Kukemea ufisadi kwamponza Sumaye

Sumaye ni mpuuzi na mtu anayetaka sifa zisizo na maana!! Alipewa 10 good years za kuleta positive impact kwenye maisha ya watanzania, lakini akashindwa. Leo hii analeta ujinga wa kunyooshea wenzake vidole. Miaka kumi inatosha kabisa kwa kiongozi makini kuwakomboa watu wake kutoka kwenye lindi la umasikini uliopita kipimo cha utu walionao watanzania, lakini aliishia kuwa mzigo na anaendelea kuwa mzigo kwa watanzania kwa kiinua mgongo tunachompa kila mwezi.

Leo hii anazungumzia kuongezeka kwa gap kati ya masikini na matajiri, huku mfano mdogo tu wa matumizi mabaya ya fadha wakati wa kipindi chake....alikwenda nchini Kenya kwa ziara ya siku 3 na kutumia zaidi ya Tsh. milioni mia tano.

Wakati mwingine nakubaliana na Mh. Rais Kikwete anaposema kuna baadhi ya wastaafu ambao wakati wa vipindi vyao hawakufanya lolote lakini leo hii ndo wa kwanza kuwanyooshea vidole wenzao waliopo madarakani....ambao yeye anaona ni kama wivu na roho mbaya waliyonayo wastaafu hao!!
 
lkn tukumbuke huyu ndiye rais mpya ajaye atapambana na richmonduli na mmjoka wa mdimu,hivyo ni vema tukamsikiliza
 
Sumaye ni mpuuzi na mtu anayetaka sifa zisizo na maana!! Alipewa 10 good years za kuleta positive impact kwenye maisha ya watanzania, lakini akashindwa. Leo hii analeta ujinga wa kunyooshea wenzake vidole. Miaka kumi inatosha kabisa kwa kiongozi makini kuwakomboa watu wake kutoka kwenye lindi la umasikini uliopita kipimo cha utu walionao watanzania, lakini aliishia kuwa mzigo na anaendelea kuwa mzigo kwa watanzania kwa kiinua mgongo tunachompa kila mwezi.

Leo hii anazungumzia kuongezeka kwa gap kati ya masikini na matajiri, huku mfano mdogo tu wa matumizi mabaya ya fadha wakati wa kipindi chake....alikwenda nchini Kenya kwa ziara ya siku 3 na kutumia zaidi ya Tsh. milioni mia tano.

Wakati mwingine nakubaliana na Mh. Rais Kikwete anaposema kuna baadhi ya wastaafu ambao wakati wa vipindi vyao hawakufanya lolote lakini leo hii ndo wa kwanza kuwanyooshea vidole wenzao waliopo madarakani....ambao yeye anaona ni kama wivu na roho mbaya waliyonayo wastaafu hao!!


Rafiki unamaanisha kama mtu hakufanya lolote katika kipindi chache asiseme ubaya unaonyemelea nchi. Na je katika kipidi chao hamkuona uchumi ukipanda. Wengi wenye mtizamo chanya walitambua nchi ilikuwa inaelekea wapi!!!.

Karagabao, nyie msikilize Kikwete wenu!!!!!!!
 
Sumaye ni mpuuzi na mtu anayetaka sifa zisizo na maana!! Alipewa 10 good years za kuleta positive impact kwenye maisha ya watanzania, lakini akashindwa. Leo hii analeta ujinga wa kunyooshea wenzake vidole. Miaka kumi inatosha kabisa kwa kiongozi makini kuwakomboa watu wake kutoka kwenye lindi la umasikini uliopita kipimo cha utu walionao watanzania, lakini aliishia kuwa mzigo na anaendelea kuwa mzigo kwa watanzania kwa kiinua mgongo tunachompa kila mwezi.

Leo hii anazungumzia kuongezeka kwa gap kati ya masikini na matajiri, huku mfano mdogo tu wa matumizi mabaya ya fadha wakati wa kipindi chake....alikwenda nchini Kenya kwa ziara ya siku 3 na kutumia zaidi ya Tsh. milioni mia tano.

