Kujishusha!!.....

Mimi ni mzito wa kujishusha hasa kama sijafanya kosa!
Hii kujishusha inayozungumziwa hapa umeielewa lakini? sio ile kujishusha ya "over 18 self service" bana ni kujishusha ya kuomba msamaha. haya fafanua zaidi tukuelewe sasa
 
mimi ninachopinga ni kuwa the price ya kuifanya ndoa idumu isiwe kubwaa saana
mpaka raha isiwepo.....

Boss, hata kama price ya kufanya ndoa iwepo lakini isiwe kwa kujishusha tu bila kuelewa kosa na kujirekebisha..mana mwishoe kuombaa msamaha na kujishusha inakuwa mazoea, mtu haoni uzito wala kukiri kosa..

Una akili kama babu yangu....ndoa sio mapambano...watu wanapambana mpaka kukosa usingizi eti ili tu ndo iwepo!!!

Huyo ndo boss inabidi uwe na kifua kupambana nae..haki tena mahusiano zinakosesha usingizi wengi sembuse ndoa ambapo ndiyo kifungo!..inabidi tuchukue muda kuwasoma wandani wetu na kudeal nao inavyotakiwa ila tu siyo kukomoana mana kuna wengine huo ndiyo uwanja wao.

wakati mwingine ukiwa mtu wa kujishusha mara zote utakuwa waonekana *****(kwa baadhi ya watu). so minadhani unajishusha lkn ukiona mtu mwenywew haelekei nawe unakomaa tu.

ha ha, hadi munkari zimekupanda!..ukiwa na mwandani mwerevu lazima awe na akili ya kuelewa kuwa umejishusha kwa njia njema siyo kudhauliana tena baada ya hapo..sasa ukikomaa na yeye akikomaa inakuwaje?au ndiyo imetoka hiyo?
wahenga wanasema aliyejuu mgonje chini ati!!
 
I love to apologise (kama hii ndio kujishusha aliokusudia mleta mada), Actually it is the best romance if you do it right.

Kloro mwana, ku-apologise ukiwa umekosea kuna maana sana mana unajua ulilokifanya..sasa kama amekutendea vibaya mwandani wako, je utaomba msamaha? au utajishusha halafu baadae mazingira yakiwa safi unashusha neno kwa bibie ajirekebishe ulikosea A na B...
How do you do it right?

Chuma hufua chuma sipendi mtu anayejishusha na kuninyenyekea as if I'm a feudal lord au slave master.
Kila mmoja lazima awe na sauti kueleza, kujadili, kuepress msimamo na hisia zake. Hiyo management of luv relation kwaaliyekosa na kukosewa.

nimependa mtazamo wako, kila mmoja awajibike na makosa yake..hata kunyenyekewa kila mara wakati wewe ndiyo mkosaji haileti maana halisi ya msamaha mana ni kama kutekeleza wajibu tu..

Mie kama nimekosea napenda tuongee na huwa niko open kukubali kosa langu lakini pia huwa napenda kusema kitu gani kilinifikisha kufanya kosa hilo hili mwenzangu haweze kujua na kujirekebisha kama alichangia mimi kufanya kosa hilo.Na nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kujaribu kurudisha hali ya kawaida ndani ya nyumba.

Sipendi mambo ya kukumbushiana makosa au mambo ya mtu kusamehe huku bado body language yake haioneshi kama kasamehe.

AW nimekusoma mkuu na nimependa mtazamo wako wa kukabiliana na mushkeri za hapa na pale!..je ukikosewa unapenda uombwe msamaha? au unaweza kuendelea kujishusha ili kuleta hiyo amani? au unaonaje kama wote wawili kuwajibika tatizo linaposababishwa na mhusika?
Kwenye kukumbushia nadhani mie mbovu kabisa, huwa siwezi kusahau na siku ya siku napendaga kufukunyua..ina-cost si kidogo kwa kweli!!
Najaribu kupambana ili nikiwa kwenye mahusiano niishi maisha ya sasa siyo past kila siku.
Wote tunakosea na ni vizuri tukijifunza kusamehana na tujifunze kutambua makosa yetu hili tusirudie makosa yale yale mbeleni.[/QUOTE]
 
