Kukata kimeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukata kimeo

Discussion in 'JF Doctor' started by Ulimakafu, Jul 9, 2011.

 1. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Naomba kujua kitaalam kama kukata kimeo kwa watoto wanaokohoa kama ni tiba au ni imani tu za watu.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kimeo ni kiungo muhimu kwenye mwili wa binadamu. Kukikata ni sawa na ukeketaji!

  Utajiona unatibu kitu unachokidhania wewe lakini ukatengeneza tatizo lingine baya zaidi.
   
 3. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni imani tu za watu wala si dawa.
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu.
   
 5. Eshacky

  Eshacky JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 966
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mimi nilisumbuliwa sana kifua baada ya kukata kimeo,kifua kimeacha afya imerudi na hakuna madhara yoyote yaliyonikuta. Ingekuwa haisadii usingeona iyo huduma inatolewa miaka nenda rud japo kuwa kitaalam hairuhusiwi. Na uthibitisho ya watu km 3 imewasaidia.
  Nb: apply mbayuwayu skills.
   
 6. k

  kamili JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Tanzania bado tupo katika kipindi cha mpito cha kutumia tiba za kudhani kuelekea tiba za kisasa ambazo zimefanyiwa utafiti wa kisayansi. Mtakumbuka miaka michache iliyopita watoto wenye homa walikuwa wanango'lewa meno ya plastik! na wapo waliodai wamepona homa, halafu watoto wenye degedege walikuwa wanatiwa kwenye ungo wanapepetwa na wakati mwingine kuwakojolea ati ndio dawa, na wapo wanaodai kuwa inaponesha degedege! wopo waliokuwa wanaumwa na kichwa halafu kichwa kinachanjwa ati wanatoa damu chafu (huku hawajui chanzo) pia wapo wanaodai inaponesha! Na sasa tuna tiba ya Loliondo ambayo nayo tunaambiwa inaponesha. Hiyo ni mifano tu.

  Kama kukata kimeo kungekuwa kunaponesha basi tiba hiyo ingepatikana hata hospitalini. Maana itakuwaje waweze kupasua kichwa, moyo, macho, mapafu nk. washindwe kukata kimeo? Kifupi kwa mazingira ya kawaida kukata kimeo hakuponeshi na tena kuna madhara.
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Shukrani kwa mawazo mkuu.
   
 8. KAKA A TAIFA

  KAKA A TAIFA JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 564
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  HII NI IMANI,MAZOEA ,UKOSFU WA ELIMU ,DESTURI ZA WATU/MAHALI FULANI.UKWELI NI KWAMBA KIMEO HUREFUKA KULINGANA NA KILA MTU ALIVYOUMBWA.HAIWEZEKANI KIKAZIDI UREFU WA KAWAIDA LABDA KAMA KUNA TATIZO LA UGONJWA AU KUGONWA (INFECTION/IMFLAMMATION/INJURY) AU UMBILE POTOFU(HEREDITARY ABDOMARLITY).KAZI KUU YA KIMEO NI KUSAIDIANA NA KINYWABUCAL CAVITY),MFUPA WA ULIMI(HYOID BONE) NA KIUNGO KINGINE(LARNX)ILI KUWEZESHA CHAKULA KUMEZWA BILA KUINGIA KWENYE KOO LA HEWA NA SAUTI.KWAHIYO KUKATA KIMEO UNAHARIBU MFUMO WOTE HUO WA UMEZAJI CHAKULA.PILI HUWEZI KULETA UGONJWA (INFECTION),USAHA AMBAO UKIMEZWA NAO NI TATIZO JINGINE NA KWA KUWA KIUNGO HICHO PIA NI KIHUSISHI KATI JICHO,PUA NA KOO MADHARA YANAWEZA KUWA MAKUBWA ZAIDI.NA KUBWA ZAIDI VIFAA VINAVYOTUMIKA VISIWE SAFI(STERILE)HIVYI KUPATA MAGONJWA AMBUKIZI MFANO UKIMWI NK.TUACHANE NA MILA POTOFU ,ELIMU ITOLEWE ZAIDI NA VYOMBO VYA HABARI Anatomy and functionThe epiglottis guards the entrance of the glottis, the opening between the vocal folds. It is normally pointed upward while one is breathing with its underside functioning as part of the pharynx, but while one is swallowing, elevation of the hyoid bone draws the larynx upward; as a result, the epiglottis folds down to a more horizontal position, with its superior side functioning as part of the pharynx. In this manner it prevents food from going into the trachea and instead directs it to the esophagus, which is posterior.
  The epiglottis is one of nine cartilaginous structures that make up the larynx (voice box). While one is breathing, it lies completely within the pharynx. When one is swallowing it serves as part of the anterior of the larynx.Mucosa
  The entire lingual surface and the apical portion of the laryngeal surface (since it is vulnerable to abrasion due to its relation to the digestive tract) are covered by a stratified squamous non-keratinized epithelium. The rest of the laryngeal surface on the other hand, which is in relation to the respiratory system, has respiratory epithelium: pseudostratified, ciliated columnar cells and mucus secreting Goblet cells.Infection of the epiglottis
  In children, the epiglottis will occasionally become infected with Haemophilus influenzae and Streptococci in the trachea, causing massive inflammation, called "Epiglottitis". This condition has become rare in countries where vaccination against Haemophilus influenzae (Hib) is administered
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,090
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Ni imani lakini inasaidia, NB: Wataalam wa kukata kimeo kwa miaka hii inaweza kuwa ni hakuna. Zaidi sana watakata mpaka nyama then utamfanya mtoto apate kansa.
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Dr. Ole ambaye ni mtaalam wa ENT pale Magomeni ambaye alikuwa Daktari Bingwa (sijui kama bado yupo) Muhimbili anakata Kimeo!!! Sijui anatumia utaalam au ni nini? Hebu wataalam wa ENT watupe elimu kwa hili.
   
