Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini? | Page 13 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Jul 11, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.

  Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?

  Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema, upinzani wa kweli, utatoka CCM. Jee hiki ndio kipindi cha upinzani huu?

  Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?

  Jee Lowassa tuliombatiza jina la mwamba, ataliishi hilo jina la mwamba kwa kuonyesha umwamba wake kwa kutokubali kuchinjwa na kufanywa mbuzi wa shughuli, au lile jina la mwamba, tulimpachika tuu, ila in reality kumbe sii mwamba lolote wala chochote, bali ni kichuguu tuu?.

  Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?

  Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?!.

  Japo CCM ni chama kikubwa, kikongwe, na chenye nguvu, mbele ya Lowassa CCM ni chepesi kama unyoya, akipuliza tuu kinapeperuka, na hizo nguvu CCM inazojivunia, mbele ya Lowassa ni kama uzi wa utando wa buibui, ukigusa tuu umekatika!.

  Wapenzi, wafuasi, na mashabiki wa Lowassa, wanachosubiri sasa ni aseme neno moja tuu na roho zao zitapoa!, akiamua kukubali matokeo kuwa kukatwa kwake ndio mwisho wa safari, na akubali na aseme wazi, "Eloi Eloi, Yemekwisha!", na kama hajakubali, atamke wazi kuianza ile safari ya ukombozi wa pili wa Mtanzania, dhidi ya mkoloni mchwa CCM, aliyelitafuna taifa letu kwa miaka 50, na akitamka tuu!, "CCM Basi!", huo ndio utakuwa mwisho wa hili zimwi linaloitwa CCM!, CCM itakuwa ni bye bye jumla, kaburini forever!, kwa sababu kazi kubwa ya kwanza ya serikali mpya, itakuwa ni kuzitaifisha mali zote za umma CCM iliyozipora na kuzipata kwa njia dhalimu kwa kuzipora toka kwa Watanzania katika kipindi cha utawala wake, na kujimilikisha kujifanya ni mali zake, yakiwemo majengo yake yote!. CCM ikiishakuwa haina kitu, hiyo sio CCM tena bali itageuka CCM mfu na tutaizika rasmi kaburini!.

  Lowassa sema....
  Sema usiogope sema!.

  Linasubiriwa Neno tuu!.

  Pasco!

   
 2. M

  Mangi Muitori JF-Expert Member

  #241
  Jul 28, 2015
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 474
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi alikatwa na CC au NEC au hukumsikiliza Nchimbi na Simba
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #242
  Jul 28, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Mkuu , kifo hiki unachokizungumza ni kifo cha CCM!, ila pia nimegundua tuna watu humu waliokuwa wakijifanya ni pro opposition, huku mioyoni mwao wanaipenda CCM kwa dhati, sasa baada ya kuenea hizi habari za possibility ya Lowassa ku cross ambayo ndio kifo cha ukweli cha CCM, sasa wanaingiwa uoga na kuanza kujionyesha rangi zao halisi kwa kuchelea kifo cha CCM!. Nasema kwa msisitizo, Lowassa akisimama UKAWA, CCM Chali!.

  Mawazo haya mimi nayaita ya ki CCM, determinant ya ushindi wa Lowassa dhidi ya CCM sio mbinu gani zitakazotumiwa bali Lowassa ni mtu aliyejaaliwa karama ya mvuto wa 'vox populi' ambayo ndio 'vox Dei!'!, CCM hawana, Magufuli hana!. Tukubali tukatae kama ni nguvu ya utendaji, Magufuli ni mtendaji mzuri kuliko Lowassa, Magufuli ni muongeaji mzuri kuliko Lowassa!, ila Magufuli hana hiyo karama ya 'vox populi!', hivyo Magufuli sio 'Vox Dei!".

  Karibu unitembelee hapa
  [h=3]Kuelekea Octoba 2015: Je, Hii "Vox Populi" ni "Vox Dei" [/h]At this juncture, nawaomba nyie ma Great Thinkers wa JF, watu wenye ushawishi mkubwa humu, tuungane kwenye hili, yuutumie uwezo wetu na nguvu yetu ya ushawishi, kuisupport hii move ya Lowassa ili tuipumzishe CCM, unless kama nilivyosema mwanzo, kama wenzetu ni pro opposition kwa nje na mna mapenzi na CCM kwa ndani, mnaweza kuendelea na kazi ya kumbomoa Lowassa na kuibeza UKAWA, we real need you, kwenye together we stand, but ukombozi wa Tanzania, don't depend on you!, we bank on "vox populi!", you only have two choices, either with us or against us!.

  Aluta Continua Victoria Acerta!.

