Kukariri darasa

Kukariri darasa

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
2,608
Reaction score
2,064
Wadau, naomba ufafanuzi kama hili linawezekana katika utaratibu Wa sasa ,maana nimepata kigugumizi kidogo.

Kuna Dada yangu kijana wake yupo kidato cha 3 (form three) Uwezo wake darasani ni Wa kati, hivyo mzazi wake anapenda kijana wake, arudie darasa kwa maana ya kumuhamisha toka shule aliyopo na kuhamia shule nyingine mwakani kwa kidato hicho hicho cha 3.

Kwa ufupi, asiingie kidato cha NNE( form IV) ahsante ni.
 
Huyo dada yako ana tatizo gani ?
Mwambie amuache dogo asome.
Afu uwezo wa kati haimaanishi ata fail form 4.mwambie dogo akomae na masomo anayoweza
 
Mambo hayo yameshapitwa na wakati japo inawezekana, ila mwachenj dogo amalize shule mambo mengine mtajua mbele unaweza kumrudisha ndio akaaribikiwa kabisa maana mtakuwa mmem discourage
 
Hiki kiswahili cha kukariri darasa kina ukakasi,nani ameweka kwenye matumizi hayo, nijuavyo kukariri sii kurudia bali ni kukimeza kitu kilivyo na kukitapika kama kilivyo kwa kuelewa ama kutoelewa maana yake
 
Mambo hayo yameshapitwa na wakati japo inawezekana, ila mwachenj dogo amalize shule mambo mengine mtajua mbele unaweza kumrudisha ndio akaaribikiwa kabisa maana mtakuwa mmem discourage
Sio kweli mkuu,mimi nilifanikiwa kuwakaririsha watoto wangu hawakuwa vizuri darasani lakini sasa hivi huwezi amini kila mtihani wako top 10.ila kazi yake sio ya mchezo kuna usumbufu wa hali ya juu sana kwani serikali hairuhusu kukaririsha mwanafunzi darasa mpaka kuwe na sababu nyingine na sio kuwa na uwezo mdogo....
 
Wadau, naomba ufafanuzi kama hili linawezekana katika utaratibu Wa sasa ,maana nimepata kigugumizi kidogo.

Kuna Dada yangu kijana wake yupo kidato cha 3 (form three) Uwezo wake darasani ni Wa kati, hivyo mzazi wake anapenda kijana wake, arudie darasa kwa maana ya kumuhamisha toka shule aliyopo na kuhamia shule nyingine mwakani kwa kidato hicho hicho cha 3.

Kwa ufupi, asiingie kidato cha NNE( form IV) ahsante ni.
Kurudia darasa kwa mwanafunzi lazima kuwe na sababu za msingi km vile ugonjwa nk pia na kuwe na supportive document. Lkn kwa hili la uwezo wa kiakili ili ufanikiwe ni lazima uzunguke mbuyu utafute sababu strong(udanganye) ndipo itakuwa rahisi.
Kumbuka government work on paper
 
Huyo dada yako ana tatizo gani ?
Mwambie amuache dogo asome.
Afu uwezo wa kati haimaanishi ata fail form 4.mwambie dogo akomae na masomo anayoweza
Hana tatizo, umetoa ushauri mzuri, ntaufikisha kwa mzazi na mwanafunzi kwa faida ya wote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom