Kujikwaa kisiki mara mbili

Kujikwaa kisiki mara mbili

Mpaka hapa hujaona umuhimu wa kuwa na mediator kutoka nje ya Nchi!!

Walikosoa kwasababu Tume ilitakiwa iwe ya ''white paper'' , iende ikafanye utafiti na kuandaa terms of reference zake. Hii ya Chande ilipewa maelekezo 'bias' ndiyo maana iliweza kueleza kwa kina uharibifu na si vifo

Jaji Kisanga alipewa kazi kama hiyo, kwa kujali heshima yake akazungumza yaliyo nje yahadidu rejea. Mkapa alimtukana sana tena katika TV na Radio nchi zima ikisikia. Moja ya jambo aliloongea Jaji Kisanga ilikuwa suala la Muungano! Leo Muungano ni tatizo kubwa kuliko wakati analiongelea. Heshima ya Jaji Kisanga ipo na inazidi.

Hoja ni kwamba kwa International figure kama Jaji O Chande kupewa kitu na kukifanya kwasababu amepewa bila kujali heshima yake na masilahi ya nchi ilikuwa ni low point katika utumishi wake.

Labda kama atarudi tumboni na kuzaliwa upya! kwa huyu wa leo amepoteza credibility and integrity!
Naheshimu ni mtazamo wako, lakini mimi naamini katika matumizi ya taaluma yako hufuatana na kazi ulopewa sio kuingia usikotakiwa hata kama unashushwa daraja.

Utiifu una sifa zake unless kazi ulopewa utawadhalilisha unao wahudumia sii kujali nafasi yako wewe kuwa kipaumbele chako. Status quo hutuponza wengi katika majaribio ya taalima kazini.
 
Well basi naelewa tatizo liko wapi. Hata ningekuwa.mimi rais nisingekubali swala la ndani lijadiliwe mbele ya msuluhishi kutoka nje (kujishusha kiasi hicho) kama vile ni swala kubwa linalohusiana na Sheria za Kitaifa.

Kama unakorofishana na Mkeo na mkashindwa kusuluhisha ni vema mkaenda kwa wazazi kwanza badala ya kwenda kwa mtu wa nje muanze kuvuana nguo pale!

Hapana sidhani kama ni Ushauri mzuri. Hata iwe wazazi wa mkeo tena ndio inapendeza zaidi wajue ubaya wa mtoto wao! Hapo Chadema wakubali kuachia sii kila kitu watakubaliwa na CCM.

Matakwa ya Chadema ni ya Kisiasa na yanahusu mgongano wao Kisiasa, na tunajua mengi ni CCM kupitia matukio kadhaa ya Kisiasa ambayo yanatakiwa kurekebishwa kimfumo. Waweke masharti yanayowezekana.

..Mama anatakiwa awatose na kuwatoa kafara baadhi ya watu wake waliomuingiza ktk aibu na balaa la OCT 29.

..Kutaka kuwabebesha lawama Chadema haitasaidia kwasababu kila mtu anajua chama hicho hakina mamlaka ya kuamrisha vyombo vya dola.
 
Maridhiano ya kweli mara nyingi hukitoa chama tawala kwenye utawala CCM atakuwa mwathirika kwa maziingira ya sasa ya kisiasa ndiyo maana ni vigumu CCM kukubali maridhiano na katiba mpya ya kweli ikiakisi matakwa ya Chadema na wananchi wazalendo. Huko Afrika Kusini makaburu walianguka kwa maridhiano. CCM analijua hilo. Itakuwa vigumu ku forge a way forward. Muhimu kwa CCM ningeshauri ilegeze kwa baadhi ya mifumo kipindi cha Kikwete ilifanikiwa ingawa walihisi kuondolewa madarakani hivyo kubadilika na kuegemea kwenye dola kimfumo.
Tuwalazimishe kwa wingi wetu hawatushindi haka ka ccm ni kakikundi kadogo sana
 
Naheshimu ni mtazamo wako, lakini mimi naamini katika matumizi ya taaluma yako hufuatana na kazi ulopewa sio kuingia usikotakiwa hata kama unashushwa daraja.

