ndoa na pia watu wanajiandaa mno na huwa wanaingia kwenye hii bond ya ndoa na majibu ya changamoto ndo mana hata ukijaribu kufuatilia aina ya maoni ya wadau wanayotoa utaona kuwa watu wameshaandaa majibu ya ndoa zao,utasikia mambo ya kiwa magumu naondoka,japo sio vibaya kujua na kujiandaa lakin vizur kutumia formula(majibu) kulingana na swal(changamoto)
 
Uliyoyasema yote ni kweli. Mi nadhani tatizo kubwa watu wanakimbilia ndoa labda kwasababu wanaona wenzao wameoa/kuolewa au wamehimizwa na familia au kupenda sifa tu hasa kwa wadada au pia kuona umri umeenda. Nimesoma vitabu vichache vya ndoa na kufahamu kua sababu pekee ya kumfanya mtu aingie kwenye ndoa ni utayari wa kuingia kwenye ndoa na si vinginevyo.
Hamna ndoa iliyokosa changamoto, ata kama hao watu walipendana kiasi gani... Uvumilivu ndo unafanya ndoa nyingi zidumu.
Pia upendo usiwe kigezo pekee cha kuingia kwenye ndoa. Upendo huzaliwa, hukua na pia hufa. Wengi pale upendo unapoyumba ndo wanagundua mapungufu yao. Mtu anatakiwa aoe/aolewe na mtu anayeendana na mipango yako ya maisha, sio mmoja ana mpango wa kwenda kuishi mbeya na mwingine anataka abaki Dar... Yote haya ni ya kuyasuluhisha ndani ya uchumba.
Ishu ya feminism pia inawaharibu wanawake wengi sana. Wanawake tusijidanganye, hatuwezi kua sawa na wanaume. Ndio una elimu yako na kazi yako ata kama unaingiza kipato zaidi ya mwanaume inabidi umpe heshima yake mume wako. Mwache mwanaume awe kichwa... Usimlinganishe na wanaume wengine na husimfanye akajiona hana thamani. Kama tunavyopenda kusifiwa, wanaume nao wanapenda hivyo. Ukimaliza tendo na mwenza wako msifie kwa kazi aliyofanya ata kama unajua siku hiyo kachemsha... Kesho yake ataongeza juhudi.

Kwa wanaume walio kwenye ndoa,,, ukimshindwa huyo ulienaye una uhakika gani huyo unaetaka kumchukua atakua tofauti?
 
Suala la ndoa ni elimu pana ambayo kila mtu anaielewa tofauti. Cha msingi ni kuishi kulingana na jinsi utaratibu huo ulivyo ikishindikana basi. Haiwezekani na haitawezekana uishi maisha ya jehanam Ukiwa duniani kisa unavumilia. Umkosee muumba wako na ukaikose pepo, hayo maisha ya furaha utaishi wapi? Si wanaume wala wanawake wote wanaingia ilimradi tu waonekane wameolewa! Taabu tupu!
 
Binafisi nikweli ndoa za zamani zili dumu nikisema mazingira ya kipindi iko yali luhusu,unakuta mwanamke tangu aolewe anashikwa kiuno na mmewe pekee ila nambie saivi hali ilivo.kwa wanaume sasa ndio usiseme.Kipindi iki ndoa zina changamoto kupita kiasi.

Kiukweli tuache kufalijiana ndoa za kweli ndio zinaishia.

Wanao sema ndoa raha waulize wamepitia matatizo mangapi bado wakaiona ndoa ni raha.

Kwa ufupi naamini miaka ijayo mtu mwenye akili timamu(ukiacha hawa wanao funga ndoa kuepuka dhambi ya zinaa) atakae kua kwenye ndoa atashangaza sana.
Hahaha umenichekesha
 
Ndoa ni tendo la kiimani hivyo wanandoa inawapasa kumtanguliza Mungu mbele ili aweze kuilinda ndoa yao. Vijana wa siku hizi wakimaliza kuoana hawamuhusishi tena Mungu wao,, Hawaendi Misikitini wala Makanisani. Hawasali pamaoja! Sala ndio nguzo pekee ya ndoa! Muwekeni Mungu wenu mbele nanyi mtaishi miaka mingi kwa raha daima!

