Kulala na mwanamke kunaleta mikosi?

Kulala na mwanamke kunaleta mikosi?

Labda kulala na mwanamke wakuokota! Lakini kwasisi tuliooa kulala na mkeo ni baraka na Mwenyezi Mungu anabariki mambo yetu! Sijui nyie msiooa labda mtuambie mkilala nao inakuwaje?

Kulala na mke ni ibada
 
Kufanya ngono husababisha kuambukizana kwa baadhi ya roho baina ya mwanaume na mwanamke.

Roho hizo huweza kuwa ni zile chafu mathalani nuksi, mikosi, pepo wachafu au wakati mwingine huweza kuwa ni roho njema.

Wapo wanaotaja kwamba ufanyaji wa ngono husababisha kuambukizana nishati inayosafiri kati ya mwanaume na mwanamke.

Hivyo hilo la nuksi kwa asilimia fulani sio dhana ya uongo isipokuwa hata mwanamke pia anaweza kupata nuksi toka kwa mwanaume.

Na mara zote ngono inayofanywa katika jina la uzinzi au uasherati ndio hupelekea sekeseke lote hili.
 
Ukilala na mwanamke asiyekuwa mkeo ni mikosi kweli.

manking,
Unajua mkosi huo ni upi? Hakuna dini iwayo yoote inayoruhusu uzinzi. Sasa weye watoka tu barabarani, unaokota malapulapu unapeleka makaburini juu ya kaburi la mwenzio ati mnamalizana. We, hiyo ni dhambi na dhambi ni laana na laana huondoa baraka. Mkosi, si kitu kingine bali ni Baraka iliyo ondoka.
 
manking,
Unajua mkosi huo ni upi? Hakuna dini iwayo yoote inayoruhusu uzinzi. Sasa weye watoka tu barabarani, unaokota malapulapu unapeleka makaburini juu ya kaburi la mwenzio ati mnamalizana. We, hiyo ni dhambi na dhambi ni laana na laana huondoa baraka. Mkosi, si kitu kingine bali ni Baraka iliyo ondoka.

Umesema vizur, "DHAMBI" Matokeo yake ni kukosa baraka sasa swali ni baraka zipi unazokosa? ni pamoja na bahati nzur(zawadi) ambazo mwenyzi Mungu angekupa.
 
kuna dada toka nianze kutembea naye nimepata neema kibao na ninaona bora nimuoe japokuwa wengne niliokuwa nao mwanzo waliniletea kweli mikosi hela zinapotea hovyo lakini huyu mpya niliyenaye ndo kwaanza naona baraka kibao kwakweli namshukuru mungu
 
Kwanza niombe radhi kuwa sina nia ya kumnyanyapaa mtu yeyote kwa jinsia yake, rangi yake, kabila lake wala dini yake.

Nimekua nikiona hii dhana ya kuwapo kwa mikosi inayotokana na kulala na mwanamke. kwa mfano katika mipira ya mchangani siku ya match watu walikuwa wakihimizana kutokulala na mwanamke na pale ambapo tulifungwa na kugundulika kuwa mmoja wetu kalala na mwanamke basi lawama zote humuendea.

Babu yangu alikuwa na wake wawili. Lakini siku ambayo kesho yake alikuwa na agenda muhimu alilala chumba chake peke yake. Kwani kila mwanamke alikuwa na chumba chake na pia alikuwa na chumba chake mwenyewe.

Baada ya kufika mjini pia hii dhana nimeikuta. iwe ni katika biashara au kazi au kitu chochote muhimu utasikia watu wanakwambia usichukue mwanamke. na pale ambapo mambo yanaenda ndivyo sivyo utasikia watu wanahoji huyo mwanamke uliye lala naye anagundu.

Mimi sito msomaji wa vitabu vya dini lakini mtu mmoja alinibia dhana hii ina chimbuko kwenye biblia hasa agano la kale na kwenye korwani pia.

Kwayeyote anayefahamu tafadhali tuelimishane.

Hebu read that
 

Attachments

  • 1392398716096.jpg
    1392398716096.jpg
    55.9 KB · Views: 227
Kwa hili namkubali watu8. Watu wanaparamia ngono tu na kutafuta sayansi ndani yake. Ingekuwa hivo kungekuwa na viwango vya kuridhika na mapenzi kama speed mita. Kufanya mapenzi kuna exchanging of spirits (pumzi). Waliolelewa na kufundwa wanajua hiyo.
 
hizi imani huwa zinarudisha nyuma sana watu kwenye maendeleo. mtu mambo hayaendi vizuri badala ya kutafakari kwa kina kujua tatizo na kutafuta suluhisho, anatafuta visingizio. matokeo yake akili zinadumaa kwa imani potofu na kijinga kama hizi.
 
yeah ni mkosi mkubwa pale unapolala na mwanamke asiye halali kwako i.e mkeo maana mnazini na uzinzi ni dhambi na matokeo kukosa baraka hivyo kupata mikosi.
 
Dadafua tafadhali
Kusema tu hivyo haitoshi!

Mkuu utakubaliana na mimi kuwa vitabu vitukufu vya mwenyez Mungu vinaeleza kwamba ndoa inayo tambuliwa kisheria kati ya mume na mke ni takatifu,Kwahiyo kulala na mkeo ni kitu chema. Unapolala na mwanamke asiye mkeo unazini na zinaa ni "DHAMBI" na dhambi ni laana na laana matokeo yake ni kukosa baraka za mwenyez Mungu ambazo ni pamoja na mikosi, ktofanikiwa kwa mambo yako mazuri binafsi yeny kukuletea maendeleo.
 
Mkuu utakubaliana na mimi kuwa vitabu vitukufu vya mwenyez Mungu vinaeleza kwamba ndoa inayo tambuliwa kisheria kati ya mume na mke ni takatifu,Kwahiyo kulala na mkeo ni kitu chema. Unapolala na mwanamke asiye mkeo unazini na zinaa ni "DHAMBI" na dhambi ni laana na laana matokeo yake ni kukosa baraka za mwenyez Mungu ambazo ni pamoja na mikosi, ktofanikiwa kwa mambo yako mazuri binafsi yeny kukuletea maendeleo.

Nakubaliana na wewe ngono nje ya ndoa ni dhambi!

Ukweli utabaki pale, ikitokea mtu akaoana na mtu mwenye asili ya haya tunayozungumza, mikosi itamwandama tu!

Hufanikiwi!

Hata ajali za mara kwa mara, nyingine zinachangiwa na madereva wanaokumbana na wanawake wa aina hii pindi wanapozini usiku na kuamkia kubeba abiria.
 
Back
Top Bottom