Kujitoa CWT na kujiunga CHAKAMWATA

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,781
6,065
Habari ndugu walimu,

Kama title I navyojionyesha kumekuwa na malalamiko na manung'uniko kuhusu huyu mdudu CWT kuwa ni mnyonyaji wa walimu na sio msaada tena...mimi nilikuwa mmojawapo wa watu niliyeiponda CWT hadharani.

Hata hivyo nikapata wadau wengine ambao tulishauriana badala ya kupiga kelele kwenye media ni bora kuchukua hatua. Tumeanza harakati hizo na hadi sasa tupo sehemu nzuri tuna machaguo mawili (a) kujiunga na chama kipya cha walimu (Chakamwata) ambacho kimeanza Kule mbeya au (b) kuanzisha chama kingine mbadala.

kwahiyo kwa sasa tupo na mchakato huo kwa yeyote anayeichukia CWT anaweza kujiunga nasi. Kumbuka huwezi kujitoa CWT kama hutakuwa na chama mbadala...nawatakia kila la kheri walimu wenzangu tusipigane vita ya mdmomdomo...kwa ufafanuzi wowote Katibu inbox
 
Habari ndugu walimu...
Kama title I navyojionyesha kumekuwa na malalamiko na manung'uniko kuhusu huyu mdudu CWT kuwa ni mnyonyaji wa walimu na sio msaada tena...mimi nilikuwa mmojawapo wa watu niliyeiponda CWT hadharani Hata hivyo nikapata wadau wengine ambao tulishauriana badala ya kupiga kelele kwenye media ni bora kuchukua hatua ...Tumeanza harakati hizo na hadi sasa tupo sehemu nzuri tuna machaguo mawili (a) kujiunga na chama kipya cha walimu (Chakamwata) ambacho kimeanza Kule mbeya au (b) kuanzisha chama kingine mbadala.
kwahiyo kwa sasa tupo na mchakato huo kwa yeyote anayeichukia CWT anaweza kujiunga nasi. Kumbuka huwezi kujitoa CWT kama hutakuwa na chama mbadala...nawatakia kila la kheri walimu wenzangu tusipigane vita ya mdmomdomo...kwa ufafanuzi wowote Katibu inbox
Kumbuka kila siku mtawala anafurahia anapoona migogoro katika vyombo vya ushirikishwaji. Hili sio geni kwetu tunaliona katika vyama vya siasa! Wingi wao unamfanya mwenye madaraka aendelee kuitawala nchi. Kwa, hili mnalotaka kulifanya linaweza likawa sio suluhisho bali kuongeza suluba kwa mwalimu.
Hebu fikiri, mwalimu amehama CWT baada ya siku kadhaa huko alipohamia ukizuka mgogoro (Na mara nyingi pale furusi inapoongezeka) anakuwa katika kizungumkuti na hajui pa kwenda. Kwa yakini kabisa, je, mtakuwa mmemsaidia au mmempotosha mwalimu pindi mtakapoanza migogoro ya kiuongozi katika hicho chama kipya? Je, mmeshindwa kuwaondoa viongozi wa CWT waliopo madarakani?
Nia yangu sio kutaka kuwakwaza ila natoa angalizo kwa hili wazo mnalotaka kulifanya.
 
me naungana na KWEZISHO kaeni chini mjaribu kusolve tofauti zenu,, kama tatzo ni mfumo muubadili, kama tatzo ni viongozi andaeni hoja za msingi za kuwashinikiza waachie ngazi.. matatzo huwa hayaishi popote even hata kwenye family zenu migogoro ipo sana tuu, lakini issue sio hyo migogoro issue ni how unaitaftie ufumbuzi? You won't know the worth of something until you leave it..
 
jamani sasa sisi ambao ndo tunapewa ajira soon mnatushaurije....? tuachane na cwt......? nahichi kipya je kipo halali kisheria...? tupeni mwangaza tusije tukakosea mapema...
 
Naamini CWT ni mafisadi tena sana,ila siungi mkono hoja yakuanzisha chama kipya,badala yake nashauri ya fuatayo:
1.Katiba ya CWT ipitiwe upya ili kubaini mapungufu na kuyarekebisha.
2.Mapato ya chama yawekwe bayana na matumizi yake.
3.Ifanyike Auditing KATIKA mali za CWT na repoti ipelekwe kwa wanachama ikajadiliwe
4.Makato ya mshahara yapungue na kuwa kiwango kimoja km vile 2,000/=kwa mwezi kuliko asilimia hiyo 3 au 2inayokatwa sasa hivi kwani:
i.Chama kina rasilimali nyingi kwa sasa tosha kuendeshea chama
ii.Chama kina ingiza wanachama wengi kwa mwaka kutokana na ajira za walimu takribani 25,000 kila mwaka walimu wapya huajiriwa,hivyo michango ya fedha ni nyingi.
iiii.Kiwango cha asilimia 2 au 3 inayokatwa sasa siyo lazima,kwani kiwango hicho kilipangwa wakati chama kikiwa kichanga na kinahitaji mapato mengi kujiendesha,kwa sasa kiwango hicho ni kikubwa.
5.Mfumo wa kuwatunza wanachama wastafu uangaliwe upya,kwani si haki mwanachama amekichangia chama kipindi chote cha utumishi halafu akistaafu aishie kupewa bati 20,atafanyia nini? bati 100 angalau na inawezekana,au apewe mkono wa kwa heri 1,500,00 0/=
6.Mikutano ya mara kwa mara na wanachama na viongozi wakuu iwe inapatiwa kipaumbele nk.
Haya ni mambo machache ya kushughulikia na wengine wanaweza kubainisha na mengine,changamoto hizi zikitatuliwa chama ni kizuri,
Kubomoa nyumba unayoishi na kujenga mpya kwa mara moja si jambo jepesi.
Pia ili kujitoa kutoka chama kilichopo na kujiunga na chama kipya bila kubainisha changamoto zilizopo katika chama cha awali ni kazibure.Utajuaje kama chama kipya hakitakuwa na matatizo?
Karibuni kwa maoni.
 
Mimi ni mmojawapo kati ya wapinzani wakubwa tunaopinga udhurumati unaofanywa na CWT, hapo mwaka 2014 tulifanya mikutano ya kuwahamasisha walimu wamuogope mdudu huyo na kuachana nae na wajiunge na CHAKAMWATA wajumbe wengi walituunga mko ila kuna mkono wa wakubwa serikalini wakatia vikwazo kibao, ila hatujakata tamaa tutarudi
 
kianzishwe chama cha Walimu wa kutoka mbinguni pekee....... lakini eti wajitoe CWT!? Kuna tofauti gani kati kifuniko na kizibo?
 
Nasikitika sana ninapoona walimu tukilikimbia tatizo Kwa naona hiyo.Ebu tujishughulishe kusoma sheria za kazi na mahusiano kazi ni na trade union act tuweze kujua CWT IPO kisheria au LA.Mie nilikuwa kati ya walalamikaji naomba moja kuhusu CWT lakini nimeelimishwa nakujua kuwa CWT ndicho chama pekee cha wafanyakazi kinachoweza kumtetea mwalimu.Marekebisho ya katiba yalifanyika mwaka 2014 lakini kama tulivyo diku zote walimu kwenye uelewa has a graduates tulijitenga na kazi hiyo tukawachia grade A waturekebishie katiba.Chama ni kizuri ila niwaombe has a walimu Wa sekondari tushiriki chaguzi ili kupata viongozi kwenye maono na siyo uongozi Wa mazoea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom