Elections 2015 Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Mkuu, Mkandara, acha hizo, kama umesoma kemia unaelewa kitu kinachoitwa catalyst, kinahitajika ku speed up the chemical reaction na sio part ya required end products, siku zote nawasisitiza watu humu, tuwe wakeli toka ndani ya nafsi zetu, Prof. Lipumba au Dr. Slaa, hakuna anayemuweza Magufuli, in fact hata Lowass as Lowassa, hamuwezi Magufuli, bali Lowassa na the people behind him, akihamia UKAWA, na akawa ndie mgombea wa UKAWA, CCM inapigwa chini kama kumsukuma mlevi!.

Kama kuna nia ya dhati ya upinzani kuingia ikulu, Lowassa is the mean and the way!, na pia ili litimie lile neno la Mwalimu, upinzani wa kweli, utatoka CCM!, tena kama ni kweli Lowassa ata cross, hata watu kama sisi, ambao sikuzote tumekuwa hatuna vyama, tuta reconsider our stands kuisaidia Chadema kuipiga chini CCM!, tena hili likitokea, hata hao CUF wakileta zile zao za kuleta, kulazimisha mgombea wa UKAWA lazima awe yule mgombea wao wa kudumu kwenye urais wa muungano, ni kuachana nao, wakwende zao, Mwamba wa Kaskazini, ukitinga Chadema, Chadema inachukua nchi asubuhi na mapema!, hata mimi nitatafuta jimbo!.

Kwenye vita, ili uweze kushinda vita, sometimes unaweza hata kulazimika ku join forces na adui yako against a common enemy, kisha mta sort out diferences zenu, baada ya ushindi!.

Tena jamaa akikross, tutailazimisha Chadema kuitagrate na ACT ndani ya UKAWA, au kwa tutamshinikiza ZZK na ACT yake wa bow down, au Chadema itoe msamaha wa bila masharti, ZZK ai disband ACT na kuirudisha ndani ya Chadema, with a united front ya opposition, hili dubwana CCM, linakwenda chini jumla!.

Pasco
 

Pasco, hembu kuwa mkweli japo hata kwa unafiki,ACT +Zitto = plan C ya Lowassa ambayo sasa imekufa so plan B ni CHADEMA na inabidi ACT na Zitto lazima wawe accommodated na UKAWA/CHADEMA kwa sababu ni "step son wa Lowasa"??!!
 
Last edited by a moderator:
chadema watangaze mgombea sasa maana porojo zimekuwa nyingi sana.. tunashindwa tushike lipi.. waamue kama huyu fisadi papa anakuja wengine tujiengue taratibu. tuwaachie wenye chama sasa..
 
Mkuu Mp Kalix2, nayatafakari maneno haya kwa kina!.
Pasco


Karibu sana!
Na ukipata nafasi mwambie Mhe.kuwa zake achanganye na za Mbayuwayu.
Ajali hii ya Kisiasa iliyomkuta muda huu lazima imempatia nafasi ya kuishi muda mrefu sana kama atakaa chini nakufanya tathimini ya aina ya watu waliomzunguka toka alipokuwa Serikalini mpaka dakika ya kukatwa na Kamati ya Maadili.(A.K.A Kamati ya Maadili)

Dunia hii binadamu amezungukwa na Watu,ndugu ,wapambe,wanafiki,maadui,wasamaria wema na wapendwa. Sasa chaguo ni lako mhusika aina ipi ya kundi unataka kushiriki nacho au kuishirikisha kwenye jambo lako.


Narudia Mhe. Bado hajachelewa kama kweli lengo nikuwaleta watanzania safari ya matumaini.
Matumaini huishi hata ukifa-muhimu umeacha misingi ya matumaini au inazikwa pamoja nawe ukifa.

Sioni namna rahisi yakueleza ninachowaza au kufikiri kama kweli Mhe.Lowassa ni msafi.
Kwa kiasi naona maneno haya hapa chini yanaeleza mazingira aliyopo;


 
Pasco, Duh hii Kemia yako mkuu haitumikii kwa binadamu, sisi tuna akili za kufikiri na Unafiki ambao unaweza toa results tofauti kabisa. Kama ulivyosema, Lipumba, Dr.Slaa na Lowassa wote hawamuwezi Magufuli kwa sababu Magufuli yupo na chama kubwa. Chama ndicho kinampelekea mtu IKULU sio nguvu ya Mtandao na ndio maana nikasema maadam UKAWA sio chama basi hakuna atakaye ishinda CCM..

UKAWA pengine inamuhitaji Lowassa kwa fikra zao za kimaskini, maana watu walio nyuma ya Lowassa ni wachumia tumbo tu hawawezi kuleta ushindi kwa sifa gani basi? Hawa watu wana sifa gani haswa zaidi ya wao wenyewe kuahidiwa!. Kundi lote hilo lilikuwa na nguvu ndani ya chama tu kama ingefika NEC sasa maadam kisha katwa huku nje hawana influence kubwa kwa wananchi zaidi ya kuogopwa!