Utiifu una sifa zake unless kazi ulopewa utawadhalilisha unao wahudumia sii kujali nafasi yako wewe kuwa kipaumbele chako. Status quo hutuponza wengi katika majaribio ya taalima kazini.

Mkuu kwanza nakusifu umeleta Mada pana yenye lengo kukuza uwelewa lkn pia kujaribu kuwavalisha mitazamo ya pande mbili tofauti

Dini ya kislam inasema mwanaume hasio na Mke basi mwanaume uyo anakosa sifa kadhaa za moja kwa moja sifa za kufungisha ndoa na ya pili kutatua changamoto za wawili walio kwenye ndoa!

Nini maana yake kama yeye hana mke ivyo hawezi jua changamoto za ndoa zipoje faida za ndoa zipoje!!!

Kwa mfano huu mzuri kiakili
Naweza sema Mkandara wewe umebeba sifa za mume mwenye mke ivyo unazo sifa zote kutatua changamoto mbali mbali!

Wafuasi wa Chadema siku zote hawataki kukubali kutatua changamoto lazima kwanza kukubaliana kuyavaa matukio ktk ukweli jinsi ulivyo !

Siku zote upande wenyekujiona wenyewe ndio umeonewa tu na wao ndio wenye haki kutoa mapendekezo kutatua matatizo mwisho wake sio mzuri !!!

watakuja kugombana wenyewe kwa wenyewe kwasababu mitazamo ya mambo inaenda kubadilika kila siku,

Siku Chadema wakija kukubali kukaa mezani na CCM wakikubali kwamba nawao nisehemu ya tatizo
Ndipo Suluhu ya kweli itapatikana
Kinyume cha ivyo

Narudia CHADEMA watakuja kugombana wenyewe kwa wenyewe yani Suluhu sasa itatokea kupitia minyukano yao wenyewe kwa wenyewe !!

Mambo muhimu Chadema hawataki kukubali japo yapo wazi kwa Watanzania wote!!

Uchochezi kuzuiya Uchaguzi ndio chanzo cha kutokea mo29

Nakumbusha pale Kenya kulitokea majanga ya ktk Uchaguzi kipindi cha Rais ni MWAI KIBAKI anagombea muhula wa pili
Kukatokea maafa makubwa watu
1000+ wakafa ICC wakaja mbio
JE swali kakamatwa nani kwenye kadhia ya ile??????
ICC waliwabeba wapinzani kwa mashtaka ya Uchochezi
Katakiwa kwenda kujibu mashtaka ni Uhuru Kenyata William Rutto na Martha karua
Wote ni Wapinzani

Ktk Serikali ya Kibaki hakuna kiongozi yoyote kashutumiwa
Sababu wenyewe walikuwa ktk Kurejesha Amani ya Wakenya,

Sasa Chadema kuvaa nguo za Uchochezi hawataki lkn mshangao wanakiri kuzuiya Uchaguzi kuvamia vituo vya Uchaguzi !

Sisemi CCM ni watakatifu lkn kukubali tatizo ni njia nzuri ya kutatua changamoto zetu

Serikali ya CCM limetangaza maridhiano pasi na kutafuta nani mtakatifu nani Shetani
Muhimu ni maridhiano tusonge mbele Watanzania tushajikwaa tayari Muhimu kuendelea mbele tu.
Mana kivyovyote lazima tusonge mbele tu!

Chadema wajifunze kupitia chama cha CUF
CUF walikuwa kama Chadema yasasa walikuwa Wasusuji kama Chadema yasasa!!!

lkn maridhiano yanajenga Safari yenye matumaini
Pasipo na Chadema CUF hakuna maana Tanzania itasimama Safari yake ,

Tusijione wenye umuhimu sana zaidi ya maslahi mapana ya kitaifa,,
 
Nimewahi kumsikia Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisema Chadema haiwezi kwenda katika Maridhiano pasipo Kiongozi wao TAL kuachiwa huru bila masharti.

