Kujikwaa kisiki mara mbili

Kujikwaa kisiki mara mbili

Chadema walitaka maridhiano kabla ya uchaguzi, wapo waliopendekeza hata uchaguzi usogezwe mbele Ili maridhiano muhimu yafanyike kwanza.

Ila yote hayo yalikataliwa na wenye mamlaka.
kitu cha kwanza alíchofanya lisu aliporudi toka uhamishoni baada ya Rais kutaka maridhiano,ni lisu kuyakataa,akisema ni mapendano,akadai mbowe karamba asali,chadema wakasubiri wiki chache kabla ya uchaguzi,ndo wakaanza kudai maridhiano,eti uchaguzi uahirishwe kwanza yaganyike maridhiano...sasa hicho kilikua kisiki cha kwanza,kisiki cha pili,chadema sasa hawataki maridhiano,watasubiri mpaka uchaguzi wa 2029 ukaribie,kisha ndo wadai maridhiano,uchaguzi usogezwe mbere😂😂,HICHO NI KISIKI CHA PILI,WATAJIKWAA,maana uchaguzi hautaajirishwa kamwe,na chàdema watasusa tena
 
Na kuna baadhi ya.Wanachama wanakataa kabisa maridhaliano ya Serikali pasipo Uwajibikaji wa Serikali kufuatia matukio kadhaa yalowahi tokea, ilihali Serikali nayo inadai Chadema wamekuwa wakitumia wanaharakati na taasisi za nje kuvuruga Amani nchini. Msema kweli nani hata sielewi..
Mkuu, serikali ilisema kuna vijana kutoka nchi jirani walishiriki Oct29. Hadi leo hakuna raia wa nje aliyeshtakiwa
Unatafuta ukweli upi?
Waingereza husema "Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me” na ingine yasema. " Once bitten, twice Shy" ni katika Maudhui hayo hayo nayotaka kuyajadili.

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu akiwa matibabu kule Ubelgiji alikutana na rais Samia wakakubaliana kufanya mazungumzo kulenga maridhiano baina ya Utawala wake na Chadema kwa masharti ambayo Tundu Lissu yaliyainisha ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi Mwenyekiti wa Chadema wakati huo Nd. Freeman Mbowe pamoja na masharti mengineyo sitoyataja yote.

Mbowe aliachiwa huru, wakaanza mchakato na vikao vya Maridhiano ambayo kufikia hatua za mwisho mwisho l, Chadema walijitoa kwa madai ya kwamba Rais Samia akikataa kuweka makubaliano yao katika maandishi na kuyasaini. Tunaambiwa Chadema Hawakutaka maridhainao ya maneno matupu pasipo Maandishi.

Kufuatia matokeo yale najiuliza maswali yafuatayo.
  • Je, Chadema wanaweza kukubali kuingia katika maridhiano na rais ambaye alikataa kusaini makubaliano ya awali iweje leo atakuwa mkweli?
Ndio moja ya sharti lao , kwamba, awepo mediator. Sharti hili linafuatia matokeo ya vikao vilivyoisha bila kujua nini walijadili kwasababu CCM haikutaka kuweka katika maandishi. Hoja ya CHADEMA ni kama yako '' once bitten, twice shy''. Kinachoshangaza, ikiwa CCM wanataka maridhiano ili Taifa lipone kwanini wanaogopa mediator?

Hili ni swali Watanzania wanapaswa kujiuliza, kwanini CCM hawataki mediator ikiwa sote tunataka suluhu
Kwani mediator anawaathiri vipi na kuna sababu gani za kumkataa!
  • Je, rais Samia anaweza kubali maridhiano na Chadema ambao anajua yawezekana ni mtegilo kama ule wa awali walojitoa katika maridhiano yale kwa sababu ambazo Yeye na majumbe wake waliona hazina msingi?
Waswahili husema mnafiki ana ishara tatu..
Kuna ugumu gani kuwa na mediator
 
Maazimio ya Chadema kuhusu maridhiano ni haya hapa:
Masharti na madai ya CHADEMA

1. Kuachiliwa huru kwa Tundu Lissu – Mwenyekiti wa CHADEMA aachiwe huru kabla ya kuanza mazungumzo ya maridhiano.

2. Kuachiliwa kwa watu waliotekwa na kupotezwa – Serikali ichukue hatua kuhusu watu waliotekwa, kupotezwa na wale wanaoshikiliwa kwa sababu za kisiasa.

3. Kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi – Matukio ya mauaji, vifo na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 yachunguzwe kwa uhuru na bila upendeleo.

4. Uwajibikaji wa waliohusika – Wale watakaobainika kuhusika na mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu wawajibishwe kisheria.

5. Mpatanishi huru – mazungumzo yaongozwe na mpatanishi anayeaminika na pande zote mbili, badala ya Serikali kuwa upande mmoja wa mazungumzo na pia msimamizi wake.

6. Kukubali kwamba kuna mgogoro wa kisiasa – Serikali na vyama vya upinzani zikubali kuwepo kwa matatizo ya kisiasa yanayohitaji kutatuliwa badala ya kujifanya kuwa kila kitu kiko sawa.

7. Katiba mpya na mageuzi ya kidemokrasia – Kuwepo kwa mchakato wa kweli wa kupata Katiba mpya na kuboresha mfumo wa uchaguzi, uhuru wa mahakama na demokrasia.

8. Uhuru wa vyama vya siasa – CHADEMA na vyama vingine viruhusiwe kufanya shughuli zao za kisiasa bila vitisho, ukandamizaji au kukamatwa kiholela.
Safi kabisa lakini hoja yangu toka mwanzo ilikuwa ya Kufikirika nikihoji kuwa - Masharti kama haya yalikuwepo hata katika maridhiano ya kwanza aloyaomba Tundu Lissu. Matokeo yake hawakufikia makubaliano ikaisha vibaya sana!

Hoja yangu inaanzia hapa -
1. Chadema wanarudisha madai kwa masharti yale yale ya kwanza (wakati wa Mbowe) Je, inawezakanaje Chadema wakaamini safari hii Samia atabadilika?

2. Kama upande wa Samia waliona Chadema ndio hawakutaka kuendelea na maridhiano kwa sababu zao. Je, Inawezekanaje Samia akubali kurudi meza ya maridhiano na Chadema akijua Maombi kama haya yaliwahi kufanywa na Tundu Lissu, akawaachia wafungwa na mengineyo lakini mwisho wa Siku Chadema Wakajitoa baada ya yeye kutimiza masharti yao.

Mimi naelewa nilichosoma ya kwamba Samia alikataa kuweka Makubaliano yao katika maandishi na kusaini lakini sielewi upande Samia kwa nini hawakusaini au kuna madai au sababu nyinginezo.

Kati yao nani atakubali Kujikwaa Kisiki mara mbili?
 
Mkuu, serikali ilisema kuna vijana kutoka nchi jirani walishiriki Oct29. Hadi leo hakuna raia wa nje aliyeshtakiwa
Unatafuta ukweli upi?

Ndio moja ya sharti lao , kwamba, awepo mediator. Sharti hili linafuatia matokeo ya vikao vilivyoisha bila kujua nini walijadili kwasababu CCM haikutaka kuweka katika maandishi. Hoja ya CHADEMA ni kama yako '' once bitten, twice shy''. Kinachoshangaza, ikiwa CCM wanataka maridhiano ili Taifa lipone kwanini wanaogopa mediator?

Hili ni swali Watanzania wanapaswa kujiuliza, kwanini CCM hawataki mediator ikiwa sote tunataka suluhu
Kwani mediator anawaathiri vipi na kuna sababu gani za kumkataa!

Kuna ugumu gani kuwa na modearator!
Mimi nazungumzia Maridhiano ya CCM na Chadema na nadhani yalikuwepo kabla hata ya Mauaji ya Oct 29. Ukichanganya mauaji ya Oct 29 upande wa Madai ya Chadema, trust me CCM watasema Chadema ndio chanzo cha yalotokea Oct 29. Huu utakuwa mchezo wa Paka na Panya.
Sijui unanielewa?

