Kujikwaa kisiki mara mbili

Kujikwaa kisiki mara mbili

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
16,271
Reaction score
9,909
Nimewahi kumsikia Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisema Chadema haiwezi kwenda katika Maridhiano pasipo Kiongozi wao TAL kuachiwa huru bila masharti.

Na kuna baadhi ya.Wanachama wanakataa kabisa maridhaliano ya Serikali pasipo Uwajibikaji wa Serikali kufuatia matukio kadhaa yalowahi tokea, ilihali Serikali nayo inadai Chadema wamekuwa wakitumia wanaharakati na taasisi za nje kuvuruga Amani nchini. Msema kweli nani hata sielewi..

Sasa, katika tafakari zangu nimejikuta najiuliza maswali kadhaa kulingana mazingira ya hoja hii ya Heche na baadhi ya watu kwa sababu zifuatazo

Waingereza husema "Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me” na ingine yasema. " Once bitten, twice Shy" ni katika Maudhui hayo hayo nayotaka kuyajadili.

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu akiwa matibabu kule Ubelgiji alikutana na rais Samia wakakubaliana kufanya mazungumzo kulenga maridhiano baina ya Utawala wake na Chadema kwa masharti ambayo Tundu Lissu yaliyainisha ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi Mwenyekiti wa Chadema wakati huo Nd. Freeman Mbowe pamoja na masharti mengineyo sitoyataja yote.

Mbowe aliachiwa huru, wakaanza mchakato na vikao vya Maridhiano ambayo kufikia hatua za mwisho mwisho l, Chadema walijitoa kwa madai ya kwamba Rais Samia akikataa kuweka makubaliano yao katika maandishi na kuyasaini. Tunaambiwa Chadema Hawakutaka maridhainao ya maneno matupu pasipo Maandishi.

Kufuatia matokeo yale najiuliza maswali yafuatayo.

  • Je, Chadema wanaweza kukubali kuingia katika maridhiano na rais ambaye alikataa kusaini makubaliano ya awali iweje leo atakuwa mkweli?
  • Je, rais Samia anaweza kubali maridhiano na Chadema ambao anajua yawezekana ni mtegilo kama ule wa awali walojitoa katika maridhiano yale kwa sababu ambazo Yeye na majumbe wake waliona hazina msingi?
Waswahili husema mnafiki ana ishara tatu..

Maasalaam
 
Serikali haina nia ya dhati ya kutafuta maridhiano na yeyote, inachofanya ni 'Usanii' tu kama ule waliomfanyia Mbowe.
Sasa kwa nini Heche anataka Tundu Lissu aachiwe huru kwanza ili Chadema washiriki wakati anajua Serikali haina nia ya dhati ya kufanya maridhiano?
 
Sawa, lakini sio Lissu alokataa maridhiano na Samia kabla hata hajakamatwa?
Kikao cha Maridhiano ni hatua ya mwisho kabisa katika mchakato wa kuridhiana.

Kama kweli serikalii ya CCM inataka hayo maridhiano ni vyema waķawaita/kuwafuata washika dau wote kila mmja aelèze dukuduku zake na mapendekezo kabla ya kiķao chenyewe.

Tofauti na hivyo itakuwa vigumu sana kufanya maridhiano na watu ambao kila mmoja ameangalia upande wake.
 
Nimewahi kumsikia Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisema Chadema haiwezi kwenda katika Maridhiano pasipo Kiongozi wao TAL kuachiwa huru bila masharti.

Na kuna baadhi ya.Wanachama wanakataa kabisa maridhaliano ya Serikali pasipo Uwajibikaji wa Serikali kufuatia matukio kadhaa yalowahi tokea, ilihali Serikali nayo inadai Chadema wamekuwa wakitumia wanaharakati na taasisi za nje kuvuruga Amani nchini. Msema kweli nani hata sielewi..

Sasa, katika tafakari zangu nimejikuta najiuliza maswali kadhaa kulingana mazingira ya hoja hii ya Heche na baadhi ya watu kwa sababu zifuatazo

Waingereza husema "Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me” na ingine yasema. " Once bitten, twice Shy" ni katika Maudhui hayo hayo nayotaka kuyajadili.

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu akiwa matibabu kule Ubelgiji alikutana na rais Samia wakakubaliana kufanya mazungumzo kulenga maridhiano baina ya Utawala wake na Chadema kwa masharti ambayo Tundu Lissu yaliyainisha ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi Mwenyekiti wa Chadema wakati huo Nd. Freeman Mbowe pamoja na masharti mengineyo sitoyataja yote.

Mbowe aliachiwa huru, wakaanza mchakato na vikao vya Maridhiano ambayo kufikia hatua za mwisho mwisho l, Chadema walijitoa kwa madai ya kwamba Rais Samia akikataa kuweka makubaliano yao katika maandishi na kuyasaini. Tunaambiwa Chadema Hawakutaka maridhainao ya maneno matupu pasipo Maandishi.

Kufuatia matokeo yale najiuliza maswali yafuatayo.