Na kuna baadhi ya.Wanachama wanakataa kabisa maridhaliano ya Serikali pasipo Uwajibikaji wa Serikali kufuatia matukio kadhaa yalowahi tokea, ilihali Serikali nayo inadai Chadema wamekuwa wakitumia wanaharakati na taasisi za nje kuvuruga Amani nchini. Msema kweli nani hata sielewi..

Sasa, katika tafakari zangu nimejikuta najiuliza maswali kadhaa kulingana mazingira ya hoja hii ya Heche na baadhi ya watu kwa sababu zifuatazo

Waingereza husema "Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me” na ingine yasema. " Once bitten, twice Shy" ni katika Maudhui hayo hayo nayotaka kuyajadili.

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu akiwa matibabu kule Ubelgiji alikutana na rais Samia wakakubaliana kufanya mazungumzo kulenga maridhiano baina ya Utawala wake na Chadema kwa masharti ambayo Tundu Lissu yaliyainisha ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi Mwenyekiti wa Chadema wakati huo Nd. Freeman Mbowe pamoja na masharti mengineyo sitoyataja yote.

Mbowe aliachiwa huru, wakaanza mchakato na vikao vya Maridhiano ambayo kufikia hatua za mwisho mwisho l, Chadema walijitoa kwa madai ya kwamba Rais Samia akikataa kuweka makubaliano yao katika maandishi na kuyasaini. Tunaambiwa Chadema Hawakutaka maridhainao ya maneno matupu pasipo Maandishi.

Kufuatia matokeo yale najiuliza maswali yafuatayo.

  • Je, Chadema wanaweza kukubali kuingia katika maridhiano na rais ambaye alikataa kusaini makubaliano ya awali iweje leo atakuwa mkweli?
  • Je, rais Samia anaweza kubali maridhiano na Chadema ambao anajua yawezekana ni mtegilo kama ule wa awali walojitoa katika maridhiano yale kwa sababu ambazo Yeye na majumbe wake waliona hazina msingi?
Waswahili husema mnafiki ana ishara tatu..

Maasalaam
Ni lini Tundu Lissu akiwa amelazwa Ubelgiji alikutana na "rais Samia"!!?!
 
Unajua mnapojibu hoja upande mmoja tu, mimi naweka walakini juu yake. Sasa ili mjadala uwe mpana zaidi, vema tusiegemee upande mmoja. Nilitegemea japo mtu mmoja aje na msimamo wa Serikali nae nimuulize lakini nashangaa kila anayeandika ni kuhusu kuitetea Chadema.
Haipendezi ionekane tunabishana juu ya hili bali tujadili kwa kutazama mawazo ya pande zote mbili ndio Ukweli utajitenga.

Anyway sitochoka kuhoji msimamo wa Chadema maana siuelewi mpaka leo hii. Na nakumbuka vema Chadema walipokataa kuendelea na Maridhiano yale walisema Mbowe kalamba Asali hawataki tena kuendelea na Maridhiano na rais Samia.

Alotaka Maridhiano ya Kitaifa kabla ya Uchaguzi Mkuu alikuwa Polepole na alisema wazi tusikubali Maridhiano baada ya Uchaguzi, sikuwahi wasikia Chadema wakisema watarudi mezani kuendelea na maridhiano. Sijawahi niseme kweli yangu najua walikataa kabisa kuendelea na maridhiano.

Na nadhani msimamo huu wa kukataa kuendelea na maridhiano na Samia ndio ilikuwa SABABU kubwa ilomwangusha Mbowe kwenye Uchaguzi Mkuu wakisema walimwambia watoke yeye bado alikuwa anakazania waendelee..

Sikumbuki kabisa wakati wowote wa Tundu Lissu akiwa Mwenyekiti wa Chama toka January 30, 2025 hadi April 09, 2025 siku Tundu Lissu anakamatwa, Chadema walikuwa wapo tayari kurudi mezani na Serikali au Samia.

Isitoshe Wananchi hawajui ama hatujui katika Makubaliano yale walikubaliana nini, marekebisho gani yalifanyika kulingana na makubaliano na yapi yalikwamisha makubaliano yale zaidi ya Wananchi kusikia Viongozi pande zote mbuli wakilaumiana.