Chuma hufua chuma sipendi mtu anayejishusha na kuninyenyekea as if I'm a feudal lord au slave master.
Kila mmoja lazima awe na sauti kueleza, kujadili, kuepress msimamo na hisia zake. Hiyo management of luv relation kwaaliyekosa na kukosewa.

babu una mabusara kibao.
Ukijishusha sana hata mtu wako anakuona mjinga.
 
kwa ninavyojua mimi wanaume wengi ni wagumu katika kujishusha na kama akijishusha kwa hilo ni lazima na yeye akutafutie sababu.

ma'swagga hivi ndivyo nilivyokuwa naamini mimi!! Wanawake ni wepesi kujishusha but leo nimepata perception nyingine kuwa wanawake ndo wanaonekana ni wagumu kukiri.
 
Kloro mwana, ku-apologise ukiwa umekosea kuna maana sana mana unajua ulilokifanya..sasa kama amekutendea vibaya mwandani wako, je utaomba msamaha? au utajishusha halafu baadae mazingira yakiwa safi unashusha neno kwa bibie ajirekebishe ulikosea A na B...
How do you do it right?
.
[/QUOTE]

Unalipiza kisasi cha Manu nini? naona masuali magumu kama interview ya Pentagon! heheh

Bek to suali lako: Unajua jambo lolote linalohusu mahusiano kwanza unapaswa umuelewe mwenza wako zaidi kuliko kujielewa mwenyewe, Kuna mwenza anaweza akaabyuzi udhaifu wako na kuna mwenza anaziba udhaifu wako kwa kujirekebisha.

Sasa kama una mwenza ambae anatafuta udhaifu wako autumie basi utahitajika kujishusha pale umefanya kosa tu na pia kwa tahadhari kwani anaweza akalitumia kosa lako kukuhukumu milele. Ila kama mwenza wako unapojishusha anaonesha kubadilika kutokana na kujishusha kwako basi ni vyema ukajishusha hata pasipobidi kujishusha na nakuhakikishia mwenza wa namna hii mwisho atajifunza kwako kujishusha na mwisho mtakuwa mnagombaniana kujishusha.

I might be wrong! Leo nina njaa ajabu pointi hazikuji.
 
kujishusha ni tabia ya mtu,anybody can groom to it. tatizo linakuja kwenye definition ya 'kosa'. it is a relative term lakini kuna wanandoa wanafanya maisha kuwa magumu.kuna mwanaume anataka mkewe aombe ruhusa ya kusafiri kikazi, kuhudhuria issue za ndugu zake etc. ila kujishusha mahali popote pale ni muhimu, iwe kwa mwenza,kwa ndugu(wa pande zote), kazini na hata kwa majirani.
kuhusu mwenza kuwa hakubali kujishuha hata kama amekosea,naamini kwenye kumpa kila mtu nafasi ya kufikiria juu ya kilichotokea,they ussually come around na kugundua. just dont overdo it and dont stress over petty stuff,ladha ya maisha inapungua.

Kweli kabisa kuna wanandoa/wapenzi wengine wanafanya maisha magumu kwa vitu vidogo yani mwingine hata uwe jinga kwa kujishusha shusha kila mara anajifanya yeye ndie kinara sasa mtu unabaki kushangaa kama hayo ni mashindano au mapenzi..
Naamini katika maisha haya japokuwa kila mtu ana kasoro zake na hamna malaika ila kuna watu wengine wanaishi vizuri tu kwa kuweza kusuhisha matatizo yao bila kukomoana.
Hamna kitu chenye raha kama mtu amekosea, kakiri na kujishusha pia asirudie makusudi kana kwamba ataomba msamaha tu yaishe...Asante kwa inputs zako!

It depends kuna kipindi najishusha hata kama sio mwenye kosa ila makosa mengine lazima nipandishe ili next asirudie..alafu sipendi mambo ya kukumbushiana makosa ya zamani

balance yako nzuri sana..kupanda na kushuka sometimes!!..kukumbushia ni swala gumu, nimejifunza sana kitu hapa..