Na sidhani kama Lowassa atakuwa mjinga kiasi hicho cha kuhama kwa sababu ya wapambe.Hawa wote ni wakapi yalokwisha kamuliwa vya kutosha hawana tena nguvu ndani wala nje ya chama baada ya zile results zilizosomwa na CC za tano bora! ilikuwa kipigo cha mbwa (kerbu). Kama wangekuwa na uwezo wa kumfikisha IKULU tungeona nguvu zao hapo.. Lowassa kisha fundishwa adabu kuwa chama ni kikubwa kuliko yeye akae pembeni ale pension yake ya Waziri mkuu mstaafu.
 


Mikwara ile ile mliyotumia kujaribu kuitikisha CCM mnataka kuingia nayo UKAWA!
Kweli sikio la kufa halisikii dawa. Kama iko hivyo kuwa Lowassa kama Lowasa hamwezi Magufuli na kwamba anahitaji watu wengine kwanini iwe lazima yeye awe mgombea wa Uraisi? kupitia UKAWA?

Si yako vyama kama ACT-Wazalendo au DP ya Mtikila kama lengo ni ushindi si aende huko kwa lengo la kupambana Zimwi mmoja (CCM) (A.K.A Kamati ya Maadili)

 
lowassa ni kweli ananguvu kubwa ya kuitikisa ccm lkn tujiulize wakina lowassa wangap walikua ccm wakahamia chama kingine stl ccm ikamove on bila kutetereka????nnavojua ccm ni zaidi ya lowassa na tusijidanganye kwa style hii ya ukawa kuchukua walioshndwa ccm kuwa malaika kwao hatutafika,inaonekana dhahiri kuwa wenyewe kama wenyewe hawawezi kutuongoza bila kumpata mtu wa ccm yaani ccm kama ndo chuo chao cha kupata watu bora at the same time wanakiponda....tuwaeleweje wapo upande gan au ndo uchu wa madaraka???
 
Watu makini wanakua team lowasa wallikosseaa step hatua za mwisho kabisa,sasa wassije kufanya huo uzembe ukawa,wakiwa smart wanabeba nchi,hivi huyu fisadi dagaa pasco yuko wap siku Hz?
 

Nasikia kisu cha CCM kilikuwa butu sasa anarudi kwa speed ya ajabu UKAWA sasa sijui huko atajisafisha. Pengine atafute mualovela wa kujisafishia!
 

Ha ha nadhan mzee wa vunjo ni mfano hapo!!
 
Ndio kashaingia Chadema sasa,leo ufurahi kidogo,Pasco,mzee wa john mtembezi
 
Ndio kashaingia Chadema sasa,leo ufurahi kidogo,Pasco,mzee wa john mtembezi
Mkuu umenikumbusha Joni Mtembezi, nilianza kutembea kwa hatua ndogo ndogo kwa mwendo wa pole, safari ya kuzunguka na Joni Mtembezi mkubwa hunichukua hata mwezi mzima!, lakini siku hizi speed ya kutembea naye imeongezeka kwa ma mahatua makubwa makubwa na ya mwendo wa haraka hivyo safari inanichukua wiki tuu!, hali iliyopelekea wife kuanza ku mind, hivyo Joni Mtembezi nimemwacha counter ya pale sitting room kwangu (Rombo), ili kuzuia ghubu home!.

Pasco
 
Sema kipenzi cha wapenda pesa. Kama kipenz cha wengi mbona huko cc wamemfyeka?

it has no doubt Lowassa ana popularity kubwa na ana watu wengi than Magufuli! Kumfyeka kwao sio kwasbb hapendwi na watu ila ni kwasababu ya hofu walizojawa! Ogopa saana kumtendea mtu mabaya akawa kimya halafu akapata nguvu!
 
Pasco,

haya hayawi hayawi yamekuwa, sasa nasema hivi kumchinja kuku unamwelekeza Kibla unamkanyaga mbawa zake na kupanda shingo lake kisha unapitisha kisu watu wakiangalia na wengine wakishangilia, hivyo ndivyo kifo cha Lowassa na UKAWA..

Kuna watu wamenambia ili kumwondoa CCm tunahitaji mikakati kama ya Kenya lakini UKAWA hawakufanya hivyo wala Kibaki hakuwa maarufu kuliko Kenyatta wakati ule ila UMOJA wao ndio ulokuwa na nguvu zaidi ya KANU..Nqa kisha basi Umoja wa Kenya uliuondwa na undi la wanaharakati walotaka magewuzi dhidi ya MAFISADFI leo nyie mnachukua MAFISADI dhidi ya CCM ambayo ina nguvu kuliko nyie.. Hamuwezi kupata mageuzi kwa njia hiyo nawahakikishia kabisa CCM chama kubwa Lowassa na kundi ake ni wachumia tumbo rahisi sana kubomolewa.

