Mkuu kinachofanya ndoa ziwe ngumu siku hizi ni watu kuingia kwenye ndoa bila kuelewa wanakuwa humo kwa sababu gani? Sasa hivi ukisema uulize mtu kwanini amefunga ndoa ni wachache sana watakaokupa majibu ya kuridhisha nilichokiona kwa muda niliokaa kwenye ndoa ni yafuatayo
1. Wanandoa wanajua ni furaha siku zote hakuna nyakati za huzuni, hasira na maumivu
2. Wanafuata mapenzi kwenye ndoa na sio kujenga familia nzuri
3. Hawaelewi kuwa mtu unaeenda kuishi naye ana mapungufu na anaweza kukosea na unapaswa kusamehe over and over bila kuweka kinyongo
4. Watu wanategeana kufanya majukumu yao mfano kuhudumia familia, na kuheshimiana
5. Watu wanakata tamaa mapema sana linapotokea tatizo hawakai kusolve au kufight ndoa iendelee kuwepo
Hayo ndo niliyoyaona na nimeyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa nyumba ina amani na ninaimani nitazeeka na mzee tukiwa pamoja in one piece.