Kulikoni itv baraza la Eid Tanga

Kulikoni itv baraza la Eid Tanga

Mwamba2025

Member
Joined
Aug 4, 2018
Posts
24
Reaction score
1
Niko hapa natazama Baraza la Eid linaloendelea jijini Tanga katika hoteli ya Tanga Beach Hotel. Baraza hili linaonyeshwa na televisheni kubwa zote TBC1, Star TV na Channel 10. ITV muda huu inaonyesha filamu ya kinigeria. Hivi ITV hawaoni umuhimu wa Baraza la Eid kwa watazamaji waislamu? Kwa kutorushwa kwa Baraza hili, ITV inatuma ujumbe gani kwa watazamaji wake waislamu? ITV ikituhumiwa kwa ubaguzi, itakuwa ni sawa?
 
Tosheka na TBC, vipi kuhusu Azamu na ZBC ? Mambo mengine si lazima televisheni zote zikarushe kwani hayana umuhimu kwa watu wote kama taifa zima
 
ITV=Televisheni ya taifa?
Kurusha live kwa angalau lisaa limoja tu nje ya mkoa uliojengwa mitambo ya TV husika ni mamilioni.
Je, umechangia?
Je, hao wanaorusha unajua wanarusha kwa mkataba upi?
 
Hili linajulikana, Hata hizo TV nyingine hazikuwa zinarusha mubashara. Walijiunga na TBC1. Hoja hapa ni hii: hivi hili tukio halikuwa na umuhimu kiasi hicho?
 
Hilo nalo la kulalamika? Kuna kipindi meli ilizama, television yako pendwa iliweka kipindi gani vile....?
 
TBC1 ni haki yako
Channel 10 vilevile ila ITV ni private hata wamuonyeshe Trump anacheza mpira wewe inakuhusu nini?
Hiyo hotel inaitwaje???
Kuwa private, hakuondoi wajibu wa msingi wa kuwatumikia watazamaji. Upo wajibu wa kijamii kwa kila taasisi binafsi, na kwa vyombo vya habari ndio wana wajibu mkubwa sana.
 
Hilo nalo la kulalamika? Kuna kipindi meli ilizama, television yako pendwa iliweka kipindi gani vile....?
Kosa moja halihalalishi kosa lingine. Na hapa nazungumzia kituo kingine, sio hicho unachozungumzia wewe. Sina maslahi binafsi kwa vituo vyote. Ni hoja, ijibu kwa hoja.
 
Kuwa private, hakuondoi wajibu wa msingi wa kuwatumikia watazamaji. Upo wajibu wa kijamii kwa kila taasisi binafsi, na kwa vyombo vya habari ndio wana wajibu mkubwa sana.
Usinichekeshe.
Uko Tanga mjini, kumbe unajali sana baraza la Eid , kwanini usiende kujumuika na wenzio LIVE? Unategemea ITV wakuletee chumbani uone ukiwa na mchepuko. Si muangalie TBCCM?
 
Back
Top Bottom