  Pasco
   
 4. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #243
  Jul 28, 2015
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,175
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Either you support and vie through TNA (In this perception "CDM") (in central Kenya) or you perish!- Uhuru Kenyatta
  Hivi ndivyo ilivyo. Ukweli na usemwe,hii coaction ya Chadema na EL ni deadly working machine. hata huko majimboni masalia ya wagombea ubunge wa ccm watakuwa na hali tete,haijalishi ni kwa Mwakyembe,kwa muhongo,kwa Mwigulu,Ni bomoa bomoa tu. Pasco nimekukubali. I admire you folk.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #244
  Jul 28, 2015
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 17,229
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  1. Kwani CC jina lake liliingia..??? Acha upofu wa fikra, ni mbaya sana...
  2. Hivi unajuwa CC yaliingia majina mangapi?
  3. Unajuwa kamati ya maadili ilifanya nini?
  4. Unajuwa siri ya wajumbe wa kamati ya CC kuimba wana imani naLowasa.?
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #245
  Jul 28, 2015
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,994
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Mkandara,

  Kwa taarifa tu EL hakukatwa na CC wala NEC bali kamati ya maadili, lakini hata baada ya jina lake kukatwa bado nguvu yake ilionekana kwa kulazimisha chaguo ambalo hawakutegemea (Magufuli).

  Pili Lowassa anaijua CCM na Kikwete in and out ana watu wakubwa ndani ya chama na serikali kwa hiyo chochote watakachopanga lazima kimfikie.

  Ni ukweli usiopingika kama akifanikiwa kuupata urais ataweka anaowataka, sawa hata mimi ningefanya hivyo lakini kumbuka kuna makubaliano possibly chanya ambayo hatuyajui ambayo lazima yazingatiwe na chama kama taasisi.

  Binafsi nafikiri real pro opposition wengi (Pasco) watakubaliana na mimi kuwa tembo afe kwanza suala la nani atachukua maini lije baadaye, tukibaki kuzozana nani atachukua hiki tembo atazidi kukua mwisho tutastukia kala mazao yote.

  Kuhusu billions za EL hiyo siyo issue kwa vile Chadema ilikuwa imejipanga kuingia kwenye uchaguzi bila hata Lowassa, Lowassa na billion zake kama kweli zipo is an added advantage au kama Pasco anavyoita ni sawa na catalyst kwenye uchaguzi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #246
  Jul 28, 2015
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 17,378
  Likes Received: 61,528
  Trophy Points: 280


  Mkuu Pasco you are a living legend!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #247
  Aug 28, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Nafanya tafakuri tuu.

  P.
   
 9. c

  chante Senior Member

  #248
  Oct 11, 2015
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  bado natafakari
   
 10. Jigsaw

  Jigsaw JF-Expert Member

  #249
  Oct 11, 2015
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 1,818
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Daah.. Hili Game zuri kweli. Ukilitazama kwa mbali unaweza tengeneza Novel ya Kiswahili yenye kuuzika vizuri. Lowassa kwa watanzania hakakiti aisee. " ULIPO TUPO.
   
 11. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #250
  Oct 11, 2015
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,443
  Likes Received: 3,693
  Trophy Points: 280
  kiongozi Pasco uliona mbaaali saana. mabadiliko2015
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. c

  chante Senior Member

  #251
  Oct 11, 2015
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pasco ana karama inaitwa precognition.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. saiditawani

  saiditawani JF-Expert Member

  #252
  Oct 11, 2015
  Joined: Jul 5, 2015
  Messages: 358
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Pasco uliona mbali sana. Congratulations to you my brother.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. c

  chante Senior Member

  #253
  Oct 11, 2015
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  precognition.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Root

  Root JF-Expert Member

  #254
  Oct 11, 2015
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,949
  Likes Received: 13,800
  Trophy Points: 280
  Mengi aliyosema huyu jamaa yametoka
   
 16. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #255
  Oct 11, 2015
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,585
  Likes Received: 12,065
  Trophy Points: 280
  Pasco kuna vitu unavijua kabla ya wengi.

  Tupe siri ya urembo.
   
 17. Eng.Livingstone

  Eng.Livingstone JF-Expert Member

  #256
  Oct 23, 2015
  Joined: Aug 29, 2013
  Messages: 881
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lowassa ni superPower amefanya kampeni mara 4 katika uchaguzi wa mwaka huu,kura za mjini na vijijini anazo za kutosha,kumbuka huyu alikuwa ccm miezi 4 iliyopita.
   
 18. tang'ana

  tang'ana JF-Expert Member

  #257
  Mar 30, 2017
  Joined: Apr 3, 2015
  Messages: 6,788
  Likes Received: 4,426
  Trophy Points: 280
  Tujikumbushe
   
 19. FORTALEZA

  FORTALEZA JF-Expert Member

  #258
  Jul 5, 2017
  Joined: Jan 1, 2017
  Messages: 1,049
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Masikini Lowassa
   
 20. m

  masterplanner Member

  #259
  Aug 29, 2017
  Joined: Oct 23, 2015
  Messages: 88
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Game over
   
 21. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #260
  Aug 30, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  HABARI YA LOWASSA HAINA MVUTO TENA. HAKUNA SIKU NILIFURAHI KAMA ALIPOKATWA NA CCM. ALIJIDANGANYA KWAMBA YEYE NI MAARUFU KULIKO CHAMA! AKATHIBITISHIWA KWAMBA SIYO HIVYO. KAKATWA NA MAISHA YANAENDELEA. SAAAAAAAAAAAAAFIIIIIIIIIIIIIII!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...