Itapendeza zaidi kama Tungesikia pia Upande wa Serikali wao walikataa nini na kwa nini rais anayetamba kwa 4R akatae kuridhia makubaliano kwa maandishi?

Ndio maana nimekuja na hoja hii kwetu sisi tuchambue nani mwenye kusema ama kuficha UKWELI.
Interesting.

Unahitaji balance kati ya taarifa/hoja za CHADEMA na serikali. Sawa.

CHADEMA "huwaelewi" lakini una maelezo kibao kuhusu chama hicho. Sawa.

Unatarajia nani atueleze kuhusu msimamo wa serikali. Wadau (wahusika) serikalini au mashabiki wa serikali walioko JF?

Una hakika wewe hauujui msimamo wa serikali ambao kwako yaelekea unakubalika?

Tupe hiyo balance, tafadhali, ili na sisi tuweke misimamo yetu.
 
Safi kabisa lakini hoja yangu toka mwanzo ilikuwa ya Kufikirika nikihoji kuwa - Masharti kama haya yalikuwepo hata katika maridhiano ya kwanza aloyaomba Tundu Lissu. Matokeo yake hawakufikia makubaliano ikaisha vibaya sana!

Hoja yangu inaanzia hapa -
1. Chadema wanarudisha madai kwa masharti yale yale ya kwanza (wakati wa Mbowe) Je, inawezakanaje Chadema wakaamini safari hii Samia atabadilika?

2. Kama upande wa Samia waliona Chadema ndio hawakutaka kuendelea na maridhiano kwa sababu zao. Je, Inawezekanaje Samia akubali kurudi meza ya maridhiano na Chadema akijua Maombi kama haya yaliwahi kufanywa na Tundu Lissu, akawaachia wafungwa na mengineyo lakini mwisho wa Siku Chadema Wakajitoa baada ya yeye kutimiza masharti yao.

Mimi naelewa nilichosoma ya kwamba Samia alikataa kuweka Makubaliano yao katika maandishi na kusaini lakini sielewi upande Samia kwa nini hawakusaini au kuna madai au sababu nyinginezo.

Kati yao nani atakubali Kujikwaa Kisiki mara mbili?
Hapo kuna mambo mapya ambayo hayakuwemo kwenye maombi ya Lissu alivyokutana na Samia Belgium. Moja ni hilo la Mediator. Utapeli wa yale mazungumzo ya kwanza umewapa maarifa Chadema ku demand an independent Mediator.
 
CCM na Serikali yake ni wazoefu wa migogoro kwao washapambana na vyama vyengine kwenye migogoro tofauti tofauti mfano mgogoro wa NCCR wakaja CUF
Nasasa Chadema

Ndiomana CCM wakaja halaka na neno Maridhiano wanajua njia pekee ya kutatua changamoto yasasa ni Maridhiano tu

Kununua hakuna maana yoyote kutomtambua Rais chama kimoja Chadema hakuna maana yoyote wkt Rais anatambuliwa kimataifa

Njia yenye unyenyekevu ni kuongea kutatua moja mbili 3 maisha yaendelee
Kususia Uchaguzi walianza CUF kugomea kumtambua Rais walianza CUF
Walivuna nini kitaifa au kimataifa ¿¿¿¿¿¿¿¿¿

Chadema wanarudia Siasa zile zile za chama cha CUF ya miaka ya 2005-2010
Hakuna changamoto ya kitaifa inaenda kutatuliwa kwa kususa susa
Wkt Chadema ni taasisi ya kisiasa¿¿¿¿¿
 
Kusema kwanza lazima yafanyike yale na yale ni ujuha ufinyu wa busara Kukosa utimamu wa kujua majukumu yako kama kiongozi wa kisiasa

SWALI ............... ??
kwa wenye akili
Ukisema lazima kwanza kufanyike yale na yale

Kumbe malalamiko yako yashatatuliwa sasa mnakutana kufanya Maridhiano au mazungumzo ya nini tena na kumbe matakwayenu yametimizwa
nje ya mazungumzo !!!!!!!!

