Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini? | Page 14 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Jul 11, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.

  Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?

  Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema, upinzani wa kweli, utatoka CCM. Jee hiki ndio kipindi cha upinzani huu?

  Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?

  Jee Lowassa tuliombatiza jina la mwamba, ataliishi hilo jina la mwamba kwa kuonyesha umwamba wake kwa kutokubali kuchinjwa na kufanywa mbuzi wa shughuli, au lile jina la mwamba, tulimpachika tuu, ila in reality kumbe sii mwamba lolote wala chochote, bali ni kichuguu tuu?.

  Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?

  Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?!.

  Japo CCM ni chama kikubwa, kikongwe, na chenye nguvu, mbele ya Lowassa CCM ni chepesi kama unyoya, akipuliza tuu kinapeperuka, na hizo nguvu CCM inazojivunia, mbele ya Lowassa ni kama uzi wa utando wa buibui, ukigusa tuu umekatika!.

  Wapenzi, wafuasi, na mashabiki wa Lowassa, wanachosubiri sasa ni aseme neno moja tuu na roho zao zitapoa!, akiamua kukubali matokeo kuwa kukatwa kwake ndio mwisho wa safari, na akubali na aseme wazi, "Eloi Eloi, Yemekwisha!", na kama hajakubali, atamke wazi kuianza ile safari ya ukombozi wa pili wa Mtanzania, dhidi ya mkoloni mchwa CCM, aliyelitafuna taifa letu kwa miaka 50, na akitamka tuu!, "CCM Basi!", huo ndio utakuwa mwisho wa hili zimwi linaloitwa CCM!, CCM itakuwa ni bye bye jumla, kaburini forever!, kwa sababu kazi kubwa ya kwanza ya serikali mpya, itakuwa ni kuzitaifisha mali zote za umma CCM iliyozipora na kuzipata kwa njia dhalimu kwa kuzipora toka kwa Watanzania katika kipindi cha utawala wake, na kujimilikisha kujifanya ni mali zake, yakiwemo majengo yake yote!. CCM ikiishakuwa haina kitu, hiyo sio CCM tena bali itageuka CCM mfu na tutaizika rasmi kaburini!.

  Lowassa sema....
  Sema usiogope sema!.

  Linasubiriwa Neno tuu!.

  Pasco!

   
 2. Masenu K Msuya

  Masenu K Msuya Verified User

  #261
  Aug 30, 2017
  Joined: Jun 20, 2017
  Messages: 1,307
  Likes Received: 1,209
  Trophy Points: 280
  fisadi papa hawezi kuingia ikulu
   
 3. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #262
  Sep 1, 2017
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,928
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Dah....maneno ya Mzee wa kiti moto  Sent from my beretta ARX 160 using JamiiForums Mobile App
   
 4. W

  Wakudadavuwa JF-Expert Member

  #263
  Sep 3, 2017
  Joined: Feb 17, 2016
  Messages: 9,948
  Likes Received: 8,475
  Trophy Points: 280
  unazungusha mikono kwa sasa
   
 5. W

  Wakudadavuwa JF-Expert Member

  #264
  Sep 3, 2017
  Joined: Feb 17, 2016
  Messages: 9,948
  Likes Received: 8,475
  Trophy Points: 280
 6. W

  Wakudadavuwa JF-Expert Member

  #265
  Sep 3, 2017
  Joined: Feb 17, 2016
  Messages: 9,948
  Likes Received: 8,475
  Trophy Points: 280
  Dah
   
 7. W

  Wakudadavuwa JF-Expert Member

  #266
  Sep 3, 2017
  Joined: Feb 17, 2016
  Messages: 9,948
  Likes Received: 8,475
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi anawachakaza "makamanda"
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #267
  Jan 10, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Kama lilivyosubiriwa neno moja tuu aseme, na sasa Lowassa ndani ya upinzani, linasubiriwa neno moja tuu, aseme anarejea CCM, kwa sababu Lowassa alijiunga upinzani kwa malengo, na maadam malengo hayo hayakutimia, hakuna ubaya wowote akirejea nyumbani!.

  Paskali
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...