Mimi ni mzito wa kujishusha hasa kama sijafanya kosa!

Husninyo huyo, yani hata kusema basi leo acha nirekebishe mambo ili tuoge wote jamani? ha ha

kwa kweli belinda mie sina formula inategemea na kosa, nikiona kosa ni kubwa sana nitakumbushia siku mbili tatu hata kama nimesamehe, ndio nilivyo ila sinaga mahasira na magubu ya kuweka vinyongo

ni vyema kusikia hivyo mana u muwazi na nafsi yako...mie suala la kukumbuka nadhani kiki kichwa kimejaa mamabo mengi, nina ubaya wa kukumbushia hata mada au kosa likiwa tofauti..poor me!!
 
sehemu hizi ndio za kuonyesha kwamba alivofany sio vizuri unasubiriaaaa kwenye chorus unaanza kulalama huku chozi linatoka kabisa , kama hivi, mpenzi mbona unanitesa hivi, babe wangu jamani why all this, hapo anakwambia yoote

Kumbe eeeh...............................,
sasa hapo hata concetration kwenye tendo lenyewe si inakuwa haipo BB?
Kwakuwa wewe akili yote umeitegeshea kwenye korasi ili umwage verse zako lol......
 
kukumbushia kosa kunakujaje? tatizo kuna mwenza mwingine yuko too vulnerable with the same kosa! sasa kama ur past kila siku ina-catch up na ww, namaanisha kila wakati unafanya kosa lile lile ila unabadili mtindo lazma utakumbushiwa tu. na hakuachi walau ukasahau,anakuchakachua tena!inakera kukumbushwa lakini ukirudie kosa, utakumbushwa tu somehow! na kuomba msamaha kila mara kwa kosa lile lile (tena kosa strategic,hahaha,with clear planning and repeatitive,lol!), inakuwa haileti maana ya msamaha kamwe!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
King'ast Msamaha tafsiri yake ni kukiri kosa na kuacha kama unarudia kosa wewe hauko tayari na msamaha!Dawa yako ni nyingine
 
mpendwa, kuna tabia ambazo inachukua muda kuacha.mimi humuomba partner wangu anikumbushe kila wakati narudia katabai kabaya... from experience,kuna mazoea hayaondoki mara moja,ila unakuta ni petty stuff ambazo hata mkosaji akifanikiwa kuacha zinampa kuwa mtu bora zaidi. kuna mambo ambayo ni straight forward,nakubaliaba na ww.

King'ast Msamaha tafsiri yake ni kukiri kosa na kuacha kama unarudia kosa wewe hauko tayari na msamaha!Dawa yako ni nyingine
 
jamani mimi gf wangu ni mbish kupitiliza, na hata akikosea hawezi kujishusha au kusema sory hata cku, instead anakugeuzia kosa kwmba we ndio mkosaji, hapa 2lipo 2mefight nachukia sana anapokosea then anakugeuzia kosa. Hivi wanawake wote mko ivi? Je inakuaje kwny ndoa m2 anakaa na mtu 50yrs wanakaaje kama ndo mko ivi?
 
pole,ndo maisha kuvumiliana kaka! ww ungeambiwa ukae na wazazi wako ama kaka zako 50 yrs mngenyofoana nywele. buggy party na jando la jf litakufunza mengi,anzia page 1

jamani mimi gf wangu ni mbish kupitiliza, na hata akikosea hawezi kujishusha au kusema sory hata cku, instead anakugeuzia kosa kwmba we ndio mkosaji, hapa 2lipo 2mefight nachukia sana anapokosea then anakugeuzia kosa. Hivi wanawake wote mko ivi? Je inakuaje kwny ndoa m2 anakaa na mtu 50yrs wanakaaje kama ndo mko ivi?
 
...Tendo lolote (incl kujishusha) kama linakusudia kuondoa/kurekebisha/kusawazisha
kasoro kubwa au ndogondogo kwenye maisha ya mapenzi ni sahihi.