Kazi kipimo cha utu 🙄 🙄
 
Nimewahi kumsikia Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisema Chadema haiwezi kwenda katika Maridhiano pasipo Kiongozi wao TAL kuachiwa huru bila masharti.

Na kuna baadhi ya.Wanachama wanakataa kabisa maridhaliano ya Serikali pasipo Uwajibikaji wa Serikali kufuatia matukio kadhaa yalowahi tokea, ilihali Serikali nayo inadai Chadema wamekuwa wakitumia wanaharakati na taasisi za nje kuvuruga Amani nchini. Msema kweli nani hata sielewi..

Sasa, katika tafakari zangu nimejikuta najiuliza maswali kadhaa kulingana mazingira ya hoja hii ya Heche na baadhi ya watu kwa sababu zifuatazo

Waingereza husema "Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me” na ingine yasema. " Once bitten, twice Shy" ni katika Maudhui hayo hayo nayotaka kuyajadili.

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu akiwa matibabu kule Ubelgiji alikutana na rais Samia wakakubaliana kufanya mazungumzo kulenga maridhiano baina ya Utawala wake na Chadema kwa masharti ambayo Tundu Lissu yaliyainisha ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi Mwenyekiti wa Chadema wakati huo Nd. Freeman Mbowe pamoja na masharti mengineyo sitoyataja yote.

Mbowe aliachiwa huru, wakaanza mchakato na vikao vya Maridhiano ambayo kufikia hatua za mwisho mwisho l, Chadema walijitoa kwa madai ya kwamba Rais Samia akikataa kuweka makubaliano yao katika maandishi na kuyasaini. Tunaambiwa Chadema Hawakutaka maridhainao ya maneno matupu pasipo Maandishi.

Kufuatia matokeo yale najiuliza maswali yafuatayo.

  • Je, Chadema wanaweza kukubali kuingia katika maridhiano na rais ambaye alikataa kusaini makubaliano ya awali iweje leo atakuwa mkweli?
  • Je, rais Samia anaweza kubali maridhiano na Chadema ambao anajua yawezekana ni mtegilo kama ule wa awali walojitoa katika maridhiano yale kwa sababu ambazo Yeye na majumbe wake waliona hazina msingi?
Waswahili husema mnafiki ana ishara tatu..

Maasalaam
Huyu naye aache ujinga wa kuweka masharti yasiyotekelezeka!
 
Hapo kuna mambo mapya ambayo hayakuwemo kwenye maombi ya Lissu alivyokutana na Samia Belgium. Moja ni hilo la Mediator. Utapeli wa yale mazungumzo ya kwanza umewapa maarifa Chadema ku demand an independent Mediator.

Kama kutapeliwa kufikia mwisho wa mazungumzo ya maridhiano ya kipindi kile basi Serikali ndio imetapeliwa na Chadema!!!!!

Mana kupitia maridhiano yale Kiongozi wake
mzee mbowe katoka Lupango lengo kuja kushiriki
maridhiano !!!!

JE
baada ya Kiongozi wao kuwa nje Chadema si tunajua wameyakimbia maridhiano yenyewe !!!

Wkt Serikali hawawezi tena kumrudisha Lupango Mzee mbowe ¿¿😄 😄 😄

Nasasa mbinu zilezile za kitapeli Chadema wamezitumia kipindi kile wanataka kuzitumia upya kwa Rais yule yule
wamemtapeli mwanzo 🙄 🙄

kwsasa hakuna mtu kutoka Lupango kwanza maridhiano shubamit!!
 
Msingi wa neno kutapeliwa ni mmoja wapo kupoteza kitu

Mazungumzo ya kipindi kile Serikali wamempoteza mzee mbowe kuwa Lupango !!!!!!

Tuje Chadema wamepoteza nini kipindi kile ???????????
 
Mkuu, serikali ilisema kuna vijana kutoka nchi jirani walishiriki Oct29. Hadi leo hakuna raia wa nje aliyeshtakiwa
Unatafuta ukweli upi?