Wakati mwingine nakubaliana na Mh. Rais Kikwete anaposema kuna baadhi ya wastaafu ambao wakati wa vipindi vyao hawakufanya lolote lakini leo hii ndo wa kwanza kuwanyooshea vidole wenzao waliopo madarakani....ambao yeye anaona ni kama wivu na roho mbaya waliyonayo wastaafu hao!!
Ukiona hata mpuuzi anauona upuuzi basi huo upuuzi umezidi viwango vya upuuzi. Basi tusimnyime mpuuzi kuusemea upuuzi anaouona.
 
Huyu ni mnafiki wa kutupwa, ufisadi wake wa mashamba na viwanja kila kona ya nchi asifikiri hatuujui. Pia nakumbuka kauli yake aliyoitoa Moshi mjini mwanzoni wa miaka ya 2000 kuhusiana na wafanyabiashara, mafanikio na kuisapoti CCM.

Asijefikiri kwamba ile shahada yake ya Harvard ndio itamfanya aonekane mwerevu, kwani hata siri ya shahada ile tunaifahamu.

Anatia aibu na unafiki wake, watu wengine bwana!
 
Mwaka jana wananchi wa mvomero walishtaki kwa jk wakati wa kampeni,sumaye na jeetu patel wamehodhi maekari ya mashamba wanawakodishia walalahoi kwa sh 50 000 pia kuna yale ya kibaigwa mpaka ilibidi mkapa amtetee.alipoingia madarakani 1990 yeye ndie akajikopesha pesa toka ppf bila ya wachangiaji wa mfuko kujua.FISADI TUU HUYU HANA LOLOTE,HIZO NI KAMPENI ZA URAISI 2015
 
Mimi nafikili tusimubeze pamoja na mambo aliyoyafanya katika utawala wake lakini nadhani anacho sema si cha kubeza yaliyo pita si dwele tugange yajayo kwani mmesahau kama alikwenda kuongeza elimu US? na Miaka ya jana sio ya leo kuna utofauti mkubwa wa uelewa KATI YA KIPINDI KILE NA SASA HATA VIJANA WAMEELIMIKA SANA JAMANI.
 
Anatafuta attention katika jamii,hamna jipya Tanzania inaweza kupata toka kwake.,
 
Jamani hivi nyie ni watu wa jana au wa leo?

I'd careless alichofanya Sumaye nyuma I care much about now and the future.

Kama Sumaye alikuwa au mpaka sasa ni muovu hakutengue alichosema kuhusu ufisadi....

Angesema kama Tatizo la Tanzania si ufisadi tungesemaje?

Hii vita tutashinda na amini usiamini Dr.Slaa na sisi tunamafanikio kiasi ni kuendelea kukaza kamba.

Kwa kuwa tumeweza kuchange tune kiasi ,mpaka sasa watu wanakubali katiba ibadilishe,wanakubali ufisadi ndio tatizo ,na watakubali mengi,kama malengo ya upinzani yanalazimishwa kufanyiwa kazi basi upinzani unatawala ahahaaaaaaaaaa
 
Kwani Sumaye ni fisadi, labda hamelewi maana ya fisadi. Fisadi ni binaadamu aliyefikia hali mbaya sana ya afya ya ubongo na akili kiasi cha kufananishwa na Shatwani. Mzinzi, jambazi, muuaji, mwizi, mlaruswa, asiyetosheka na chochote, mwenye tamaa isiyoelezeka. Utaona kwamba kama binaadamu amekuwa fisadi, maro nyingi ni mshirikina mwenye kuweza hata kula nyama ya mwanae mpendwa. Sasa neno fisadi si la mchezo hata kidogo.

Hebu tuone mfano wa fisadi katika Least Developed Countries:

1. Kiongozi ambaye hana uchungu na nchi yake kiasi cha kuingia mkataba wa aina yeyote ile ambao anajinufaisha binafsi kwa kuliletea taifa hasara kubwa sana. Mfano mrahaba wa madini asilimia tatu na ishirini za kwake.
2. Kiongozi mshirikina mwenye kuua nduguze kwa ajili ya madaraka.
3. Kiongozi asiye na kiasi, mbinafsi, mwenye kujilimbikizia mali hata kama itaoza, bilu kujali waliomzunguka na shida zao (Kama kuna mtanzania kwenye hii kampuni inayodai Tanesco, ni mfano mzuri)
4. Kiongozi anayeabudu mashetani na ushetani. (walala makaburini).

hawa wanakuwa wamepoteza kabisa "guilty conciousness" na hivyo huwa na mithili ya hayawani. neno fisadi si mchezo bwana, hawaendi mbinguni ng'o, kama vitabu vya mwenyezi Mungu vinavyosema.

