Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Mbinguni kuna makao mazuri sana, ya nini kuhangaikia mapito ya hapa duniani huku tukijua tunapita tu.... bwana Yesu yuko bize kutuandalia makao mazuri kwa kila mmoja wetu.

Farijianeni kwa maneno hayo, mengine yote ni ubatili mtupu.... na hata usiku utapokwisha.
 
Umeongea vyema kabisa.

Wengi wenye mijumba mikubwa wana zaidi ya vyumba huko ndani.

Kuna swimming pool, garage, movie theatre, sports arcade, bathrooms za kutosha, studio ya kurekodia, ofisi, library, walk in closets, kitchens za kutosha, living rooms za kutosha.

Sio kila mtu anapenda kujibana kwenye 3 bedrooms.
...umenena vyema Mkuu. Kwa mfano Mimi in lazima jumba langu uwanja Wa Basketball ambao pia utaweza kutumika pia kwa Tennis na Badminton in lazima uwepo!!
Mambo ya kuishi kajumba ambako mkiongezeka kidogo tu inabidi kuweka traffic lights, Mimi hapana kwa kweli...!!
 
Wote mliojibu labda bado ni watoto wadogo sana tena wa maskini,

Nyie, mjumba wangu mmoja una vyumba 35, nipo na mke wangu tu, tumejimega ghorofa ya kwanza chini chumba 1 na sebure,

Na vyumba vilivyo baki tumepangisha Guest house, na Hotel, na fremu za maduka 9, hatujala na kutembelea watoto ulaya kwa hela yetu? ndugu washamba hawajapata ajira? tunapata hela kwa wakati.

mwingine una vyumba 7 hostel ya wanafunzi nimefanya

wa tatu una vyumba 4 Mbezi beach, nimepangisha nyumba nzima!
 
Kinachobadilika ni matumizi. Structure ?umekariri chumba cha kulala ni square,library au gym haiwezi kuwa square. Kama ushajenga ungenielewa. Kuna stage ya nyumba ukiwa unajenga ukiwa na MTU inabidi umuambie hapa ni jiko,library,bedroom etc kwasababu haviko kama nyinyi mlivyokariri
Teh teh teh...'ungekuwa emeshajenga'! Mkuu kwani mnafahamiana?
 
Pesa ikiwepo nyumba yangu ikikosa vyumba 20 basi itakua na vyumba 30

yani nizaliwe kwenye nyumba ya vyumba vi 4 namimi nije ishi kwenye nyumba hiyo

nizaliwe nguo naweka kabatini,namimi niendeleze huo umaskini Hapana BIG NO

umaskini mwisho kwangu nimesema,vizazi vyangu kuanzia wanangu lazima waishi tofauti

Chumba cha nguo
Chumba cha viatu
Chumba cha mafuta
Chumba cha movie
Chumba cha maombi
Chumba cha story
Chumba cha library
Chumba changu

yani nina list ya vyumba vya muhimu vingi sana,nasema hiviiiii mawazo yangu yatabaki kama mawazo only if "ntabaki kuwa maskini"

ila nikishika pesa nawambia hivii mimi sijengi nyumba ya kichoyo kabisa nishasemaga,Afe refa afe kipa wafe wachezaji

Mpira lazima uchezwe dk 90 na mshndi apatikane,Msinchanganye.
Chumba cha nguo, chumba cha viatu, chumba cha soxy, chumba cha kuvalia!

Mateso yote hayo ya nini kutawanya activities zenye kufanana?

Tusiseme sana, tupige wote magoti tukuombee umri mrefu 80+.

Utakuwa unasahau hata chumba cha kuvalia kilipo! Tuombe uzima.
 
tuombe uzima mkuu,si rahisi kunielewa naongelea kitu ya aina gani.
 
View attachment 1273865

Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.

Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.

Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,

.......Nikiwa mzee nageuza lodge inaendelea kunilea.
 
Nimekusikia mkuu , itabidi hiki kijumba changu cha ghorofa 4 nihame nikifanyie mipango mingine , yaani uzi huu ni kama nimetungiwa mimi !
 
Watu tuliotokea kwenye umaskini (hasa wa africa) huwa tuna shida sana......mara nyingi huwa tunadhamini sana mali kuliko kitu kingine lakini pia tunapenda vitu vitakavyotuonyesha kwenye jamii.......yaani kujenga nyumba ya vyumba vitatu mtu anawaza hivi na uprofesa wangu wote watu wataniona je?........wakati huo huo wazazi ama jamaa zake wa karibu wanaishi kwenye nyumba za udongo kijijini hata kama hawaishi kwenye nyumba za udongo lakin maisha yao unakuta ni duni mno..... there are so many things we could do kwenye investments zikasaidia vizazi na vizazi.....tatizo letu ni exposure na umaskini
Kasome tena, hata kwenye vitabu vya Mungu kuna mfalme Suleimani alijenga
mjengo wa haja.
 
Back
Top Bottom