Elections 2015 Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

quote_icon.png
By Pasco
Kwa msisitizo, rais bado ni Lowassa ila kupitia nje ya CCM, infact nashauri ndie awe mgombea wa UKAWA!.

Pasco

Poor Pasco miaka yote ulikuwa unapuuza vyama vya upinzani na kuvikejeli leo unataka mgombea wako agombee kupitia Ukawa. To hell Pasco na Lowassa
 
Walioimba ufisadi wa Lowassa ni CCM.
Mara kuvua gamba, n.k.

Sikumbuki popote Wapinzani walipomtaja Lowassa kuwa ni fisadi.
Ufisadi ndani ya Chama cha Mapinduzi ni MFUMO RASMI.
UKAWA wasipompokea Lowassa, maana yake ni kwamba hawataki kuuondoa madarakani mfumo wa ufisadi.
Tatizo letu ni mfumo, siyo watu au majina ya watu.
Kama kweli Ukawa wanaitakia mema nchi yetu, basi naamini wako kwenye kikao na Lowassa hivi sasa.
Mungu ibariki Tanzania.




iukisema wapinzani, jua kuwa lowasa hawezi kuhamia CHADEMA, CUF, NCCR bali atachagua vyama vile ambavyo huwa vinaunga mkono ccm kama TLP, PPT MAENDELEO, TADEA, UDP YA CHEYO nk. hawezi kutia mguu vyama bora, anaenda kwa salvages.


Unaona hata ukawa kwenyewe kuna mtifuano wa wadau.. Hizi ni contradictory comments toka kwa member hawa!! Lowassa na marafiki zake na move zake zote zimetajwa na ukawa na wanaccm pia kuwa ni za kifisadi!!

Bado naendelea na msimamo wangu wa kuwadharau ukawa kama wakimpokea Lowassa na kumpa mikoba.

Moja inaonesha jinsi ambavyo hawakujipanga kwa zaidi ya miaka mitano, wanasubiri makombo yanayotemwa na ccm ndo wachukue (Ganda la muwa la jana chungu kaona mavuno).

Pili baada ya muda yatajirudia yaleyale ya akina shibuda wanapigwa chini ccm wanakimbilia cdm.

Bado cdm itajiita ni chama kisafi kinachopigania maslahi ya watanzania!?
 
Leo nimefurahi sana Lowasa kukatwa. Tuone sasa wale manabii na wachungaji feki kwamba Lowasa asipokuwa rais wao watawajibika...na wawajibike sasa.
 
Pasco ungepumzika for now
sioni kama una make sense anymore
kila ulichotuambia huko nyuma kimeenda the opposite
labda sasa ungenyamaza kwanza.......ni kama vile nyinyi wapambe wa mgombea
mna kiu na urais kuliko mgombea mwenyewe

Ushauri mwanana

Wadau wengi humu ndani tunaeshimu michango ya
Pasco
Ila usipozingatia ushauri huu hadhi yako itashuka. na nipende kukazia tuu, my brother
Pascousikubali njaa ikaongoza akili yako, na jitaiti sana kusapoti actions na sio mtu. Kwani kusaport mtu siku akifa kila kitu kitasimama lakini kusuport actions siku mtendaji akifa mliobaki mtaendeleza.

 
lowasa akienda ukawa anashinda urais, achague vyama vile ambavyo havina hata shilingi mia mfukoni au vile vinavyotaka kufa, achukue fomu, anashinda uchaguzi bila shida. ila awe makini ahofie usalama wake kwa sasa kwasababu ni kitu kigumu sana kupigana na system hasa katika wakati kama huu ambao wamemwonyesha wazi kuwa wanapambana naye.
Watu wote wenye mawazo kama haya mnasahau kwamba tume ya uchaguzi iliyopo ni ile ile ya ccm, ambayo katu haitamtangaza mpinzani kuwa kashinda uchaguzi. Nadhani bado tuna jukumu kubwa sana la kushinikiza kupata tume huru kabla ya kufikiria mpinzani kwenda ikulu.
 
Huo ni mpango wa Mungu.

Ivi kwa mfano Mungu amepanga CCM ife 2015, atatumia mbinu gani?!

Chukulia mipango ya Yesu Kuuawa, je waliokua wanatoa ukumu, kumsulubisha, walijua ni mpango wa Mungu?!
 
Kilichomuua Edo ni TISS, Apson ndo kamuharibia mwamba wa Kaskazini, ni
uchaguzi wa Edo sasa kuamua kama ataenda kile chama ambacho alimuanzishia Kabwe.............ACT.....maoni yangu
 
Pole sana PASCO SIKIONI CHOCHOTE ALICHOIFNYIA TANZANIA LOWASA KIASI CHA KUMPA UMWAMBA KAMA WA PETRO KWENYE BIBLIA HIVI NINI HASA ALICHOWAPA MPAKA MNASHABIKIA UJINGA ILI HALI MNAONA?

HIVI LOWASA WAWEZA KUMLINGANISHA NA MAGUFULI AMBAYE AMEDUMU KWENYE CABINET AWAMU ZA BEN NA KIKWETE ? UNAWEZA NITAJIA HATA KITU KIMOJA TU AMBACHO HUYO NABII WAKO AMEIFANYIA TANZANIA?

TULIZA AKILI USIBURUZWE NA UPEPO WA RUSHWA NA MWAMBIE AHAMIE ACT KAMA ATASHINDA
 
PASCO,mwalimu wangu wa MEDITATION,sijui PRE COGNATION haikufanya kazi maana kila ulichokisema kuwa kitatoke hakijatokea
 
Wapinzani ntawadharau na pasina shaka hata watanzania wengi watawadharau kama wakimpokea Lowassa!

Wameimba nchi nzima kwa miaka chungu nzima kwamba EL ni fisadi eti leo wampokee na kumpa nafasi ya juu kabisa ya kugombea urais!!!

Kupata nafasi UKAWA haiwezekani na yeye analijua hilo. Zitto alishaijua picha yote ndiyo maana alishamkaribisha ACT.

Sasa Pasco, mshaulini Lowasa atangaze mali zake akagombee ACT. Supremo Leader atampokea kwa mikono miwili.

Watanzania inabidi tumpe support huyu bwana maana ndiye atakaye tukomboa kutoka kwenye minyororo ya CCM!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco
Awali ya yote naomba niweke sawa hili neno ‘amekatwa' Kwalugha ya kwetu neno hlio lna tashititi kidogo.

Kijana akitengenezwa kwa suna twasema amekatwa. Sisi wa mwambao linatutesa sana hili neno, tuvumiliane

Pasco , mwaka wa pili kama si wa tatu tumekueleza kwa uhakika mzee hatapata fursa ya kubeba bendera kwenda' nchi ya ahadi' Pamoja na ukweli ni shamba la ngano liloilojaa magugu, waashi wamekataa.

Atakuwaje jiwe la pembeni ikiwa pembe zote zina mawe tayari?

Hili ni funzo kwa wanasiasa. Tulipopigania sana wagombea binafasi hatukuwa tunatetea nafsi zetu.

Tuliangalia nafasi ya jiwe kuu la pembeni nje ya mfumo wa waashi


Kwa muda uliopo, hakuna safari tena isipokuwa ya kurejea karibu na Minjingu.

Hakuna anayependwa, kilichopendwa ni rupia.

Nakuhakikishia usiku huu ''wafanyakazi'' wake hawafikiri mzee yu hali gani, wanavuta tafakuri ya kambi ya kuhamia


Ikifika kesho, mzee atabaki mwenyewe. Safari ya Minjingu ndiyo tumaini pekee. Inauma sana, ndio ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom