Naombeni connection ya kazi nimekwama kabisa

Kalamu Nzito

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
318
662
Wakuu nina degree ya sheria ambayo nimeipata kwa mbinde sana (mishale mingi bado kidogo ni-disco). Nimeenda law school nikasema ngoja nikaze walau nitoke first seat kusafisha maumivu ya degree, ila wapi. Nikakamatwa vimeo vitatu somo moja (pale law school tunaita “full suit”). Nimechomoa kimeo kimoja. Hivyo vingine viwili huu unaenda mwaka wa tatu sijafanikiwa kuchomoa.

Sina ajira mpaka sasa. Naishia kufanya tu internship bila malipo. Sijui naanzia wapi nifanikiwe na umri nao unasogea. Moyo unanisukuma kukata tamaa lakini katika hilo nimeshinda kwani bado ninalo tumaini kwamba nitafanikiwa tu.

Ombi langu kwenu;

1. Kama kuna sehemu wanashea nafasi za kazi/fursa yoyote naaomba nikumbukwe.

2. Kama unaweza binafsi kuniunga mahali nikafanya kazi basi nitashukuru sana.

Mwisho kabisa, wakuu hii maisha inatunyoosha wallah Mungu atusaidie sana.
 
Pole mkuu, utafanikiwa tu sababu ni mtu wa kuhakikisha mbio unazozianza unazimaliza. Pambana na law school ukipata mhuri uokote hata hizi za mikataba kama ajira itachelewa.

Umenikumbusha kuna mtu mwaka wa kwanza tu wa masomo advance aliona atapoteza muda kwani anatumia nguvu kufaulu akaacha akaenda kozi fupi fupi hizi, niliambiwa wakati tuko mwaka wa pili advance yeye alishakuwa kazini, mpaka tunaingia chuo alikuwa kampuni nzuri tu nikajifunza kuwa hii nchi wakati mwingine masomo kuwa magumu ni ishara kutoka mbinguni kuwa unapoteza muda.
 
NAFASI 8 MPYA ZA AJIRA KATIKA SHIRIKA LA BRAC MAENDELEO TANZANIA.

Mwisho wa Kutuma Maombi: 11th December, 2023.

KUSOMA MAELEZO KAMILI NA KUTUMA MAOMBI, Bonyeza Hapa

JESHI: NAFASI 200 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.
Link Nafasi 200 za Ajira Mpya JESHI la Zimamoto Tanzania December, 2023 | Apply Now

NECTA: MATOKEO YA DARASA LA SABA 2023 MIKOA YOTE | YACHEKI KIRAHISI HAPA!
Link AjiraLeo Tanzania

KUCHEKI NAFASI NYINGINE MPYA ZA AJIRALEO, BONYEZA HAPA AjiraLeo Tanzania

NOTE: IKIWA LINK HAIFUNGUKI/INASUMBUA, SAVE NAMBA YA ALIYEZITUMA au INSTALL APP YA AJIRALEO - ELIMU NA KAZI.

SAIDIA WANAOTAFUTA FURSA NA AJIRA, SHARE MAGROUP MENGINE TAFADHALI!

Uwe unapitia hapo, kuna siku Mungu atabariki,
 
Pole sana endelea kupambana wala usikate tamaa kabisa, wakati wa Mungu ni wakati sahihi, Mungu afungue Mlango wa Ajira kwako.
 
Pole mkuu, utafanikiwa tu sababu ni mtu wa kuhakikisha mbio unazozianza unazimaliza. Pambana na law school ukipata mhuri uokote hata hizi za mikataba kama ajira itachelewa.

Umenikumbusha kuna mtu mwaka wa kwanza tu wa masomo advance aliona atapoteza muda kwani anatumia nguvu kufaulu akaacha akaenda kozi fupi fupi hizi, niliambiwa wakati tuko mwaka wa pili advance yeye alishakuwa kazini, mpaka tunaingia chuo alikuwa kampuni nzuri tu nikajifunza kuwa hii nchi wakati mwingine masomo kuwa magumu ni ishara kutoka mbinguni kuwa unapoteza muda.
Habari Mkuu, Uliyo andika yana ukweli 100%. Nakumbuka wakati niko Uboyzini Old Moshi,Mambo yalikuwa magumu sana.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom