Kuko wapi Kuhongwa kwa Lissu na Acacia?

Kuko wapi Kuhongwa kwa Lissu na Acacia?

Kuna waovu waliochonga Maneno ya Visa sana ati Tundu Lissu alikuwa anahongwa na Acacia ili kuitetea. Masikini alikuwa akielezea Mtazamo wake tu Kuwa Approach aliyotumia Magufuli itaweza Kusababisha Nchi Kushitakiwa.

Wabunge wa CCM sio wote nao ati wakaanza Kuwazomea Upinzani Kuwa ni mafisadi au Wasaliti ati wao CCM ndio wakombozi wa Nchi! What a joke!

Anyway Nachotaka Kuuliza Hapa ni Kuwa, Kama Tundu Lissu alikuwa Akihongwa na hao Wazungu wa Acacia inakuwaje fedha hizo Mkewe au Chadema hawakuzitoa kukodisha ndege! Yaani Dola 9000 tu walikuwa Hawana. Na hao chadema kama wanahongwa na Acacia mbona hao akina Acacia hawakujikeza kumlipia Tundu Lissu matibabu? Utamwacha mtetezi wako afe?

Hila za Kusingizia watu Wazalendo kuwa ni Wasaliti na Wasaliti kujiita Wazalendo! Mungu anaona. Tundu Lissu hata kama alikuwa ni Bombastic in communication, Alikuwa ni Mtanzania mwenye roho nzuri sana na Mzalendo. Alichotendewa. Malipo yatatolewa kwa laana ya Ajabu kwa Wahusika.
Actually mimi bado na jiuliza usaliti na uadui wa wapinzani ni upi!? Maana maadui nma wasaliti wa kwanza ni wale walio tuingiza kwenye hii mikataba ya Ovyo. Na sijaona hata mmoja akiwekwa ndani au kufilisiwa au kupigwa risasi.
 
Meku ulitaka hao wazungu waite press conference wakutangazie kwamba wanamhudumia Lissu? Wewe huwa unaamini kila ambacho hakisemwi basi hakipo??

Tunachotaka Mungu amponye Lissu na waliompiga risasi watiwe nguvuni... Hizi kombolela zingine hazina maana
Kaka umeandika mbolea tupu, umafia siku zote hufanyika mafichoni, madili yote hufanyika mbali kabisa na camera.

Yanapoharibika mambo ndipo unamuona mtu akiwa kainamisha kichwa chini ameketishwa kwenye kiti cha mahakama fulani.
 
Mkuu mbona unatoa kauli za kama vile Lissu is no longer with us. Lissu yuko hai na imani yangu akitoka huko atakuwa bombastic mara kumi zaidi ya awali.
Still Damu yake ilimwagika! Na iite kisasi na Laana ya Mauti juu ya Wauaji na Waliowatuma na Nyumba zao zote! Asiwepo wa Kusalia
 
You r nothing closer to a preacher, you r an agent of devil in its own manifestation.
Dont you think the devils are those who wanted to Assassinate Lissu, together with their stooges you being one of them? Time will tell who is the devil. Na Ni kitu gani Kimekukasirisha hivyo ghafla, Je unahusika na Kutaka Kumuua Lissu? Maana nakushangaa Ghadhabu inatoka wapi hiyo!
 
serikali ya magufuli imewekeza ktk uwongo, hila na propaganda. think tank take ni bashite, hakuna maendeleo hapo, ni mauaji tu.
 
Hakuna mkombozi ndani ya nchi hii si ccm wala upinzani wote lao moja ni maslahi binafsi...yaani hao akina lissu naamini wamepiga hela ndefu sana ya acacia hilo lipo wazi.
 
Upo sahihi kabisa huwezi kuhongwa uwe simple kiasi kile ..

Maana historian yawahongwaji tunaijua kutoka kula mihogo mpaka kwenda kuishi canada.
Yupo simple kivipi..acha zako watu wanapiga hela sio lazima ujue..au hukuona Biligate
 
chukua tano, hawa Maccm hawakumwelewa Mzalendo kamili Lissu, aliwambia kwanza wajitoe kwenye mahakama za nje za kibiashara vinginevyo tutaumizwa na mikataba ya mazuzu wa kitanzania walioifunga na haya majizi, nyie mkajidai wajanja, ona sasa Nooah zetu zimepotea
Hapo ndio tungeumia zaidi...yaani alikuwa anaongea kitu ambacho yeye mwenyewe anajua hakiwezi kufanyika kuwaaminisha watu kama nyinyi
 
No hata wangetoa Kwa siri Tusingeona Chadema wakihaha kutafuta Usafiri wala Matibabu! Hata Hela za Kuwaweka Nairobi wale wanaomtazama pale wanachangiwa Kanisani!
Hahaaa...hizi ni mbinu tu, wewe unafikiri Lowassa kutoa millioni 500 kwake ni shida?
 
Tundu Lissu anaweza akawa amehongwa. Sasa cha Mke wake kuamua asizitumie hizo fedha kumpeleka Nairobi, inawezekana hela hiyo Lissu hawakumwekea kwenye benki zetu wameweka nje! Maana kwene mabenki ya hapa si serikali itajua na kuuliza Lissu kazipata wapi? Hivyo kama ziko nje siyo rahisi kuzipata haraka kulipia jambo la dharura kama lile. Hivyo hoja yako haiwezi ikawa proof kwamba hakuhongwa. Vivyo hivyo kwa Chadema. Na mkewe anaweza asiwe signatory wa kuweza kuachiwa hela kutoka benki. Mimi nataka Lissu apone.
Aliyosema lisu kuwa sheria hamzifaham mtalitia taifa hasara mbona tyr imeshituka!??

Noah zetu ziko wapi sasa!?
 
Hata angekuwa nazo angewezaje kuzitumia katika mazingira hayo?

Tujikite kumuombea wepesi katika ugonjwa wake ili apone haraka aje kuhudumia familia yake na umma Kwa ujumla.
Aje kuwaumbua waovu... Mungu kumfanya aendelee kuishi anamaana yake mkuu
 
Ccm ni kikundi cha wapigaji tu na wanajuana sema wamejificha chini ya kivuli fake cha uzalendo na sizonje wao!!
 
Dhana ya wapinzani kuungana na wazungu kuhujumu nchi ni mfu, hawana uwezo kupitisha sheria au sera. Kama ni utetezi kisheria hiyo ni kazi.
Aliye saini mikataba mibovu ni nani na kwa masrahi ya nani na nani hapo atakuwa ameungana na wazungu!?!?
 
Kwenye suala la Lissu kwamba alikua anatetea maslahi ya taifa kwa kweli bado napata shida sana kukubali. Maana sijui ni maslahi gani ya taifa aliyokua anayatetea? Labda mniambie maslahi ya kisiasa ntakubali. Na katika hili nadhani aliamua kupigana vita ambayo alijua ama hakujua mwisho wake ni nn?

By the way, mungu amponye arudi kwenye harakati zake.
Ukweli wa lisu mbona umeshajifhirisha!?

Noah zetu ziko wapi!???
 
Katika watu walioumchafua uongozi wa raisi magufuli ni huyu ni bashite ajue hata tuliokuwa upande wa raisi sasa hivi roho zetu zimeingia ganzi kwa kweli
 
Back
Top Bottom