Kukomesha mauaji ya maalbino; tunafanya usanii…? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukomesha mauaji ya maalbino; tunafanya usanii…?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ilumine, Feb 3, 2009.

 1. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuanzia mwaka 2008 wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi limekuwa likiongezeka sana kiasi cha kutufedhehesha wanajamii wote hasa ndugu zetu hawa wanaowindwa. Jamani, sisi ni binadamu, tunawindana sisi kwa sisi, inakuwaje? Simba hawezi hata siku moja kuwinda samba mwenzake, au mbwa mwitu kwa mbwa mwitu. Tunakwenda wapi?
  Serikari imejitahidi kutokaa kimya. Tumesikia hapa na pale viongozi wakionesha juhudi fulanifulani za kujaribu kukomesha mauaji haya.
  Nimekuwa nikijiuliza kila siku, hivi ni watu wangapi hadi sasa walioshitakiwa na kupewa adhabu zao kama vifungo n.k? Sisemi juu ya watu wanaotumwa kwenda kuua; hawa tumesikia wamekamatwa hapa na pale. Je, hawa wauaji ndio hasa wanaotumia viungo hivi au kuna wale wanaowatuma? Nahisi pengine kuna kitu Fulani ambacho si sawa kwani hadi sasa hatujasikia wameshikwa wahusika wenyewe wanaovitumia viungo hivyo. Au kuna watu Fulani wenye heshima zao hapa nchini tunawastahi? Kama mimi sijasikia basi nifahamisheni, ni akina nani? Nina imani sana na Jeshi letu la Polisi, kwani likiamua ‘kufanya kitu’ linaweza.
  Na kwa mtazamo wangu, naona vita hii kukomesha mauaji haya inaendeshwa kisiasa zaidi.
   
Loading...