Hilo la "Once bitten, twice Shy" Yawezekana hata Samia anaona vile vile alidanganywa na Lissu, akawapa kila kitu walichotaka Kichama, lkn ilipofikia wakubali matakwa ya CCM au Serikali yake, Chadema wakajitoa! Tunamsikia sana yule mzee wetu Wasira nae akijichanganya! Nani atakubali kujikwaa kisiki mara mbili?

Sisi tulioko nje ya ulingo huo hatufahamu Ukweli hasa ni upi? Na pengine wewe mwenzangu unaujua lakini kwangu haitoshi. Mimi sii mtu wa kuambiwa nikaamini, huchanganya na zangu.
 
Yani Tanganyika imefikia hatua ngumu sana.

Inaongizwa na Fairule
watu Wapumbavu pumbavu
Wajinga jinga
Waingo.
Wezi.
Matapeli.
Mafisadi.
Wahuni hadi kwenye Ndoa.
Mke wa pili.
Ameachika
Nk
Matusi ya nini? Hapa tunajadili hoja mkuu wangu. Unadhani kutukana ndio itabadilisha hulka zao ama basi Unatutukana Watanzania wote ambao tumekubali kuongozwa na watu kama hao ikiwa ni pamoja na wewe mwenyewe, wazazi ndugu zako na n.k. wakati mwingine epuka kunyooshea watu kidole, huwa kuna vidole vitatu vinakunyooshea wewe..
 
..Chadema pia wamesema wanataka maridhiano yasimamiwe na msuluhishi toka nje, asiye na upande, ili udanganyifu uliotokea ktk mazungumzo ya awali usijirudie.

..Wapambe wa Ccm hawataki kusikia hoja ya maridhiano kuhusisha msuluhishi toka nje wakidai huko ni kuingiliwa ktk mambo yetu ya ndani.

..Kwa maoni yangu, hoja hiyo haina nguvu kwasababu hata ktk Tume ya Uchunguzi inayoongozwa na Jaji Lila kuna wajumbe toka nje ya nchi.
Hilo la Msuluhisho kutoka nje katika Swala la Kisiasa, sidhani kama ni sharti la maana kwa nchi Huru kama Tanzania. Inaonekana kama Chadema haiamini mtu yeyote aliye ndani ya Tanzania ana uwezo wa kufikiri ama kuamua bila kuwa na Upande. Gharama zake atalipa nani?

Na ubaya zaidi CCM wakikataa hawakuhusika na mshauri tote hayo, huyo msulihisho hajui Ukweli ni upi, hata tukisema mfano Ben Saanane hamjui! Serikali inaweza kana kila kitu na kikao kikaishia hapo. Maiaji na Utekani nadhani haya ni maswala ya Kimahakama, mkoyaweka.kwenye maridhiano hakuna kitakacho patikana. Trust me..

Mimi nadhani kama atahitajika msuluhishi basi iwe mzee anayeaminika mathlan Mzee Warioba au Prof. Shivji ambao wameonesha nia ya dhati kabisa na wana Elimu na Uwezo mkubwa wa kufikiri.
 
..Chadema wanaogopa " kukwaa kisiki mara mbili, " ndio maana wanataka mazungumzp yawe chini ya Msuluhishi wa nje.

..Uzoefu wa Chadema wakati wa mazungumzo yao na Ccm ndio umepelekea wao kuomba mazungumzo yasimamiwe na mtu toka

..Kuitwa kwa Msuluhishi toka nje hakumaanishi kwamba Watanzania hatuna uwezo wa kufikiri, au hakuna Mtanzania mwenye uwezo huo.

..Kwa maoni yangu, pendekezo hilo linaashiria kiwango cha kutokuaminiana kati ya Chadema na Ccm. Vilevile ombi hilo linaashiria ukubwa wa tatizo tulilonalo, kwamba nchi yetu imekuwa kama ukoo uliokosa watu wazima wa kusimamia mambo yao.

..Kama kweli tuna nia njema na tunataka maridhiano ya kweli basi hatuna budi kuliweka suala letu chini ya usimamizi wa Jumuiya ya kimataifa na Msuluhishi anayekubalika na kila upande.
 
