Kujiuza

Kujiuza

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,010
Reaction score
60,472
Mara nyingi tunasikia na kuona watu wakinyooshewa vidole kua "wanajiuza tu hao" au "anajiuza tu huyo".

Sasa nimejikuta najiuliza Je kujiuza kunaanzia wapi na kuishia wapi? Ni mpaka mtu atilie pamba matata na kusimama barabarani huku akisubiria atakaevutiwa nae atokee? Ni mpaka mtu awe na buzi ambalo linamuweka mjini? Vipi anaeoa/olewa kabisa kwasababu ya pesa na sio mapenzi. . . huyu nae anajiuza?
 
Kujiuza katika mapenzi ni kufanya ngono bila kuwa na mapenzi ya kweli na unayefanya naye ngono kwa ajili ya kujipatia faida ya aina yeyote iwe pesa, vitu, ulinzi n.k
 
Leo.... Kazi kweli kweli.

Hata kama anafanya hivyo kwa kulipwa, kwani anapo do nae haoni raha?
 
kuna makundi mawili ya kujiuza 1. profesheno 2. Ridhaa........
1. lazima ulipie....
2. bure bure........maneno yako tu...
 
Kujiuza katika mapenzi ni kufanya ngono bila kuwa na mapenzi ya kweli na unayefanya naye ngono kwa ajili ya kujipatia faida ya aina yeyote iwe pesa, vitu, ulinzi n.k

una akili sana kongosho! Wewe wera, yaani kwa hii definition ni kuwa hata nyumba ndogo ni sawa na changudoa anayejipanga pale kimboka,corner bar,ohio,au jolly ili apate chochote.
 
Si nyumba ndogo tu
Unaweza jiuza kwa mumeo au mkeo

Ukiolewa mtu kwa ajili ya maslahi binafsi bila kuwa na upendo wa kweli afu ukawa na mahusiano na mtu mwingine unayempenda kwa dhati ni kujiuza tu ila unakuwa na heshima mbele za watu.

una akili sana kongosho! Wewe wera, yaani kwa hii definition ni kuwa hata nyumba ndogo ni sawa na changudoa anayejipanga pale kimboka,corner bar,ohio,au jolly ili apate chochote.
 
una akili sana kongosho! Wewe wera, yaani kwa hii definition ni kuwa hata nyumba ndogo ni sawa na changudoa anayejipanga pale kimboka,corner bar,ohio,au jolly ili apate chochote.

nani alikwambia kila nyumba ndogo inakuwaga nyumba ndogo ili ipate hela?
 
Kujiuza katika mapenzi ni kufanya ngono bila kuwa na mapenzi ya kweli na unayefanya naye ngono kwa ajili ya kujipatia faida ya aina yeyote iwe pesa, vitu, ulinzi n.k

kama ni kufanya ngono bila kuwa na mapenzi bali kwa ajili ya kujipatia chochote,inamaana hata huyo mwanaume anayemchukua changudoa pia anajiuza ili ajipatie starehe..si ndio?am just thinking
 
hilo ndilo swali gumu sana huwa najiuliza hasa ninapokatiza mitaa ya kona bar ila wengi wao huwa wanadai ni njaa ndio zinawasumbua..
 
kwani kujiuza kuna jinsia?
Kwa nini unadhani mwanamme hawezi jiuza?

Kwenye changu na mteja, mwanamme ananunua maana yeye anakuwa ameamua kufanya mapenzi.

kama ni kufanya ngono bila kuwa na mapenzi bali kwa ajili ya kujipatia chochote,inamaana hata huyo mwanaume anayemchukua changudoa pia anajiuza ili ajipatie starehe..si ndio?am just thinking
 
hata nyumba ndogo inajiuza kama imefuata faida yeyote pale isipokuwa upendo.

Swali, je unaweza penda kwa dhati mtu ambaye tayari ana mtu mwingine kihalali?

nani alikwambia kila nyumba ndogo inakuwaga nyumba ndogo ili ipate hela?
 
hii thread mtaishia kutukana watu weengi bila kupata muafaka.....

definition ya kujiuza ni kubwa saana...

ndo maana hata wasioolewa huambiwa 'hawana soko'
au 'hawajapata soko'......

shakespeare alisema 'nothing is good or bad only your mind makes you think so'....
 
kwa hiyo unataka mods waifunge? Ngoja wenye kudadavua mambo waje watuweke sawa.
 
Mara nyingi tunasikia na kuona watu wakinyooshewa vidole kua "wanajiuza tu hao" au "anajiuza tu huyo".

Sasa nimejikuta najiuliza Je kujiuza kunaanzia wapi na kuishia wapi? Ni mpaka mtu atilie pamba matata na kusimama barabarani huku akisubiria atakaevutiwa nae atokee? Ni mpaka mtu awe na buzi ambalo linamuweka mjini? Vipi anaeoa/olewa kabisa kwasababu ya pesa na sio mapenzi. . . huyu nae anajiuza?

kwa mantiki ya mapenzi, kuuza ina maanisha yeyote mwenye fedha anayeza hudumiwa, au tuseme kila huduma inalipiwa. Inapokuja kenye ndoa, aliyeingia kwa ajili ya fedha basi huyu yuko kwenye ajira ambayo ni kutoa penzi kwa malipo anuai toka kwa mwajiri huyu mmoja tu.
 
Back
Top Bottom