Hawana utu, hawajui haki, sio wakweli wanaweza kuuza hata wake zao. Kwa kifupi hamna maneno mazuri zaidi ya kufananishwa na shetani aliyevaa mwili wa mwanadamu. Afrika ina viongozi wa namna hii? kama wapo tumekwisha.
 
napata shaaka na maneno ya huyu bwana tegemea na vitendo vyake..nahisi wachache wanamjua lakni sidhan kama kuna tofauti kubwa sana na lowassa yawezekana lowassa aliwahi ufisadi akiwa waziri yeye akaanza kukamua akiwa waziri mkuu..kazi ipo

tanzania yetu
 
Hakuwa fisadi mkuu. Ni mtandao wa kikwete ukiongozwa na EL ndo walikuwa wanamchafua. Pia walimchafua Dr. Salim kua alikua member wa Hizib na alishiriki kumuua Mzee Karume. Hivi umeshtukia jinsi EL anavyoanza kujipigia campaign kwa ajili ya 2015 kiana? Naona hata gazeti la Mwana halisi limekua likimsafisha kiaina. Kweli pesa hununua haki!
 
Sumaye akerwa uchumi kuacha kando maskini


*Asema ni hatari kwa utulivu wa nchi

Na Tumaini Makene

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Bw. Frederick Sumaye amesema kuwa takwimu za ukuaji wa uchumi ambazo hazijidhihirishi katika hali
chanya miongoni mwa wananchi wengi maskini hauna maana, kwani unaweza kuwa unakua lakini uko mikononi mwa mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu wachache wabinafsi.

Amesema kuwa watu maskini wanapoachwa pembeni huku ikisemwa 'shauri yao' kutokana na watu wenye mamlaka kuendekeza ubinafsi badala ya kutumikia umma wa Watanzania, ni hatari kwa utulivu wa nchi.

Bw. Sumaye, aliyasema hayo jana katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Pungu, akiwaasa vijana hao kujiandaa kuwa watumishi wa umma wa Watanzania maskini wanaolipia masomo yao kupitia kodi.

Huku akishangiliwa na wanafunzi, waalimu, wafanyakazi na wageni waalikwa, Bw. Sumaye alisema kuwa moyo wa upendo wa watu wanaonufaika na jasho la walipa kodi maskini wa Tanzania kuutumikia umma unazidi kupotea badala yake 'unajengeka moyo wa ubinafsi'.

"Sijui wangapi wanajua umuhimu wa mahafali haya ya leo...ukiwauliza vijana watasema majibu tofauti...wapo watakaosema wanafurahi kumaliza kuachana na mwalimu fulani, wapo watakosema kuwa wameachana na somo fulani...hivi kuna mtu hata mmoja amefikiria baada ya hapa itakuwaje.

"Ni kipindi cha kuonesha mavuno baada ya shamba, tunatumaini kuwa wahitimu wa leo wanayo mavuno ya kuonesha mara fursa itakapofika...lakini ni vyema mkajua kuwa kuhitimu kwako maana yake unategemewa kuwa kioo au msaada mkubwa kwa jamii inayokuzunguka.

"Unapaswa kutambua kuwa kuna Watanzania wana maisha magumu kiasi kwamba hawana viatu vya kusitiri miguu yao, chakula chao cha siku ni shida. Wengi wakiulizwa nani kawasaidia hapo walipofika mtasema ni serikali...lakini ukweli ni kuwa ni walipa kodi maskini, wamejitoa kuwasomesha ili msaidie kutatua matatizo yao," alisema Bw. Sumaye na kuongeza.

"Watanzania wanatakiwa watoke katika umaskini, itakuwa ni kosa tukijijali wenyewe na kuisahau jamii...siku hizi moyo wa upendo wa kutumikia umma unapungua, badala yake unajengeka moyo wa ubinafsi sana, watu maskini wanaachwa pembeni ikisemwa kuwa ni shauri yao.