..Chadema pia wamesema wanataka maridhiano yasimamiwe na msuluhishi toka nje, asiye na upande, ili udanganyifu uliotokea ktk mazungumzo ya awali usijirudi
Kanuni za asili ''natural justice'' zinakubaliana na CHADEMA.
Haiwezekani Serikali ya CCM inayotuhumiwa ikawa msuluhishi au kuongoza usuluhishi.
..Wapambe wa Ccm hawataki kusikia hoja ya maridhiano kuhusisha msuluhishi toka nje wakidai huko ni kuingiliwa ktk mambo yetu ya ndani.

..Kwa maoni yangu, hoja hiyo haina nguvu kwasababu hata ktk Tume ya Uchunguzi inayoongozwa na Jaji Lila kuna wajumbe toka nje ya nchi.
Hoja haina mantiki kwasababu tuliwahi kumwalika msuluhishi wa Commonwealth kule Zanzibar

Tanzania ilikwenda Kenya kupata suluhu. Arusha ni kitovu cha usuluhishi iwe kwa Burundi, Rwanda , DRC au Sudan. Mugabe na Nkhomo walisuluhishwa Dar. Sisi tuna ''immunity' gani hatuwezi kutafuta mediator

Kama livyosema,. hiyo Tume yao ya Lila ina watu wa nje, nini wanakwepa kualika msuluhishi?

Kuna nadharia nyingi katika kukataa kwao'
Kwanza, wanahisi yapo mengi yanayowahusu yanayohitaji Uwajibikaji, Oct29
Pili, wanataka control ya '' narratives'' ili waweze kuwafunga wapinzani kwa kutumia vyombo vyao
Tatu, wanataka kuficha taarifa kama Taarifa ya Jaji Chande

Ikiwa wanataka suluhu, kwanini wasifanye haya;
Kwanza , waeleze ni maridhiano yanayohusu nini, kwanini, kati ya nani na nani, wapi na lini
Pili, wakubali awepo msuluhishi atakayekubaliwa na pande zote ili Taarifa iaminike kwa Umma
 
..Chadema wanaogopa " kukwaa kisiki mara mbili, " ndio maana wanataka mazungumzp yawe chini ya Msuluhishi wa nje.

..Uzoefu wa Chadema wakati wa mazungumzo yao na Ccm ndio umepelekea wao kuomba mazungumzo yasimamiwe na mtu toka

..Kuitwa kwa Msuluhishi toka nje hakumaanishi kwamba Watanzania hatuna uwezo wa kufikiri, au hakuna Mtanzania mwenye uwezo huo.

..Kwa maoni yangu, pendekezo hilo linaashiria kiwango cha kutokuaminiana kati ya Chadema na Ccm. Vilevile ombi hilo linaashiria ukubwa wa tatizo tulilonalo, kwamba nchi yetu imekuwa kama ukoo uliokosa watu wazima wa kusimamia mambo yao.

..Kama kweli tuna nia njema na tunataka maridhiano ya kweli basi hatuna budi kuliweka suala letu chini ya usimamizi wa Jumuiya ya kimataifa na Msuluhishi anayekubalika na kila upande.
Well basi naelewa tatizo liko wapi. Hata ningekuwa.mimi rais nisingekubali swala la ndani lijadiliwe mbele ya msuluhishi kutoka nje (kujishusha kiasi hicho) kama vile ni swala kubwa linalohusiana na Sheria za Kitaifa.

Kama unakorofishana na Mkeo na mkashindwa kusuluhisha ni vema mkaenda kwa wazazi kwanza badala ya kwenda kwa mtu wa nje muanze kuvuana nguo pale!

Hapana sidhani kama ni Ushauri mzuri. Hata iwe wazazi wa mkeo tena ndio inapendeza zaidi wajue ubaya wa mtoto wao! Hapo Chadema wakubali kuachia sii kila kitu watakubaliwa na CCM.

Matakwa ya Chadema ni ya Kisiasa na yanahusu mgongano wao Kisiasa, na tunajua mengi ni CCM kupitia matukio kadhaa ya Kisiasa ambayo yanatakiwa kurekebishwa kimfumo. Waweke masharti yanayowezekana.
 
