Kujishusha!!..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujishusha!!.....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BelindaJacob, May 30, 2011.

 1. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Hello wapendwa,

  Kwa wapenzi/wanandoa linapotokea suala la mifarakano ya hapa na pale mpaka wengine kutaka kuachana, mnalichukuliaje suala la kujishusha? Hapa naongelea kuwa chini (kupunguza hasira/jazba) na kuweza kurudisha amani kwa kuanzisha maongezi au/na kuomba msamaha.

  Pia, ukiwa na mtu asijependa kujishusha ilhali kakosea unakabiliana vipi na hali hii? Mana kuna mtu hakubali kosa yao wala kuomba msamaha hata kama amekosea.

  Wimbo mahususi:- Ain't Too Proud To Beg - The Temptations

  Siku njema katika kulijenga Taifa!...
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Wanawake wachache sana amba ukijishusha
  na kuomba msamaha hata kama kosa ni lake ,mambo yanakwisha na kuwa mazuri...

  Wanawake walio wengi ukijishusha na kuomba msamaha.....

  1.anakupanda kichwani na kuongeza ujeuri

  2.anahifadhi hilo kosa,na kila siku utakumbushwa kuwa

  alikusamehe kosa siku fulani.....

  I prefer kuomba msamaha kwa vitendo....

  Zawadi hivi,au out ya nguvu......
   
 3. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mmh then one of the couple should see more by his head than feelings/emotions. wote mkiwa juu, it is the end of the road...

  Mimi huwa najishusha....
   
 4. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Yah,ni jambo la maana kujishusha hasa pale utakapojua kuwa umekosa,lakini pia hata kama hujakosa inapotokea misunderstanding ni vizuri ukawa mtulivu na kutatua tatizo,ndoa yenu itakuwa njema,kutofautiana kwa binadam ni kawaida na msichukulie hilo kama tatizo labda iwe kwa kila siku au kwenye kila jambo!
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  As for me, zawadi and outing do not matter in this case! zawadi na outing zina maana gani kama hatuelewani?

  I prefer to talk about it and kiishe.... zawadi and outing baadaye!
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mhhh nimesahau kama mimi hua najishusha au najiweka juu kama mlima Sayuni!Ngoja nikumbuke mara ya mwisho ilikuaje!!

  Ohhh owkey..last time nilituliza makeke kwa faida binafsi lakini.Ila mara nyingi hua napenda kuongea yaishe...sipendi viporo maana hua naendelea kukasirika kwahiyo nikiona vipi nashuka chini kidogo kumpa mwenzangu unafuu wa kujieleza !

  Mtu kujishusha ni muhimu sana maana ikiwa wote mnajiweka juu tu amani haipatilabi kirahisi na kuachana itakua ni rahisi kama kuagana usiku mwema!Wale wasioweza kufanya hivi inabidi wajifunze!
   
 7. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Lakini hata kama kosa lako huwezi kusema 'samahani kwa hiki na kile' hata kwenye hiyo outing mana lazima kutakuwa na maongezi..Au ndiyo imeisha kijuu juu?..angalau lakini unafanya kwa vitendo.


  Yani kweli mkiwa juu wote, naona ni kuugulia hasira japokuwa kila mmoja anatamani mwenzie aanze..Je unajishusha muda wote hata kama makosa siyo yako?!..huwagi na kinyongo kwamba ni wewe tu kujishusha?
   
 8. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa maana hiyo mie ni mwanamke wa kipekee, napenda nikikosewa tuongee tuombane msamaha yaishe na huwa sikumbushi kabisa makosa yaliyopita, cause na mie huwa nakosea na nikisamehewa sipendi kabisa kukumbushiwa yalopita
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Blackberry hongera kama ni kweli,kip it up!
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Mtazamo wako mzuri ni bora kutatua matatizo yakaisha..kwahiyo unajishushaga hata kama siyo kosa lako? au pande zote mbili kutokana na tatizo ndiyo mnajishusha?


  Nadhani kuna wengine wanaanza na vitendo halafu huko kama outing wanaongelea walipokosea na kuomba msamaha..Nimeshawahi kuwa na mpz ambae msamaha kwake wakati ambao amekosea ilikuwa ni ngumu..mpaka tuchuniane halafu anasema twende mahali na huko alikuwa akikiri alikosea na kuomba msamaha..
  Ila kuanza kusema 'sorry' muda aliokosea ilikuwa ngumu sana..


  Lizzy mamii kweli viporo vinakera sana, bora kumalizana yaishe..tatizo kubwa ni kukutana na mtu mwenye kiburi yani yeye akosee haombi msamaha wala kukiri kosa, sijui ni tabia hii au?

  Nimejifunza kitu hapo, amani inatafutwa haiji yenyewe mana utaachana na wangapi kwa kutokujishusha au kurekebishana mnapokosea.
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Ha ha BlackBerry, you're one in a million!!..nadhani linapokuja suala la kukumbushia, ni ngumu kwa binadamu kusahau kila kitu sema kuna wengine wamezidi kukumbushia yani badala ya kuishi maisha ya sasa kila siku mpo past tense.
   
 12. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kama mnamapenzi ya kweli sidhani kama hivo visasi vitakuwepo.
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri linapotokea tatizo wote mkajishusha,mkazungumza kisha mkajua nani mwenye tatizo halafu yakaisha kwa amani na furaha!
   
 14. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #14
  May 30, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Interesting eh.I usually think wanaume ndo wagumu kujishusha na kuwa kujishusha ni kwa wanawake tu!! Thanx Boss another day, another knowledge

  Ningeomba ufafanuzi kujishusha ndo kukoje? Kuna maanisha
  1. Uombe msamaha hata kama kosa si lako?
  2. Ukae kimya -usijibizane naye pale ambapo amepanda
  3. Kumjibu kwa upole ukijaribu kumwelewesha??

  1. Kuomba msamaha hata kama kosa si lako inawezakuwa njia nzuri ya kumaliza hacra zake kwa wakati huo. But hii inatakiwa iwe na follow-up plan yaani utafute siku mko vizuri uclear whatever mlichokuwa mnagombana (Hapa nitaambiwa una-bank makosa) Potelea mbali lakini ni vema mkawekana sawa kwani haichelewi kuwa kawaida - yaani akajua akifanya makosa utakiri wewe na kisha imetoka. Unamzoesha

  2. kukaa kimya pale anapopandisha - inategemea na mtu, mwingine anawezakukuchukulia una kiburi na dharau ndio maana umemgeuza radio- anaongea we unasikiliza. Mwingine anawezakukuelewa

  3. Kumjibu kwa upole- akiwa mwelewa atakusikiliza but kama kapandisha jazba sidhani kama itawork. But mwingine anawezakuona unamjibu kwa kuwa unajeuri.

  So nafikiri inategemea situation yenyewe but always ya kwanza (iwe na follow-up) husave more trouble
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  ngoja nije pm lol
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kibaya zaidi wanawake wengi mnagombana asubuhi

  mnayamaliza....

  Wewe unafikiri yameisha......

  Sasa pale jioni unapotaka game......ndo yanaaaanza upyaaaaaaaaaa....

  Talaka mnatafutaga wenyewe kwa kweli
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  mimi kama siko kwenye mood ya ugomvi
  hata kama sina kosa naomba msamaha....

  Tatizo wengine ukiomba msamaha unajipalia makaaa
   
 18. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Karibu The Boss
   
 19. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Looo mie sehemu hizo huwa sirembi, napiga mzigo kwanza nikimaliza kama kununa niendelee kununa
   
 20. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #20
  May 30, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Nimekusamehe lakini sitokusahau aliimba nani tena???

  Unaomba msamaha hata kama kosa si lako ndo solution mambo yaishe na maisha yaendelee mbele
   
Loading...