Pia vijana waache kuhusisha maisha ya ndoa na mambo ya social networks.. Social networks ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga ndoa nyingi! Wana ndoa wanapotaka kuiga mambo ya watu wengine wanayoyaona kwenye social network ndio tatizo linapoanzia hapo. Mdada anaona mwenzake kila siku katolewa outing na mumewe naye anataka mumewe amfanyie vivyo hivyo bila kujali mpangilio wao wa kimaisha yeye na mwenza wake!
Ushauri mzuri sana huu. Asante
 
Uliyoyasema yote ni kweli. Mi nadhani tatizo kubwa watu wanakimbilia ndoa labda kwasababu wanaona wenzao wameoa/kuolewa au wamehimizwa na familia au kupenda sifa tu hasa kwa wadada au pia kuona umri umeenda. Nimesoma vitabu vichache vya ndoa na kufahamu kua sababu pekee ya kumfanya mtu aingie kwenye ndoa ni utayari wa kuingia kwenye ndoa na si vinginevyo.
Hamna ndoa iliyokosa changamoto, ata kama hao watu walipendana kiasi gani... Uvumilivu ndo unafanya ndoa nyingi zidumu.
Pia upendo usiwe kigezo pekee cha kuingia kwenye ndoa. Upendo huzaliwa, hukua na pia hufa. Wengi pale upendo unapoyumba ndo wanagundua mapungufu yao. Mtu anatakiwa aoe/aolewe na mtu anayeendana na mipango yako ya maisha, sio mmoja ana mpango wa kwenda kuishi mbeya na mwingine anataka abaki Dar... Yote haya ni ya kuyasuluhisha ndani ya uchumba.
Ishu ya feminism pia inawaharibu wanawake wengi sana. Wanawake tusijidanganye, hatuwezi kua sawa na wanaume. Ndio una elimu yako na kazi yako ata kama unaingiza kipato zaidi ya mwanaume inabidi umpe heshima yake mume wako. Mwache mwanaume awe kichwa... Usimlinganishe na wanaume wengine na husimfanye akajiona hana thamani. Kama tunavyopenda kusifiwa, wanaume nao wanapenda hivyo. Ukimaliza tendo na mwenza wako msifie kwa kazi aliyofanya ata kama unajua siku hiyo kachemsha... Kesho yake ataongeza juhudi.

Kwa wanaume walio kwenye ndoa,,, ukimshindwa huyo ulienaye una uhakika gani huyo unaetaka kumchukua atakua tofauti?
Ushauri mzuri dada asante. Vijana tuuzingatie
 
Wanandoa hasa wanawake hawataki kujikubali wanapenda maonyesho anataka awe juu zaidi ya wanawake wote vitu ambavyo havimsaidii moja kwa moja social netwek ndo inawaharibu imefikia mahali me nimepiga marufuku insta na fb ili kunusuru ndoa maana ilishakuwa ICU imekata kauli kauli.ndoa ya miaka 9 nilikuwa naivunja ndani ya siku moja!
Mwanamke anakwambia ona kina fulani wanavyoishi vizuri sijui mara hivi,huwezi kujua ndoa za watu ndani wanaishi vipi ni sisi wa nje ndo tunafurahia maisha ya ndoa ya watu wengine ila wao hawana raha ndani inafikia wanataka kuwekeana hata sumu
 
Dah! Hadi sumu? Kuna mtu aliwahi kuniambia kuna wanandoa wanaombeana hadi vifo ili wawe huru .
 
nani anataka kuishi na Malaya aje aletewe miwaya ndani!! wacha waachane tu.

na usiseme wanawake wanalipiza, sema wanaenda kutafuta furaha yao. unafikiri ni maboksi hawana hisia au wana mioyo ya chuma? aishi maisha yake kumlilia MTU ambaye hamjali? acha tu watafute furaha nao.

ukisema tu ndoa ina miaka thelathini wala hunivutii, hadi nijue ni ndoa kweli ama vepee! sio sifa kusema tu ndoa INA muda mrefu wakati wahusika hawafurahii, mnafurahia nyie watazamaji!
As if kukaa muda mrefu kwenye ndoa means anything.