Ndio moja ya sharti lao , kwamba, awepo mediator. Sharti hili linafuatia matokeo ya vikao vilivyoisha bila kujua nini walijadili kwasababu CCM haikutaka kuweka katika maandishi. Hoja ya CHADEMA ni kama yako '' once bitten, twice shy''. Kinachoshangaza, ikiwa CCM wanataka maridhiano ili Taifa lipone kwanini wanaogopa mediator?

Hili ni swali Watanzania wanapaswa kujiuliza, kwanini CCM hawataki mediator ikiwa sote tunataka suluhu
Kwani mediator anawaathiri vipi na kuna sababu gani za kumkataa!

Kuna ugumu gani kuwa na mediator
huyo mediator wanaemtaja chadema obvious ni mtu wao,let say ni Amsterndam au jamaa zake,akishamaliza ku mediate,repirt atampa nani kwa utekekezaji?,au atampa heche?🤔
 
Msingi wa neno kutapeliwa ni mmoja wapo kupoteza kitu

Mazungumzo ya kipindi kile Serikali wamempoteza mzee mbowe kuwa Lupango !!!!!!

Tuje Chadema wamepoteza nini kipindi kile ???????????
chadema wao walitaka kila jambo lao likubaliwe,shida ndo ilianzia hapo,,chadema ni extremists,hawa watu huwezi kuridhiana nao,maana wào siku zote wanataka mambo yao yapite yote,kuridhiana na chadema ni kupoteza mda tu,,kwa maoni yangu tuendelee na statu quo,katiba ifanyiwe marekekebisho sehemu muhimu,maisha yaendelee,,endapo chadema wataamua kuunga tela,sawa,wakisusa,sawa,wakiingia msituni nayo sawa tu,hatuwezi kuwa tunabembeleza mijitu mizima miaka nenda rudi
 
Nia njema ya mtu inapimwa hata kwa kuangaliwa sura ila jamaa zetu wa mbogamboga wao maridhiano yamejikita kwny kukifanya chadema kama ngazi hasa kwny maovyo ovyo yao ya oct 29
 
Mkandara,

..labda ungetupa muongozo ni Serikali inapaswa kurekebisha wapi, vilevile Chdema, ili mazungumzo yasonge mbele na tufikie ktk maridhiano.
 
Interesting.

Unahitaji balance kati ya taarifa/hoja za CHADEMA na serikali. Sawa.

CHADEMA "huwaelewi" lakini una maelezo kibao kuhusu chama hicho. Sawa.

Unatarajia nani atueleze kuhusu msimamo wa serikali. Wadau (wahusika) serikalini au mashabiki wa serikali walioko JF?

Una hakika wewe hauujui msimamo wa serikali ambao kwako yaelekea unakubalika?

Tupe hiyo balance, tafadhali, ili na sisi tuweke misimamo yetu.
Nashukuru umeniuliza swali na niseme wazi ya kwamba nimesema Chadema siwaelewi kutokana na maelezo ya yao wenyewe wanajichanganya sana kuhusu Maridhiano yao yatahusu nini? Na Upane wa Serikali sijui wanataka nini. Nakiri kabisa sijui Undani wa Maridhano.

Kuna mjadala nilipitia siku za mwanzi narudi JF nikasema Chadema wanataka Maridhiano kwa masharti kadhaa, nikimnukuu Heche, nikaja sahihishwa ya kwamba nani alonambia Chadema wanataka Maridhaino ya CCM.?

Nikasema nimemsikia Heche akisema wataingia Maridhianono ikiwa Tundu Lissu ataachiwa bila masharti (hii ni wakati kesi bado ipo Mahakamani) wakasema Chadema haiwezi kurudi mezani na Kiongozi aliyeua watu Oct. 29 mpaka awajibike.

Na kulikuwa na Ushindani baina yao wanaotaka Maridhiano na wengine hawataki kama maneno ya Polepole alosema Maridhiano baada ya Uchaguzi ni kuwakosea Wananchi.

Na kweli yalotokea ni exactly kama Polepole alivyotabiri au alivyosema kuhusiana na matokeo ya Uchaguzi.

Sasa naposikia Serikali inataka Maridhiano baada yq Uchaguzi ndio nashindwa kuelewa tunaridhiana kwa kitu nini? Je, Serikali inataka kuridhiana na nani na kwa tatizo gani?