Kama tulishindwa kuzuia matatizo kabla hayajatokea Oct 29 , watu wakauawa na TV za dunia zikaonyesha kuna kujishusha chini zaidi ya hapo? At face value watu 500 kwa siku 2-3 hapa tuli hit rock bottom.

Mkuu narudia tena at face value kwamba ni watu 500 hivi hili unaweza kusema ni jambo dogo.
Kenya kwa wiki 3 walikufa watu 1000, huoni tatizo hapo
Kama unakorofishana na Mkeo na mkashindwa kusuluhisha ni vema mkaenda kwa wazazi kwanza badala ya kwenda kwa mtu wa nje muanze kuvuana nguo pale!
To assume Mzee Warioba ndiye mzazi. Kabla ya matatizo alisema kuna tatizo akatukanwa na upande mmoja wa ndoa . Tuonyeshe wazazi wawili watatu tu wenye credibility and integrity to handle such a disaster.

JokaKuu kasema hatuna wazazi, kuna tab gani kwenda kwa jirani?
Matakwa ya Chadema ni ya Kisiasa na yanahusu mgongano wao Kisiasa, na tunajua mengi ni CCM kupitia matukio kadhaa ya Kisiasa ambayo yanatakiwa kurekebishwa kimfumo.
Unaweza kusema hivyo lakini jiulize kwanini CHADEMA wana public support kiasi cha CCM kuwahitaji.
Usisahau kuna UMMA ndani ya CHADEMA usioweza ku ignore. Wamejaribu uchaguzi mkuu leo wanavuna mabua! Wali ignore leo wanatafuta maridhiano wasiyoweza kuyaeleza ni ya nini!
 
Well basi naelewa tatizo liko wapi. Hata ningekuwa.mimi rais nisingekubali swala la ndani lijadiliwe mbele ya msuluhishi kutoka nje (kujishusha kiasi hicho) kama vile ni swala kubwa linalohusiana na Sheria za Kitaifa.

Kama unakorofishana na Mkeo na mkashindwa kusuluhisha ni vema mkaenda kwa wazazi kwanza badala ya kwenda kwa mtu wa nje muanze kuvuana nguo pale!

Hapana sidhani kama ni Ushauri mzuri. Hata iwe wazazi wa mkeo tena ndio inapendeza zaidi wajue ubaya wa mtoto wao! Hapo Chadema wakubali kuachia sii kila kitu watakubaliwa na CCM.

Matakwa ya Chadema ni ya Kisiasa na yanahusu mgongano wao Kisiasa, na tunajua mengi ni CCM kupitia matukio kadhaa ya Kisiasa ambayo yanatakiwa kurekebishwa kimfumo. Waweke masharti yanayowezekana.

..Kwenye post yako nyingine ulisema Jaji Warioba, na Prof.Shivji, ni miongoni mwa Watanzania wenye uwezo na uadilifu wa kusimamia mazungumzo ya maridhiano.

..Na mimi sipingani na wewe kuhusu uadilifu, uzoefu, na uwezo wa kitaaluma, wa Jaji Warioba, na Prof.Shivji.

..Sasa mimi nataka nikuulize hivi kuna Mtanzania mwenye sifa za kushughulika na mgogoro tulionao kuliko Jaji Mohamed Chande Othman? Je, alipoteuliwa nini kilitokea? Je, ripoti ya OCT 29 inashabihiana na sifa na CV ya Jaji Chande Othman kimataifa?
 
Kama tulishindwa kuzuia matatizo kabla hayajatokea Oct 29 , watu wakauawa na TV za dunia zikaonyesha kuna kujishusha chini zaidi ya hapo? At face value watu 500 kwa siku 2-3 hapa tuli hit rock bottom.

Mkuu narudia tena at face value kwamba ni watu 500 hivi hili unaweza kusema ni jambo dogo.
Kenya kwa wiki 3 walikufa watu 1000, huoni tatizo hapo

To assume Mzee Warioba ndiye mzazi. Kabla ya matatizo alisema kuna tatizo akatukanwa na upande mmoja wa ndoa . Tuonyeshe wazazi wawili watatu tu wenye credibility and integrity to handle such a disaster.

