Kukosekana kwa ushindani kunafanya tuwe na huduma nyingi mbovu

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
16,494
41,663
Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza maswali kadhaa, ambayo mengi sikuwahi kuyapitia majibu. Kwa mtazamo wangu, nadhani kukosekana kwa ushindani kwenye sekta kadhaa, kunafanya hata upatikanaji wa huduma hasa za kijamii ziwe mbovu/hafifu.

Ushindani ni nyenzo kuu linapokuja swala la huduma bora, pasipokuwa na ushindani, huduma lazima ziwe chini, maana watoa huduma huwa wanabweteka. Hoja zangu nitaziweka kwa kutumia mifano kadhaa:

1. Sekta ya mafuta/petrol

Katika hali ya kutaka kukuza kampuni yake, Mr Ambani aliamua kuja kuwekeza Afrika Mashariki. Kampuni yake ya Relience Industries Limited (RIL) waliwekeza kwenye sekta ya mafuta, chini ya Gulf Africa Petroleum Corp (Gapco).

Malengo ya Mr Ambani ilikuwa ni kulishika soko la Africa Mashariki, inasemekana alikuwa na visima vya mafuta kule kwao India, so aliplan kuuza mafuta kwa bei ya chini, ambayo in long run, ingeleta profitable return. Kwa EA, Gapco walikuwa na matank mengi yenye ujazo mkubwa waliwazidi hata wale wakongwe, pia walikuwa na petro stations za kutosha.

Baada ya kuhisi mission ya Gapco itakuwa tishio kwa soko la makampuni mengine, kilichofuata ni makampuni makubwa kushawishi makampuni mengine madogo, ili watengeneze umoja utakaokuwa na tija kwa makampuni yote ya mafuta (Oil Marketing Companies, OMC's).

Lengo la huu umoja, ni kununua/kuagiza mafuta kwa pamoja toka nje ya nchi, alaf yakifika nchini, wanagawana kulingana na kila mmoja alivyoagiza.

Makampuni madogo yasiyo na uwezo wa kuagiza kiasi kikubwa cha mafuta, hii kwao ikawa ni opportunity nzuri sana maana hata kwa mitaji yao midogo ingekuwa rahisi kuagiza, hivyo ikawa rahisi kukubali. Lakini in reality, makampuni makubwa yalikuwa yanataka kumneutralize Gapco.

Mr Ambani alikuwa against na ili swala, kwake haikumake sense, watu mnaocompete mshirikiane kununua bidhaa na kuregulate bei. Yeye akawa anasisitiza kwamba makampuni yote yapo kwenye competition, na yeye pamoja na kampuni yake wanataka kuwin soko, so kila mtu aendelee kuagiza anapoagizaga, then wakutane sokoni.

Ila wengi wape, Mr. Ambani na Gapco yake, walikuwa peke yao, makampuni mengine yakapitisha huo uhamuzi, kutokea pale around 2015 ikaanzishwa Petroleum Bulk Procurement Agency (PBPA) , then 2016 Mr. Ambani na kampuni yake ya RIL wakaamua kuuza matank na Petro stations zao kwa Total Energy then wakaamsha.

Tokea hapo, kwa kupitia PBPA, mafuta yanaagizwa in bulk, yakifika yanakuwa distributed kwa OMC's, bei inakuwa elekezi kwa wote. Baadae PBPA ikachukuliwa na serikali, na mpaka sasa ipo chini ya serikali.

2. Mitandao ya simu

Sina uhakika na uwepo wa umoja kati ya hizi kampuni za mawasiliano, ila Iko wazi kuna makubaliano ya aina fulani kwenye utendaji kazi wao au mahamuzi yao. Mtandao mmoja ukipandisha gharama, kabla hatujakaa sawa, na wengine nao wanapandisha pia, hivyo huna unapoweza kukimbilia. Unajikuta unalalamika huku unaendelea kutumia.

Lakini endapo pangekuwa na ushindani kibiashara, nadhani gharama zingekuwa zinashuka ili kuvutia wateja. Ila kwasasa ukilalamika, utaishia kuambiwa internet ni anasa au kitu cha ziada.

3. Huduma zinazotolewa na serikali pekee.

Vuta picha leo hii upande wa mawasiliano na internet provider pekee angekuwa TTCL, maisha yangekuwaje? Sasa twende kwenye huduma za maji na umeme, binafsi sielewi mambo mengi kuhusu mipaka ya serikali katika kuhudumia wananchi, ila kwa uelewa wangu mdogo najua serikali inatakiwa kusimamia uendeshwaji wa nchi na ustawi wa raia (correct me if I'm wrong).

Hivi haiwezekani kampuni binafsi kutoa hizi huduma pia, alaf serikali ikabaki kusimamia ubora?

Kuna siku niliona tamko la kuzuia watu wote wenye visima wanaosambaza maji majumbani, why iwe hivyo wakati dhumuni ni kuhakikisha raia wanapata huduma bora? Kwanini serikali isingejikita kusimamia ubora wa hayo maji ili raia wake tusidhurike?

Mpaka leo hii, kuna sehemu hapa Dar bado hawapati maji ya dawasco. Ukienda huko vijijini ndio usiseme.

Tukirudi kwenye umeme, kama kuna kampuni binafsi zinazosambaza umeme wa Sola (hasa vijijini), kwanini serikali isiruhusu na makampuni binafsi kutoa huduma za umeme majumbani? Umeme na maji imekuwa shida mpaka leo hii, kwavile provider pekee ni serikali. Serikali Ina vipaumbele vingi sana, na inafanya mambo yake kwa utaratibu maalum, je lini itaweza kufikia maeneo yote kwa hizi huduma?

Kwenye mfano niliotoa huko juu kuhusu kampuni za simu, leo hii kuna minara mpaka vijijini, na hii ni kutokana na uwepo wa sekta binafsi.

Naamini ushindani au pakiwa na mtoa huduma zaidi ya mmoja, huduma zinaboreshwa kwa namna fulani. Kama nitakuwa sipo sahihi kwa lolote nililoandika huko juu, nipo tayari kujifunza, napenda kupokea mawazo na mitazamo mipya. Ila ushindani ni kitu muhimu sana kwa maslahi mapana ya huduma za kijamii.

Wasalaam,

Analyse
 
Bungeni na serikalini wamejaa wafanyabiashara wa mafuta na zingine kubwakubwa. Lazima watunge sera na sheria zitakazowapendelea. Tanzania nayo ni Oligarchy. Na bado.
Maamuzi na sera hazilengi maslahi ya wengi, tatizo linaanzia hapo
 
Back
Top Bottom