Mtemi Mbojo
JF-Expert Member
- Apr 27, 2017
- 2,290
- 3,974
Napenda kuanza kwa kuwasalimu,Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..........
Nikiwa kama MDAU wa Elimu Tanzania (Bara na Visiwani) kwa muda, nimekuwa namfuatilila huyu Mtanzania ,ambaye nadhani kwa sasa anasoma nchi Marekani, Onesmo Mushi @EdutalkTz kupitia Mtandao wa X zamani Tweeter. Mtanzania huyu amekuwa akitoa mchango mkubwa wa kimawazo kupitia Mtandao huu wa X kwa muda mrefu sasa.
Sehemu kubwa ya Mchango wake amekuwa akijitahidi kuonyesha ufaulu wa wanafunzi hasa kwa Matokeo ya Kidato cha IV, hasa wilaya Temeke hususani kwenye shule hizi za Serikali maarufu kama Shule za Kata,amejaribu kuonyesha
i.UFAULU ulivyo na changamoto zilizopo kwenye shule zetu hizi pendwa,
ii. Kikwazo za LUGHA ya kiingereza na namna kinavyoathiri maendeleo na ufaulu wa watoto wetu
iii.Mwisho amekuwa akiishangaa Jamii na serikali kwa ujumla tunavyoyachukulia kirahisi matokeo ya watoto hawa waliomaliza Kidato cha nne kwa Kupata division IV na 0. Sehemu kubwa ya Jamii tumekuwa tunaona ni SAWA tu kwa kijana kwenda shule na kupata haya madaraja..Mbaya zaidi daraja IV, huchukuliwa ni kundi lililofaulu pia
Mwito wangu kwako Waziri na timu yako hebu jaribuni kumsoma huyu Mtanzania, ikiwezekana hata kuwasiliana nae, kwa ufafanuzi zaidi..Naamini ana KITU ambacho tukikifanyia kazi,sekta hii NYETI ya Elimu inaweza boreka kwa kiasi flani