  • Je, Chadema wanaweza kukubali kuingia katika maridhiano na rais ambaye alikataa kusaini makubaliano ya awali iweje leo atakuwa mkweli?
  • Je, rais Samia anaweza kubali maridhiano na Chadema ambao anajua yawezekana ni mtegilo kama ule wa awali walojitoa katika maridhiano yale kwa sababu ambazo Yeye na majumbe wake waliona hazina msingi?
Waswahili husema mnafiki ana ishara tatu..

Maasalaam
Gentleman,
those are useless, meaningless and completely helpless political stands, politically speaking :1Head:
 
Sasa kwa nini Heche anataka Tundu Lissu aachiwe huru kwanza ili Chadema washiriki wakati anajua Serikali haina nia ya dhati ya kufanya maridhiano?

..Chadema pia wamesema wanataka maridhiano yasimamiwe na msuluhishi toka nje, asiye na upande, ili udanganyifu uliotokea ktk mazungumzo ya awali usijirudie.

..Wapambe wa Ccm hawataki kusikia hoja ya maridhiano kuhusisha msuluhishi toka nje wakidai huko ni kuingiliwa ktk mambo yetu ya ndani.

..Kwa maoni yangu, hoja hiyo haina nguvu kwasababu hata ktk Tume ya Uchunguzi inayoongozwa na Jaji Lila kuna wajumbe toka nje ya nchi.
 
Nimewahi kumsikia Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisema Chadema haiwezi kwenda katika Maridhiano pasipo Kiongozi wao TAL kuachiwa huru bila masharti.

Na kuna baadhi ya.Wanachama wanakataa kabisa maridhaliano ya Serikali pasipo Uwajibikaji wa Serikali kufuatia matukio kadhaa yalowahi tokea, ilihali Serikali nayo inadai Chadema wamekuwa wakitumia wanaharakati na taasisi za nje kuvuruga Amani nchini. Msema kweli nani hata sielewi..

Sasa, katika tafakari zangu nimejikuta najiuliza maswali kadhaa kulingana mazingira ya hoja hii ya Heche na baadhi ya watu kwa sababu zifuatazo

Waingereza husema "Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me” na ingine yasema. " Once bitten, twice Shy" ni katika Maudhui hayo hayo nayotaka kuyajadili.

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu akiwa matibabu kule Ubelgiji alikutana na rais Samia wakakubaliana kufanya mazungumzo kulenga maridhiano baina ya Utawala wake na Chadema kwa masharti ambayo Tundu Lissu yaliyainisha ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi Mwenyekiti wa Chadema wakati huo Nd. Freeman Mbowe pamoja na masharti mengineyo sitoyataja yote.

Mbowe aliachiwa huru, wakaanza mchakato na vikao vya Maridhiano ambayo kufikia hatua za mwisho mwisho l, Chadema walijitoa kwa madai ya kwamba Rais Samia akikataa kuweka makubaliano yao katika maandishi na kuyasaini. Tunaambiwa Chadema Hawakutaka maridhainao ya maneno matupu pasipo Maandishi.

Kufuatia matokeo yale najiuliza maswali yafuatayo.

  • Je, Chadema wanaweza kukubali kuingia katika maridhiano na rais ambaye alikataa kusaini makubaliano ya awali iweje leo atakuwa mkweli?
  • Je, rais Samia anaweza kubali maridhiano na Chadema ambao anajua yawezekana ni mtegilo kama ule wa awali walojitoa katika maridhiano yale kwa sababu ambazo Yeye na majumbe wake waliona hazina msingi?
Waswahili husema mnafiki ana ishara tatu..

Maasalaam
Mkandara umeandika kama hukuwepo duniani kwamba Leo ndio umefufu kutoka makabulini inashangaza eti hujui nini CHADEMA wanakitaka unapiga TU milele kama kasuku
 
Waingereza husema "Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me” na ingine yasema. " Once bitten, twice Shy" ni katika Maudhui hayo hayo nayotaka kuyajadili.

Maasalaam
Pia kuna "You can fool some people for sometimes, but you can't fool all the people all the times"
Chadema wameamua kuwa they are not fools, but sisi Watanzania, we are!.
 
Hoja fikirishi sana

mbowe alitolewa ndipo maridhiano yakaanza

Leo LISU hastahili kutoka ili maridhiano yafanhike

Uzito wakesi ,lisu uchochezi while mbowe ugaidi
Lakini serikali iliona gaidi atoke mchochezi hapana!

Lisu nimihimu kuwa nje anaumuhimu kuliko wote tuliopo nje ya nondo yaani Lisu anaumuhimu kuliko sisi milion 64.99 tuliopo nje
 
Chadema walitaka maridhiano kabla ya uchaguzi, wapo waliopendekeza hata uchaguzi usogezwe mbele Ili maridhiano muhimu yafanyike kwanza.

Ila yote hayo yalikataliwa na wenye mamlaka.