Kwanza wataanza na yeye kisiasa wakishindwa, mwanaye ana scandal ya nyumba London inaweza ibuliwa, kesi ya EPA na Richmond zinaweza ibuliwa upya hata akisema JK ndiye mwenye mzigo (wewe ulihusika vipi?) itabidi asimamishwe yeye kugombea. JK ni rais ana kinga hata akisha achia ngazi wala hagombei tena. Kesi inapikwa mahakamani KWISHA kazi!. Muda wa Uchaguzi umekwisha..
 



Kwenye vita, ili uweze kushinda vita, sometimes unaweza hata kulazimika ku join forces na adui yako against a common enemy, kisha mta sort out diferences zenu, baada ya ushindi!.
Pasco

Pasco kama wewe huwa unaangalia mieleka ile ya WWE au kama kuna mtu huwa anaangalia ataelewa hoja yako.

Huwa **** mechi zinaitwa triple threat match au one man stand match. Hizi mechi mnawekwa ulingoni zaidi ya watu wawili, mshindi anatakiwa awe mmoja.

Woye mlioko ulingoni ni maadui ila yupo adui ambae labda ni giant na mwenye nguvu kuliko nyie as individual, kwa hiyo nyie weak wawili kwa mfano kama ni triple threat mna team up ili kumuondoa yule adui yenu strong/giant.

Mkishamtoa badae mechi inaendelea ila yule big threat kwenu katoka nje au mmemshinda tayari. Hapa ni triple threat match, ccm,ukawa na lowassa, ccm ni giant, kuitoa itabidi hawa weak ukawa na lawassa wateam up kuitoa ccm.

Hilo linawezekana maadui kuungana kushinda vita dhidi ya adui yao mkubwa. Wakurd hawaelewani na uturuki miaka nenda rudi, wakati huo huo islamic state ni adui wao wote, imebidi uturuki akubali vifaa vipitie kwake kwenda kwa wakurd ili kupambana na islamic state.

Huko mexico serikali kupambana na magenge ya kina el chapo huamua kushirikiana na magenge madogo ili kuteketeza magenge makubwa ya madawa ya kulevya.
 
Kama una ndoto za kufunguliwa kesi za EPA, Richmond kipindi kabla ya uchaguzi sahau, hata wakilazimisha atakayechafuka zaidi ni Kikwete na hata kama ana kinga ni rais gani anayependa kuishi maisha ya kesi?

Ya KANU na NARIC tuwaachie wakenya tujikite na yetu ya UKAWA na Lowassa.

Kwa wasiomfahamu EL wanaweza kufikiri kaanza leo kuusaka urais, EL amejipanga kwa takriban miaka 20 ana resources zote watu, ukwasi, mbinu njema na ovu nk..bila kusahau kuwa timu yake ndiyo iliyofanikisha uchakachuaji wa 2005 na 2010.

EL ana watu hadi ndani ya usalama kwenyewe issue zote na mauchafu ya viongozi wengi anayajua ndiyo maana kaamua Ku cross line bila hofu, nani aanze kumtupia madongo? watabaki kina Makonda na Nape wasiojua lakini the big fish hutowasikia.
 
Peingine nyie ndio hamumumfahamu Lowassa, maana CCM wanamfahamu zaidi yenu mkimsoma katika magazeti tu, na wamemwaga. Kama angekuwa na nguvu hizo wasingethubutu ila walijua yote haya mapema sana na watu wake walitishiwa toka zamani kuwa akikosa Urais CCM atahamia CDM na bado CCM wamlimwaga - huwezi kufikiria hapo tu?

Pili, Lowassa akiwa Rais atakuwa rais wa Kundi lake yeye, na sio wa UKAWA maana Urais kautafuta kwa miaka 20 akiwa CCM kama ulivyosema, hao CDM wala NCCR hawakuwa naye wakati wote. Hilo kundi lake pekee kisha waahidi wizara na kushika mamlaka ya juu kabisa ya serikali yake ataweza vipi awaachie nyie ambao hamkuwa naye miaka yote?.. Na akisha apishwa akawa Rais ana kinga zote, Je,kimchagua Chenge waziri mkuu mtamfanya nini? hamtakuwa na la kusema ila kulalamika!..Ame Cross line kwa sababu ana uchu wa madaraka na huko CDM kumejaa mbumbumbu wachumia tumbo. Ebu fikiri moja kwanza Je akikosa Urais mtakuwa mtabakia na sura gani machoni mwa watu maana kuna kupata na kukosa!

Hizo Billioni mnazotegemea kupewa ili wabunge wenu waweze kuwa na fedha za kujitangaza hazitawasaidia chochote maana siku hizi watu wanakula mshiko kisha kura zao wanampa mtu mwingine. Sii wajinga hivyo na ndivyo alivyofanywa Lowassa kwenye vikao vya CC ya CCM watu walikula fedha na bado wakamwaga wengine wamesha mkimbia!...Imekula kwenu mkuu, tamaa ya fedha imewafikisha pabaya wala sii kutaka mageuzi ya kisiasa maana mngeweza hata bila yeye wala UKAWA kama mngejipanga na kusikiliza ushauri wa watu wanaojua Siasa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…