Katika hili nilianzisha mada siku za nyuma kidogo, hakuna alojitokeza kutueleza upande wa Serikali haya maridhiano ni ya nini. So far, kweli sifahamu Serikali inataka nini mpaka leo hii kuitisha Maridhiano. Je ni kutokana na matakwa.ya baadhi Wazee, Wachungaji, Masheikh, Mawakili au ni matakwa yao wenyewe kama alivyosema Polepole?

Upande wa Chadema sasa umekuwa wazi zaidi kama nilivyosema mimi toka mwanzo Chadema Wataka kuingia kwenye Maridhiano mapya lakini kwanza masharti yao yatimizwe ikiwa ni pamoja na Tundu Lissu aachiwe.

Mpaka hapo nilikuwa sawa, walonipinga wamegeuka sasa nao wanasema Chadema ipo tayari kwa maridhiano toka zamani ikiwa masharti yao yatatimizwa ni pamoja na Mediator kutoka nje. Hili sikuligusia mwanzo kwa sababu halikuwa mjadala wa awali ulokataa Maridhiano.

Na maadam sasa hivi tunazungumza lugha moja na kwa Uwazi zaidi ndio nimesema sharti hili la msuluhishi kutoka nje sidhani kama ni wazo zuri, hata mimi ningekuwa rais nisingelikubali kwa sababi Samia kafanya makosa mengi ambayo UE na washirika wake wapo Upande wa Chadema. Isitoshe mambo yetu ya Ndani hayahitaji msuluhishi kutoka nje, ni kuvuana nguo hadharani.

Bado huamini ya kwamba naelewa madai ya Chadema lakini sielewi madai ya Serikali? Nimalizie kusema, nimewahi msikia Mzee Wasira akisema CCM hawahitaji kufanya Maridhiano na Chadema, akawashusha hata umuhimu wao ndio narudi kuuliza, hivi sasa Serikali inataka Maridhiano ya kitu gani na akina nani?

Maridhiano ya mwanzo yalikuwa ya CCM na Chadema hayakuvihusu vyama vingine wala Wananchi kwa sababu masharti na mambo yalozungumzwa sisi Wananchi hawaufahamu. Yalikuwa maridhiano ya faragha baina ya viongozi wa CCM na Chadema.

Ila sasa hivi, Serikali na sio CCM wanapotaka Maridhiano na Kitaifa ndio najiuliza Maridhiano ya kitu gani? Je, ni kuhusu Katiba Mpya, Demokrasia, Mauaji ya Oct 29, Utekaji ama kitu gani? Na Chadema watashiriki Maridhiano haya au yale yanaowahusu wao na CCM! Hili limeongezeka katika hoja za washirika humu ndani japo mimi nilitaka kujadili hayo Maridhiano ya CCM na Chadema.

Nadhani nimejieleza vya kutosha, gazeti ni refu sana ntawachosha..
 
Unajua umesema kweli kabisa kwamba Sijui Chadema wanataka nini. Kama wewe unajua tafadhali nambie maana hata hao CCM sijui wanataka nini ila najua mmoja wao ni Mnafiki na ishara za mnafiki ni 3.

1. Kusema uongo: Huongea uongo anapozungumza.
2. Kutotimiza ahadi: Huvunja au hatekelezi ahadi anapotoa.
3. Kufanya khiyana: Hukosa uaminifu au hufanya khiyana anapoaminiwa.
Neutral Referee.
CCM wanamtaka au hawamtaki?
 
Ccm hawakuchaguliwa bali walitangazwa na tume yao wameshinda
Mkuu Radiriki, rodrick alexander , hivyo ndivyo katiba yetu inavyosema, tume ikiisha tangaza mshindi wa urais, tangazo hilo ni final and conclusive, hata kama amepatikana kwa ushindi batili, bao la mkono, uchaguzi usio huru na wa haki, tangazo hilo linatumia kanuni ya the end justify the means kwa kuhalalisha chochote kilichofanyika!.

P
 
Back
Top Bottom