Kukamatwa kwa ndege yetu Afrika ya Kusini: Hakuna la kushangilia wala kuhuzunikia. Kisheria, kila jambo hadi sasa liko sahihi na mambo yatakuwa sawa!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Kwanza, kuna kukubaliana kwa hoja kuwa aliyefungua shauri nchini Afrika ya Kusini na kupata amri ya kuishikilia ndege yetu huko anaidai Serikali(kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali, anaidai Serikali ya Tanzania kiasi cha dola milioni kumi za kimarekani).

Pili, Mahakama Kuu ya Afrika ya Kusini (kama zilivyo Mahakama zetu hapa Tanzania), ina mamlaka ya kupokea na kusikiliza mashauri yanayofunguliwa kwa mujibu wa sheria za Afrika ya Kusini ikiwemo ya MDAI wa Tanzania. Pia, ina mamlaka ya kushughulikia shauri hilo na kutoa amri zinazopasa kwa mujibu wa sheria za huko.

Tatu, naamini kuwa kuna Maombi Madogo na Maombi ya Msingi yaliyofunguliwa na MDAI wa Tanzania huko Afrika ya Kusini. Maombi Madogo (ambayo yaweza kuwa yaliwasilishwa kwa Hati ya Dharura) yalihusu kuizuia ndege ya Tanzania (kama mali ya MDAIWA) hadi pale Maombi ya Msingi yatakaposikilizwa. Maombi ya Msingi yanahusu hasa deni husika na gharama nyinginezo za kisheria.

Nne, Maombi Madogo (kama ilivyo hata hapa kwetu) huweza kusikilizwa baina ya pande zote (inter-partes) au upande mmoja (ex-parte). Daima, kusikilizwa Maombi kwa upande mmoja hutegemea uharaka wa jambo linalohusiana na Maombi hayo. Mfano, hapa kwetu Tanzania Maombi mengi ya kuzuia mnada wa hadhara na mengineyo yenye uharaka kama hayo husikilizwa upande mmoja (MUOMBAJI husikilizwa peke yake). Maombi ya Msingi husubiriwa.

Tano, Maombi Madogo hayo pia husikilizwa baina ya pande zote baada ya MJIBU MAOMBI/Tanzania kupatiwa nakala za Maombi na nyaraka za kuitwa Mahakamani. HIYO NI NAFASI YA KWANZA kwetu kuiondoa amri hiyo ya kuishikilia ndege iliyotolewa kwa upande mmoja (yaani ex-parte). Hilo laweza kufanyika kutegemeana na athari za amri iliyotolewa ex-parte na hoja pamoja na uhalali wa kutolewa kwa amri hiyo.

Sita, baada ya pande zote kusikilizwa kwenye Maombi Madogo na uamuzi kutolewa wa ima kuizuia ndege au la, Maombi ya Msingi yataanza kusikilizwa. Yawezekana, MDAI aliharakisha na kusikilizwa peke yake/upande mmoja kutokana na sababu kuwa ndege yetu ingetua na kuruka kutoka nchini Afrika ya Kusini. Labda kuizuia ni 'kuishinikiza' Serikali kuharakisha kusikilizwa na kulipwa kwa deni husika.

Saba, tayari timu ya Mawakili nguli na wabobezi wa Serikali wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dr. Kilangi ilishatua Afrika ya Kusini ili kuweza kusimamia, kuratibu, kutatua na kumaliza sintofahamu ambayo ni ya kisheria. Hadi sasa, hakuna la kushangilia wala la kuhuzunikia. Ndege ni yetu na nchi ni yetu. Uzalendo wetu utusukume kuunga mkono juhudi za Serikali katika kulishughulikia suala hili na kulimaliza. Mambo yote yatakuwa sawa!
 
Ujue mdai anachotaka ni kulipwa kwa mujibu wa hukumu ya mahakama ya miaka ya 90 ambayo serikali ilii kaidi.

Sidhani kama kuna dawa zaidi ya ama KULIPA au kufanya MAKUBALIANO MAPYA yenye dhamana ya kulipa.

Jopo la mawakili kwenda huko ni ku-panic tu, dawa ya deni ni KULIPA.
 
Asante Petro, hawa wananchi walinituma kuulizia maendeleo ya ndege yao

1566902233885.jpeg
 
Mtoa hoja umeelezea vema ingawa mwishoni umeingiza siasa na suala hili SI la kisiasa ni la kisheria,na tuelewe hii ndege imeshikiliwa kwa AMRI ya mahakama SIO serikali ya SA(ILA TUELEWE KUWA SA imesahini mkataba wa kuruhusu kitu kama hiki kutokea)kuna mifano mingi tu ya mali kuzuiwa kwenye nchi iliyotia sahihi mkataba huu,ni wajibu wa nchi yangu kupambana zaidi kisheria ili mwafaka utokee sio kuliweka suala hili kisiasa.tujitahidi tujenge utetezi wetu ulio water tight ili kuinusuru ndege yetu,na mbaya zaidi hatujui nani atawajibika kulipa gharama za eneo ilipopakiwa hii ndege yetu pale OR Tambo Airport.,kama ni mlalamikaji ndie anayetakiwa kulipa its ok ila kama ni sisi,itabidi jop[o hili lifanye kazi kwa uharaka na ufanisi ili kuitoa ndege hii.
 
Asante Petro, hawa wananchi walinituma kuulizia maendeleo ya ndege yao

View attachment 1191183

Haaaa haaaa, hii picha imenikumbusha picha fulani wakati wa ile ripoti maarufu ya makinikia, zilikuwa zinawekwa picha cha watoto kama hawa na watoto wa kizungu ambao wanafaidi madini yetu. Ila sasa hivi madini yetu hayaibiwi lakini bado watoto masikini hivyo wapo!
 
walipata wapi ndege hawa wachafu hivi?

hivi wanalipa kodi kweli hawa? au wanatudandia tuu! mikoani bana! bongo hkn wa hivi!

ombaomba wa bongo ni wasafi, ngozi lainiii sababu ya joto.
Hivi unaelewa kuwa wazazi wa hawa watoto ndiyo wakulima wa alizeti , korosho, pamba, miwa nk. Mpaka sasa hawajapata soko linaloendana na nguvu ya kazi zao.
Kodi na Mauzo ya mazao hayo ndiyo yamekupeleka shule na kulipia mshahara wa daktari anaekutibu
 
Back
Top Bottom