JokaKuu kasema hatuna wazazi, kuna tab gani kwenda kwa jirani?

Unaweza kusema hivyo lakini jiulize kwanini CHADEMA wana public support kiasi cha CCM kuwahitaji.
Usisahau kuna UMMA ndani ya CHADEMA usioweza ku ignore. Wamejaribu uchaguzi mkuu leo wanavuna mabua! Wali ignore leo wanatafuta maridhiano wasiyoweza kuyaeleza ni ya nini!
Narudia kusema - Swala la Oct 29 halihusiki na maridhiano ya Chadema. Kama mtaliongeza basi CCM itasema Chadema ndio chanzo cha mauaji hayo. Hivi unadhani Tundu Lissu kukutwa na hatia ya Uchochezi ni bahati mbaya! Think big...

Kumbukeni yule Mchungaji wa Rwanda amehukumiwa kama Mchochezi kesi ya Genocide Rwanda kwa kuchochea tu mauaji ya Kimbari yakatokea Rwanda. Kagame kaepuka kuwa chanzo na sababu.

Na tume hii maadam inatafuta nani alosababisha VURUGU za Oct. 29 sio nani aloua watu 500+ inaandaa ushahidi wa Wananchi Tanzania nzima kuwa kina nani walosababisha. Ushahidi wa Watanzania utaupingaje?

Tulienda ICC Samia anapundua kama alivyoweza Kenyatta wa Kenya. Same case on same basis. Kwa hiyo mtazamo wangu mimi haya mambo tuyamalize wenyewe ndani.

Hata kama ni kushikana mashati, na baadae sisi wenyewe tutawahukumu walotufokisha hapa. Kumbukeni maneno ya Polepole sii kwamba watu hawajui ama wamekubali yaishe! Laa hasha wameyahifadhi vifuani mwao.

Tunahitaji tu kupiga hatia ya kwanza nayo ni kufikia maridhiano ya Kitaifa. Achana na lawama hazisaidii kiti, mazungumzo hutujengea imani kuna mwisho wa yote haya na wala hauko mbali sana.
 
..Samia na Serikali wakifikishwa ICC itakuwa ni kwasababu ya mauaji, na sio kwasababu ya kuvunja mabaa, na kuchoma moto sheli.

..Mchungaji wa Rwanda anahusishwa kwa kuwachochea Interahamwe [ uv-ccm ya utawala wa habyarimana ] kufanya mauaji ya Kimbari.

..Tundu Lissu huwezi kumhusisha na kushawishi / kuchochea Polisi na vyombo kufanya mauaji kiholela. Yeye mwenyewe ni mhanga wa watu hao hao waliouwa OCT 29.
 
Narudia kusema - Swala la Oct 29 halihusiki na maridhiano ya Chadema. Kama mtaliongeza basi CCM itasema Chadema ndio chanzo cha mauaji hayo. Hivi unadhani Tundu Lissu kukutwa na hatia ya Uchochezi ni bahati mbaya! Think big...
Labda sijakuelewa. CHADEMA hawakushiriki uchaguzi , wanahusika vipi na Oct29?
Na tume hii maadam inatafuta nani alosababisha VURUGU za Oct. 29 sio nani aloua watu 500+ inaandaa ushahidi wa Wananchi Tanzania nzima kuwa kina nani walosababisha.
Ndiyo maana watu hawana imani na Tume! Hadidu za rejea zimeandaliwa na wanaonyeshewa vidole
Tulienda ICC Samia anapundua kama alivyoweza Kenyatta wa Kenya. Same case on same basis. Kwa hiyo mtazamo wangu mimi haya mambo tuyamalize wenyewe ndani.
Kuna tatizo gani kama atapindua! at least kutakuwa na chombo impartial kitakachomsafisha
In fact kwakwe itakuwa ni nzuri kwasababu bias za Tume na Mahakama zitakuwa zimeondolewa
Tunahitaji tu kupiga hatia ya kwanza nayo ni kufikia maridhiano ya Kitaifa.
You're dancing to unknown tune dude! Maridhiano ya nini, kati ya nani na nani na kwasababu gani