Mbaya ni 'kujifanyisha' (pretending!) Unajishusha wakati nia na madhumuni ni
kutimiziwa kwanza matakwa (yako mtu) binafsi.
Ni bora mtu awe real.
 
Kumbe eeeh...............................,
sasa hapo hata concetration kwenye tendo lenyewe si inakuwa haipo BB?
Kwakuwa wewe akili yote umeitegeshea kwenye korasi ili umwage verse zako lol......
Bacha na wewe kujifanya hujui si anakuwa anakubembeleza, then unakuwa kama hutaki unataka mara kitu na box, hapo ndio nakuwa nimepata pa kulalamikia sasa
 
AW nimekusoma mkuu na nimependa mtazamo wako wa kukabiliana na mushkeri za hapa na pale!..je ukikosewa unapenda uombwe msamaha? au unaweza kuendelea kujishusha ili kuleta hiyo amani? au unaonaje kama wote wawili kuwajibika tatizo linaposababishwa na mhusika?
Kwenye kukumbushia nadhani mie mbovu kabisa, huwa siwezi kusahau na siku ya siku napendaga kufukunyua..ina-cost si kidogo kwa kweli!!
Najaribu kupambana ili nikiwa kwenye mahusiano niishi maisha ya sasa siyo past kila siku.
Wote tunakosea na ni vizuri tukijifunza kusamehana na tujifunze kutambua makosa yetu hili tusirudie makosa yale yale mbeleni.[/QUOTE]

@ BJ, Napendelea kuombwa msamaha kwa vile ni njia moja ya muhusika kuonesha kwamba amekubali kwamba yeye ndio mwenye makosa. Lakini sasa kuna wale amabao wanahisi kuomba msamaha kama kujishusha; wao sio mbaya kama hawatoomba msamaha lakini sipendi pale wanapojaribu kuendeleza zogo kujitetea kwamba hawakufanya kosa. Kuna wale ambao hawwapendi kuomba msamaha lakini watakuonesha kw a njia nyingine kwamba wamekubali wao ndio wamefanya kosa, hao sina wasi wasi nao maisha yanaendelea tu kama kawaida.

Napenda mawasiliano ndani ya mahusiano, yawe negative au positive, kwani kama kuna tatizo nitaweza kurekebisha na kama ni jambo zuri nitaweza kuliendeleza au kuli boresha zaidi.
 
AW nimekusoma mkuu na nimependa mtazamo wako wa kukabiliana na mushkeri za hapa na pale!..je ukikosewa unapenda uombwe msamaha? au unaweza kuendelea kujishusha ili kuleta hiyo amani? au unaonaje kama wote wawili kuwajibika tatizo linaposababishwa na mhusika?
Kwenye kukumbushia nadhani mie mbovu kabisa, huwa siwezi kusahau na siku ya siku napendaga kufukunyua..ina-cost si kidogo kwa kweli!!
Najaribu kupambana ili nikiwa kwenye mahusiano niishi maisha ya sasa siyo past kila siku.
Wote tunakosea na ni vizuri tukijifunza kusamehana na tujifunze kutambua makosa yetu hili tusirudie makosa yale yale mbeleni.

@ BJ, Napendelea kuombwa msamaha kwa vile ni njia moja ya muhusika kuonesha kwamba amekubali kwamba yeye ndio mwenye makosa. Lakini sasa kuna wale amabao wanahisi kuomba msamaha kama kujishusha; wao sio mbaya kama hawatoomba msamaha lakini sipendi pale wanapojaribu kuendeleza zogo kujitetea kwamba hawakufanya kosa. Kuna wale ambao hawwapendi kuomba msamaha lakini watakuonesha kw a njia nyingine kwamba wamekubali wao ndio wamefanya kosa, hao sina wasi wasi nao maisha yanaendelea tu kama kawaida.

Napenda mawasiliano ndani ya mahusiano, yawe negative au positive, kwani kama kuna tatizo nitaweza kurekebisha na kama ni jambo zuri nitaweza kuliendeleza au kuli boresha zaidi.[/QUOTE]
Well spoken mkuu
 
Back
Top Bottom