Unajua mnapojibu hoja upande mmoja tu, mimi naweka walakini juu yake. Sasa ili mjadala uwe mpana zaidi, vema tusiegemee upande mmoja. Nilitegemea japo mtu mmoja aje na msimamo wa Serikali nae nimuulize lakini nashangaa kila anayeandika ni kuhusu kuitetea Chadema.
Haipendezi ionekane tunabishana juu ya hili bali tujadili kwa kutazama mawazo ya pande zote mbili ndio Ukweli utajitenga.

Anyway sitochoka kuhoji msimamo wa Chadema maana siuelewi mpaka leo hii. Na nakumbuka vema Chadema walipokataa kuendelea na Maridhiano yale walisema Mbowe kalamba Asali hawataki tena kuendelea na Maridhiano na rais Samia.

Alotaka Maridhiano ya Kitaifa kabla ya Uchaguzi Mkuu alikuwa Polepole na alisema wazi tusikubali Maridhiano baada ya Uchaguzi, sikuwahi wasikia Chadema wakisema watarudi mezani kuendelea na maridhiano. Sijawahi niseme kweli yangu najua walikataa kabisa kuendelea na maridhiano.

Na nadhani msimamo huu wa kukataa kuendelea na maridhiano na Samia ndio ilikuwa SABABU kubwa ilomwangusha Mbowe kwenye Uchaguzi Mkuu wakisema walimwambia watoke yeye bado alikuwa anakazania waendelee..

Sikumbuki kabisa wakati wowote wa Tundu Lissu akiwa Mwenyekiti wa Chama toka January 30, 2025 hadi April 09, 2025 siku Tundu Lissu anakamatwa, Chadema walikuwa wapo tayari kurudi mezani na Serikali au Samia.

Isitoshe Wananchi hawajui ama hatujui katika Makubaliano yale walikubaliana nini, marekebisho gani yalifanyika kulingana na makubaliano na yapi yalikwamisha makubaliano yale zaidi ya Wananchi kusikia Viongozi pande zote mbuli wakilaumiana.

Itapendeza zaidi kama Tungesikia pia Upande wa Serikali wao walikataa nini na kwa nini rais anayetamba kwa 4R akatae kuridhia makubaliano kwa maandishi?

Ndio maana nimekuja na hoja hii kwetu sisi tuchambue nani mwenye kusema ama kuficha UKWELI.
 
Mkandara umeandika kama hukuwepo duniani kwamba Leo ndio umefufu kutoka makabulini inashangaza eti hujui nini CHADEMA wanakitaka unapiga TU milele kama kasuku
Unajua umesema kweli kabisa kwamba Sijui Chadema wanataka nini. Kama wewe unajua tafadhali nambie maana hata hao CCM sijui wanataka nini ila najua mmoja wao ni Mnafiki na ishara za mnafiki ni 3.

1. Kusema uongo: Huongea uongo anapozungumza.
2. Kutotimiza ahadi: Huvunja au hatekelezi ahadi anapotoa.
3. Kufanya khiyana: Hukosa uaminifu au hufanya khiyana anapoaminiwa.
 
Sasa kwa nini Heche anataka Tundu Lissu aachiwe huru kwanza ili Chadema washiriki wakati anajua Serikali haina nia ya dhati ya kufanya maridhiano?
Mkuu Unakosea sana. Heche hajasema akiachiwa Lissu wataenda kwenye maridhiano.

Kuachiwa kwa Lissu ni condition moja tu kati ya conditions kadhaa zinazotakiwa ikiwemo ya maridhiano Chini ya msimamizi huru.
 
Maazimio ya Chadema kuhusu maridhiano ni haya hapa:
Masharti na madai ya CHADEMA


1. Kuachiliwa huru kwa Tundu Lissu – Mwenyekiti wa CHADEMA aachiwe huru kabla ya kuanza mazungumzo ya maridhiano.


2. Kuachiliwa kwa watu waliotekwa na kupotezwa – Serikali ichukue hatua kuhusu watu waliotekwa, kupotezwa na wale wanaoshikiliwa kwa sababu za kisiasa.


3. Kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi – Matukio ya mauaji, vifo na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 yachunguzwe kwa uhuru na bila upendeleo.


4. Uwajibikaji wa waliohusika – Wale watakaobainika kuhusika na mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu wawajibishwe kisheria.


5. Mpatanishi huru – mazungumzo yaongozwe na mpatanishi anayeaminika na pande zote mbili, badala ya Serikali kuwa upande mmoja wa mazungumzo na pia msimamizi wake.


6. Kukubali kwamba kuna mgogoro wa kisiasa – Serikali na vyama vya upinzani zikubali kuwepo kwa matatizo ya kisiasa yanayohitaji kutatuliwa badala ya kujifanya kuwa kila kitu kiko sawa.


7. Katiba mpya na mageuzi ya kidemokrasia – Kuwepo kwa mchakato wa kweli wa kupata Katiba mpya na kuboresha mfumo wa uchaguzi, uhuru wa mahakama na demokrasia.


8. Uhuru wa vyama vya siasa – CHADEMA na vyama vingine viruhusiwe kufanya shughuli zao za kisiasa bila vitisho, ukandamizaji au kukamatwa kiholela.
 
Back
Top Bottom