Watu wengi ni ignorant kuhusu maridhiano. Maridhiano ''consensus '' ni conclusion ya jambo. Kinachoanza kwanza ni ku define tatizo then deliberate it halafu ndiyo mnafikia consensus ikimaanisha kulikuwa na tatizo

Wapo wanaotaka conclusion bila kutueleza ni ya kitu gani!
Achana na lawama hazisaidii kiti, mazungumzo hutujengea imani kuna mwisho wa yote haya na wala hauko mbali sana.
Hatutaki yale ya Zanzibar ya muafaka kila baada ya miaka 5. Watu wanataka suluhu ya kudumu
 
..Kwenye post yako nyingine ulisema Jaji Warioba, na Prof.Shivji, ni miongoni mwa Watanzania wenye uwezo na uadilifu wa kusimamia mazungumzo ya maridhiano.

..Na mimi sipingani na wewe kuhusu uadilifu, uzoefu, na uwezo wa kitaaluma, wa Jaji Warioba, na Prof.Shivji.

..Sasa mimi nataka nikuulize hivi kuna Mtanzania mwenye sifa za kushughulika na mgogoro tulionao kuliko Jaji Mohamed Chande Othman? Je, alipoteuliwa nini kilitokea? Je, ripoti ya OCT 29 inashabihiana na sifa na CV ya Jaji Chande Othman kimataifa?
Jaji Mohamed Chande alielekezwa kufanya kazi gani na sii kuhukumu. Alielekezwa kama ilivyo Tume hii nyingine wotw wameelekezwa report zao zitqzame eneo gani. Ndio maana hata Warioba na Shivji walikosoa na maelekezo hayo. Mzee Warioba akapigwa kipapai, sijii mzee wangu anaendeleaje!

Kaa hiyo siwezi kumlaumu Jaji Othman wala kiongozi yeyote alopewa jukumu maalum kwa kulenga eneo maalum.l tofauti na report za tume zingine walopewa kukusanya maoni ya Wananchi kuhusiana na Katiba Mpya.

Mwambie Jaji Chande awe msuluhishi unaweza kukushangaza akisikiliza madai ya pande mbili. Hata mimi leo hii Sami aniteuwe kuwa Mkuu wa Mkoa unaweza shangaa nitakavyo badilika maana yanilazimu nichukue Upande. Yule kijana Katambi mnashangaa bure alivyobadilika!
 
Serikali ya CCM chini ya Samia inai-blackmail Chadema kwa kumtumia Lissu, yaani Chadema wakubali masharti ya CCM ili Lissu aachiliwe huru.
Inahitaji akili ya mpumbavu ili kuiamini CCM hii inayopokea ushauri wa Wasira na Kikwete.
FB_IMG_1765768878021.jpg
FB_IMG_1747646513450.jpg
 
Labda sijakuelewa. CHADEMA hawakushiriki uchaguzi , wanahusika vipi na Oct29?

Ndiyo maana watu hawana imani na Tume! Hadidu za rejea zimeandaliwa na wanaonyeshewa vidole

Kuna tatizo gani kama atapindua! at least kutakuwa na chombo impartial kitakachomsafisha
In fact kwakwe itakuwa ni nzuri kwasababu bias za Tume na Mahakama zitakuwa zimeondolewa

You're dancing to unknown tune dude! Maridhiano ya nini, kati ya nani na nani na kwasababu gani

Watu wengi ni ignorant kuhusu maridhiano. Maridhiano ''consensus '' ni conclusion ya jambo. Kinachoanza kwanza ni ku define tatizo then deliberate it halafu ndiyo mnafikia consensus ikimaanisha kulikuwa na tatizo

Wapo wanaotaka conclusion bila kutueleza ni ya kitu gani!