"Hali hii ni hatari sana kwa utulivu wa nchi yetu...hata kelele hizi zinazopigwa juu ya ufisadi, wizi, rushwa, ushirikina, mauaji ya kutisha ni matunda ya ubinafsi, moyo usiojali wengine. Ni kweli kuwa uchumi wa nchi yetu unakua vizuri, lakini ukuaji wa uchumi uonekane katika hali chanya ya wananchi walio wengi."

Bw. Sumaye ambaye ni waziri mkuu mstaafu pekee mpaka sasa aliyewahi kutumikia vipindi viwili vya miaka mitano mfululizo wakati wa serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, alisema kuwa uchumi unaweza kukua lakini ukawa mikononi mwa mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu wachache.

Alisema kimsingi hapigi vita utajiri, wala kuwaonea wivu wenye utajiri, bali anawaonea huruma wenye maisha duni, waliojitoa maisha yao, kwa njia ya kulipa kodi, kuwasaidia baadhi ya watu, hususan wenye mamlaka hapo walipo.

Alisema Watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya maisha magumu, umaskini uliokithiri, ujambazi, rushwa, ufisadi unaoikumba jamii nzima na kuiathiri, hasa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa.

"Ukuaji wa uchumi unaweza kuwepo kwa kundi la watu wachache au mtu mmoja...ni hatari...tiba ni kuwatumikia wananchi kwanza kabla ya nafsi zetu...tuwe na moyo wa upendo kutumikia binadamu wenzako kwanza...umuhimu wako utakuja tu ukijitoa kutumikia wenzako hasa wenye hali duni.

"Kuna msemo mmoja wa Kiingereza unasema it is nice to be important but it is more important to be nice (ni vizuri kuwa mtu muhimu lakini ni muhimu sana kuwa mtu mwema). Sipigi vita utajiri la hasha, siwaonei wivu wenye utajiri wao, nawaonea huruma wenye hali duni waliojitoa maisha yao," alisema Bw. Sumaye.

Akiwatakia kila la heri na yote mema ya maisha wahitimu kwa ajili ya kuwatumikia wananchi huko waendako, Bw. Sumaye aliipongeza serikali kwa kujitahidi kuboresha sekta ya elimu, ambayo alisema ndiyo nyezo ya kupambana katika ulimwengu usiokuwa na huruma wa maendeleo ya sayansi.

Aliongeza kuwa shule ni sawa na karakana ya maisha kwa mwanadamu, ikimsaidia kujichongea mitambo ya kuendesha maisha yake mwenyewe, ingawa itategemea anaamua kujichongea mtambo wa aina gani anapokuwa amepata fursa ya kuwa darasani kusoma.

"Naipongeza serikali kwa kutoa kipaumbele kwa elimu kwa mafanikio yaliyofikiwa...elimu ni tofauti kabisa na huduma zingine za jamii...ni uzima wa maisha yenye maana kwako na jamii inayokuzunguka...umuhimu wake hauna mjadala, nchi iliyo nyuma kielimu haiwezi kushindana...

"Ni muhimu tukajielekeza kutoa elimu bora badala ya bora elimu ili kushindana katika ulimwengu wa utandawazi, serikali ihakikishe kuwa elimu inayotolewa inakidhi viwango vinavyokubalika kimataifa. Tusitengeneze viwango vyetu wenyewe kujiridhisha.

"Imekuwa kawaida sasa kuona katika taarifa za habari watoto wetu wamerudia mtindo wa kukaa sakafuni, kwenye vumbi huku wakiandikia magotini au kwenye migongo ya wenzao. Hapo hatutengenezi elimu ya viwango vya kimataifa, bali vya kwetu sisi wenyewe...haya ni mambo ya kuaibisha kabisa elimu yetu, ni vyema serikali ikayafanyia kazi.

"Mtaalamu mmoja alisema kama unafikiri elimu ni ghali jaribu ujinga...walimu Nyerere alikuwa akimfananisha mtu aliyekwenda chuo kikuu sawa na mtu aliyepewa chakula chote cha kijiji ili aende akatafute chakula cha kutosha kijiji cha jirani kisha alete...msiwasaliti Watanzania," alisema Bw. Sumaye.