 11. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Baada ya kukutwa kimeo kwa tuliopona maana me nilikatwa miaka zaidi ya 25 ss nipo fikikinatokea nn?acheni uongo na porojo hapa ni watu wengi saaaaanaaaaaaa tulioponea kwenye kukatwa kimeo hata hao madaktari wenyewe wengine wamekatwapia achezi uzushi na upotoshaji suala hapa ni kuwawezesha wataalamu wafanye kazi hii kitaalamu na si mengineyo!!!!!!
   
 12. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Dr Ole anakata kimeo?
   
 13. k

  kamili JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60

  Mkuu pamoja na maelezo yako mazuri umechanganya mambo mno. Alichouliza ni ukataji wa kimeo ambao kwa kiingereza huitwa uvula, sio Epiglottis ambayo kwa kiswahili huitwa kidaka tonge. epiglottis na uvula ni viungo tofauti kabisa kwa maana vilipo na kazi zinazofanywa

  [​IMG]
  unachokiona kwenye hiyo picha ambacho kimepewa na 3 ndio kimeo ambacho hukatwa na waganga wa kienyeji. Na hiyo picha hapo chini imekuonesha epiglottis au kidaka tonge.!!
   
 14. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu kamili kwa ushauri.
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Kuna ndugu yangu mmoja mwanae alikuwa anasumbuliwa nacho sana na kikohozi kiasi cha kushindwa hata kula,kapelekwa kwa mtaalam mitaa ya Temeke sasa mzima.
   
 16. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Acha uongo wewe..
   
 17. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  We Mamndenyi wee...nani kakuambia hizi hadithi? Sijawahi kuona maandiko/chaposho yanayosema hivyo!
   
 18. c

  cilla JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 249
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Hawa hawajui chochote.huu sio ushirikina ni matibabu tosha .Sisi kwetu wote tumekatwa kimeo kwasababu tumerithi kuwa na vimeo virefu ambavyo huwa vinagusa sehemu za chini za koromeo nakusababisha kukohoa kavukavu wakati mwingine husababisha kutapika.na huwezi kupona kwa dawa ila operation.lla sio tiba ya kifua kikuu.serekali inawasiwasi na vifaa
   
 19. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jamani Mi Naushahidi wa kutosha kuhusu ukataji wa vimeo kuwa unaondoa kabisa la kukohoa haswa kwa watoto. Wadogo zangu wengi wamekatwa vimeo na kweli wamepona kabisa. Tatizo Letu tunaponda sana Traditional Medecine Wakati hatujapatwa na matatizo kama haya lakini kama kweli upo na mtoto ambaye anatatizo kama hili yaani we mwenyewe utalia kuona jinsi gani mtoto anapoteseka kwa kikohozi mpaka mbavu zinabana. Na hao wanaobisha na kuona kuwa ni mambo ya kiswahili waende kwa Nassoro Mkata Vimeo Wakaone Idadi ya watu wanaokuepo hapo na status zao ili wajue.
   
 20. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Tatizo wengi wetu ni wavivu wa kudocument vitu, kiasi kwamba argument zetu zote zinakuwa baseless! Ukisifia kukata vimeo na eti kuna faida kwa watoto wenye kikohozi....wapi machapisho? Huwezi ukachallenge sayansi bila tafiti na machapisho, huwezi kusema inasaidia wakati wakata vimeo hata hawajui hao watoto wanakohoa kwa sababu gani (Diagnosis), uliona wapi mtu anatibu ugonjwa bila kujua ni ugonjwa gani? Hata mpiga ramli atleast amakuambia umelogwa na matibabu yake yatakuwa hivi! Wekeni evidence hapa kuwa inasaidia sio tuinabishana bila evidence.
   
Loading...