Hatutaki yale ya Zanzibar ya muafaka kila baada ya miaka 5. Watu wanataka suluhu ya kudumu
Maridhiano ya Chadema na CCM hayanihusu mimi na ndio maana nimeelekeza kwao tu. Kama kuna.Maridhiano mengine ya Kitaifa basi hayo hatahusu Mauaji ya Oct. 29, kupotea na kutekwa kwa baadhi ya watu, kukosoana hasa rais na Utawala katika Utawala bora na Upande wa Serikali nao watakuwa na madai yao yatazingatiwa na kutungiwa Sheria.

Huo utakuwa msaada mkubwa marekebisho ya Katiba ama Uandishi wa Katiba Mpya. Nadhani Chadema hawakwenda kwenye mkutano wa juzi kwa sababu hauwahusu wao na madai yao ni ya kwao wao ambao pengine hayawahusu vyama vingine vilivvyokubaliana na Serikali ya Samia.

Wanataka madai yao yashughulikiwe kivyao tofauti na maridhiano ambayo CCM inayataka sijui na kina nani na kwa sababau gani. Niliweka mada hiyo huko nyuma bila shaka unakumbuka.
 
Jaji Mohamed Chande alielekezwa kufanya kazi gani na sii kuhukumu. Alielekezwa kama ilivyo Tume hii nyingine wotw wameelekezwa report zao zitqzame eneo gani.
Mpaka hapa hujaona umuhimu wa kuwa na mediator kutoka nje ya Nchi!!
Ndio maana hata Warioba na Shivji walikosoa na maelekezo hayo. Mzee Warioba akapigwa kipapai, sijii mzee wangu anaendeleaje!
Walikosoa kwasababu Tume ilitakiwa iwe ya ''white paper'' , iende ikafanye utafiti na kuandaa terms of reference zake. Hii ya Chande ilipewa maelekezo 'bias' ndiyo maana iliweza kueleza kwa kina uharibifu na si vifo
Kaa hiyo siwezi kumlaumu Jaji Othman wala kiongozi yeyote alopewa jukumu maalum kwa kulenga eneo maalum.l tofauti na report za tume zingine walopewa kukusanya maoni ya Wananchi kuhusiana na Katiba Mpya.
Jaji Kisanga alipewa kazi kama hiyo, kwa kujali heshima yake akazungumza yaliyo nje yahadidu rejea. Mkapa alimtukana sana tena katika TV na Radio nchi zima ikisikia. Moja ya jambo aliloongea Jaji Kisanga ilikuwa suala la Muungano! Leo Muungano ni tatizo kubwa kuliko wakati analiongelea. Heshima ya Jaji Kisanga ipo na inazidi.

Hoja ni kwamba kwa International figure kama Jaji O Chande kupewa kitu na kukifanya kwasababu amepewa bila kujali heshima yake na masilahi ya nchi ilikuwa ni low point katika utumishi wake.
Mwambie Jaji Chande awe msuluhishi unaweza kukushangaza akisikiliza madai ya pande mbili. Hata mimi leo hii Sami aniteuwe kuwa Mkuu wa Mkoa unaweza shangaa nitakavyo badilika maana yanilazimu nichukue Upande. Yule kijana Katambi mnashangaa bure alivyobadilika!
Labda kama atarudi tumboni na kuzaliwa upya! kwa huyu wa leo amepoteza credibility and integrity!
 
Mkandara umeandika kama hukuwepo duniani kwamba Leo ndio umefufu kutoka makabulini inashangaza eti hujui nini CHADEMA wanakitaka unapiga TU milele kama kasuku
Maridhiano ya kweli mara nyingi hukitoa chama tawala kwenye utawala CCM atakuwa mwathirika kwa maziingira ya sasa ya kisiasa ndiyo maana ni vigumu CCM kukubali maridhiano na katiba mpya ya kweli ikiakisi matakwa ya Chadema na wananchi wazalendo. Huko Afrika Kusini makaburu walianguka kwa maridhiano. CCM analijua hilo. Itakuwa vigumu ku forge a way forward. Muhimu kwa CCM ningeshauri ilegeze kwa baadhi ya mifumo kipindi cha Kikwete ilifanikiwa ingawa walihisi kuondolewa madarakani hivyo kubadilika na kuegemea kwenye dola kimfumo.
 
Back
Top Bottom