Kulikoni Mbona rais Samia, ameanza kujitenga Kimataifa?

Mto wa mbu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2021
Posts
4,472
Reaction score
11,252
Hali si nzuri Kwa mama Samia, Alipoingia madarakani Samia alikuja na kauli ya kuifungua nchi, alijaribu kurejesha taswira ya Tanzania kwenye mstari.

Alisafiri nchi za ulaya kama zote na Marekani. Alikalibishwa ikulu ya white house na kupokelewa na Kamala. Vice president Kalama alimtembelea Samia Dar es salaam. Kwakweli Samia aling'ara sana Kimataifa.

Sahivi Samia hasafiri Tena nje, haendi kwenye makongamano ya Kimataifa, akisafiri anaenda Msumbiji na Madagascar.

Ziara za Ulaya na Marekani zimekata kabisa.

Tunakutumia salamu Samia Ile zomea zomea uliyokutana nayo Marekani 2021, Hadi ukapitishwa uhani ilkuwa ni Cha mtoto, sahivi ukikanyaga Marekani, Uingereza,Canada na German utakipata Cha moto.

By the way mbona Samia amejitenga Kimataifa?

Mto wa mbu,
Illinois -USA
 
Hakuna anayetaka kuwa mwenyeji wa muuaji!
 
Iran,urusi,china na wajomba zake pamoja na mumewe jakaya wanampa matumaini alivyo mjinga
 
Mkuu huku kuna uchaguzi. Pingine hujui kwani uko mbali.
 
Chawa Lucas Mwashambwa tunaomba majibu. Au mama kaishiwa nauli?
 
Strong contender akiwa Salum Mwalimu

HE, President Salum Mwalimu😡, hawezi mshinda hata the weakest incumbent President
Hivi ccm wanaweza kukubali kufanya debate?
 
Izo nchi ata msaada wa kibajeti wa $40m hawatoi
Ni maskini sana unahitaji msaada ?
Au umeshindwa kusimamia Rasilimali zako za Nchi ?
Et $40m wao wanachuma mtini.
Ndio maana masharti na mikataba mibovu haiishi nchi hii.
 
Eti Secretary Rubio, apoteze muda kumkalibisha huyo mrekodi video za utupu wakosoaji wake

Ila walimpokea kwa heshima Benjamin Mileikowsy "Netanyahu" na akapewa hadi nafasi ya kuhutubia Congress licha ya kuwa ni mtu anaye commit genocide na ana arrest warrant juu ya kichwa chake kutoka ICC.

Vipi kuhusu Ishu ya Epstein wamefika wapi?
 
Hapo mnaoneaaaa!!! Chama Kiko kwenye maandalizi ya Uchaguzi ambapo yeye kama Mwenyekiti na Mgombea lazima awepo.

Jambo jingine ni kwamba, pamoja na changamoto zilizopo kwenye utawala wake, yeye pia ni binadamu, tukosoe kwa staha hata kama kelele tunazotoa hazileti majibu tunayotaka. Urais ni mzigo japo ni mtamu. Lakini pia Pole pole keshasema kazungukwa.na manyang'au. Wakati mwingine tunamlaumu bure. Tuombe sana Mungu atusaidie jamani.
 
Nadhani bado hujamfahamu rais Donald Trump WA marekani rais ambaye hakujibu congratulations ya Samia pale aliposhinda URAIS dhidi ya Kamala . Bwana eee chezea vitu vingine na sio Yule jamaa . Samia NI heri aendelee kubaki nyumbani kuliko aibu ambayo itamkuta siku akienda USA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…