Kuna ndugu yangu ndoa ina miaka 15. Lakini kutwa analalamika mume wake anavyomnyanyasa (kupigwa na kutukanwa).

Yeye furaha yake ni kuwa kakaa kwenye ndoa miaka mingi...ni role model wetu..... Hahaha.

Kuna siku waligombana na mumewe nikiwepo. Ile scenario mpaka leo nikiikumbuka huwa siamini na hunipa hofu sana.

Mdada akaniambia hapo ilikuwa kawaida tu. Inakuwaga timbwili kweli kweli, mpaka watoto hujificha...mh

Ila haya mambo naona hutegemea na mtu pia. Kuna watu wastahimilivu sana.
 
Uliyoyasema yote ni kweli. Mi nadhani tatizo kubwa watu wanakimbilia ndoa labda kwasababu wanaona wenzao wameoa/kuolewa au wamehimizwa na familia au kupenda sifa tu hasa kwa wadada au pia kuona umri umeenda. Nimesoma vitabu vichache vya ndoa na kufahamu kua sababu pekee ya kumfanya mtu aingie kwenye ndoa ni utayari wa kuingia kwenye ndoa na si vinginevyo.
Hamna ndoa iliyokosa changamoto, ata kama hao watu walipendana kiasi gani... Uvumilivu ndo unafanya ndoa nyingi zidumu.
Pia upendo usiwe kigezo pekee cha kuingia kwenye ndoa. Upendo huzaliwa, hukua na pia hufa. Wengi pale upendo unapoyumba ndo wanagundua mapungufu yao. Mtu anatakiwa aoe/aolewe na mtu anayeendana na mipango yako ya maisha, sio mmoja ana mpango wa kwenda kuishi mbeya na mwingine anataka abaki Dar... Yote haya ni ya kuyasuluhisha ndani ya uchumba.
Ishu ya feminism pia inawaharibu wanawake wengi sana. Wanawake tusijidanganye, hatuwezi kua sawa na wanaume. Ndio una elimu yako na kazi yako ata kama unaingiza kipato zaidi ya mwanaume inabidi umpe heshima yake mume wako. Mwache mwanaume awe kichwa... Usimlinganishe na wanaume wengine na husimfanye akajiona hana thamani. Kama tunavyopenda kusifiwa, wanaume nao wanapenda hivyo. Ukimaliza tendo na mwenza wako msifie kwa kazi aliyofanya ata kama unajua siku hiyo kachemsha... Kesho yake ataongeza juhudi.

Kwa wanaume walio kwenye ndoa,,, ukimshindwa huyo ulienaye una uhakika gani huyo unaetaka kumchukua atakua tofauti?
Ubarikiwe mkuu
 
Nini sababu nyingine zinachangia? Karibu mtoe maoni tuwaandae vijana kabla hawajaingia kwenye ndoa takatifu.
Sababu kuu ndoa za siku hizi ni maigizo unakuta shoga au rafiki ana kauli ndani ya ndoa ya wenzake na kuifanya atakavyo. Pia mashemegi na wakwe nao hawana furaha na ndoa zao huanza fitna kwa ndoa za watoto wao. Bila ya kusahu wadada wengi hutamani mapenzi kama za kwenye tamsilia wakisahau hayo mapenzi ni ya mchezo tu na yameshapangwa.
 
Back
Top Bottom