Mapema Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Bw. Rukonge Mweru alisema kuwa moja ya changamoto wanazokabiliana nazo ni 'uvamizi' wa mipaka ya shule, hali ambayo mbali ya kumega eneo la shule pia inatishia ufanisi katika masuala kama vile kilimo, kama ilivyokuwa enzi za nyuma na kuhatarisha usalama na mali za wanafunzi na shule.

Wanafunzi wahitimu katika risala yao walirudia kero hizo, ikiwemo hiyo ya uvamizi wa eneo la shule, tatizo la maji, vitendea kazi (kama vile vitabu, vifaa vya maabara), uchakavu wa majengo na upungufu wa dawa katika zahanati ya shule.




6 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... mheshimiwa mstaafu ni kweli hayo maneno yanatoka moyoni mwako? hongera sana kwa kuyajua hayo baada ya kutoka madarakani. au ulikuwa unayajua hayo kabla? hongera sana. hongera sana.hongera sana.
January 28, 2011 12:35 AM
blank.gif

Anonymous said... Hivi unampa hongera ya nini huyu,anazungumzia UFISADI looo maajabu na vituko vya wanasiasa wa Bongo,huyu mzee alikuwa Waziri Mkuu enzi ya Mkapa na ndio awamu iliyoleta balaa katika nchi hii.UFISADI WA EPA UMETOKEA HUKO,RELI,RADA,NDEGE YA RAIS,BANDARI,MADINI,MABENKI NA KILA AINA YA BALAA IMETOKEA KATIKA AWAMU YAKE NA MKAPA SASA LEO ANATUAMBIA NINI? Kikwete una kazi kubwa maana hawa vigogo uliowaacha ndio wanakutupa mkono na kukuzunguka. SUMAYE TUBU KWA MUNGU NA WAOMBE RADHI WANANCHI MLILOLIFANYA WEWE NA MKAPA NDIO MATOKEO YA VURUGU ZA HAPA NCHINI KWA SASA.
January 28, 2011 1:47 AM
blank.gif

Anonymous said... Ee Bwana wee,

Nyie kwenye enzi ya uongozi wenu mliuza raslimali za nje kama vile hakuna kesho: si tu mashirika ya uma bali pia mali asili na chochote kile - hata nyumba za serikali. Mliwapuuza waalimu, madaktari, wauguzi na hata wakulima, mkajinufaisha nyie wenyewe, mkatajirika haraka haraka, sasa unatuambia nini? Hebu Frederick taja mali ulizokuwa nazo wakati hujawa waziri na ulizokuwa nazo ulipoacha uwaziri mkuu mwaka 2005. Na kama utakuwa mkweli kama unavyojifanya tutakuuliza umezipataje?

January 28, 2011 1:55 AM
blank.gif

Anonymous said... Ni kweli uchumi umewaacha kando maskini lakini hii inatokana na misingi wewe na wenzio mliyoijenga yenye kujenga matabaka. Bwana Sumaye usidhani wananchi hawakumbuki mliyofanya, na kama sasa unatafuta cheap popularity umenoa. Hukumu yako itakuwa ile ile ya wale walioifikisha hii nchi hapa ilipo.
January 28, 2011 2:00 AM
blank.gif

Anonymous said... Huyu mzee hawezi kusema haya kwa ujasiri kama alikuwa fisadi.

Naanza kuamini magazeti yaliyokuwa yanamwandama yalikuwa ni propaganda za siasa. Kwani hata leo magazeti ya chama fulani hayana mvuto hata wa kuyasoma. Wao kuandika habari za kupakana matope ni biashara yao. Laiti wasingepata ruzuku, wangefunga virago.

Hongera Sumaye kwa kutoa elimu ya uraia.

January 28, 2011 2:42 AM
blank.gif

Anonymous said... Maadam kaliona hilo na kulipatia tafakari basi nawajibike kama mtanzania na mwenye nafasi kubwa kuwasilisha na kusimamia katika ngazi husika na sio kusema tu na kukaa kimywa ninamini bado anayo nafasi ya kutetea hoja yake kwa vintendo.
January 28, 2011 5:54 AM
 
Back
Top Bottom