Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,268
- 17,097
Hawawezi kumuita muda umeisha na Kawawa hayupo.....Tingatinga wamelibwaga....Nyerere hayupo...so Kolimbanization is not possible
hongera Mh. Sumaye wakikuita kataa waambie uko busy, wakikusumbua amia Chadema
Wakati huo huo eti kuna watu wanashabikia hicho chama. Hivi ukiambiwa simba huyo, anakula watu utaendelea kumchezea? Nawaonea huruma wale wanaoshabikia ccm wakati wao ni wanyonge!
Kukemea ufisadi kwamponza Sumaye
Na Tumaini Makene
Kauli ya tahadhari kuwataka Watanzania wawe makini katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu, wasichague watoa rushwa na mafisadi, iliyotolewa na Waziri Mkuu mstaafu Bw Frederick sumaye inaelekea kumgharimu baada ya kuwepo taarifa kwamba imekera baadhi ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na sasa wanapanga kumchukulia hatua.
Vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya CCM vimeliambiua Majira kuwa baadhi ya vigogo hao wanalalamika na kutaka Sumaye aitwe na kuhojiwa na vikao vya juu vya chama hicho kwa madai kuwa matamshi yake yamekidhalilisha chama hicho.
Hivi karibuni Sumaye, ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka kumi mfululizo chini ya serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa, alinukuliwa na vyombo vya habari akitoa angalizo kuwataka wananchi kuwa makini wasichague viongozi wanaotoa rushwa ili washinde uchaguzi kwaniu hawataweza kujali matatizo yao wakishaingia madarakani.
……..Chanzo chetu kimedokeza kuwa kauli hiyo ya Sumaye imewakera baadhi vigogo wa CCM huku wengine wakidai kuwa kwa nafasi yake ndani ya chama, Sumaye hakupaswa kjukemea jambo hilo hadharani ambalo CCM imekuwa ikiandamwa nalo..….
Habari zaidi ktk Majira ya leo.
akiitwa tu na ccm.....watz tuandamane na tumpoongeze na tumpe heshima ya udaktari..........

Sijaona mahali ambapo Sumaye kataja sisiemu jamani. Kumwita ni kumuonea!
ndugu hukusoma hesabu za mafumbo, Sumaye katumia lugha ya mafumbo wakati anajua kwa ukweli kwamba maneno aliyotumia katika mafumbo yake ndiyo yaliyokipa misukosuko chama chake kwa takribani miaka 3.