Kuitwa Training TAESA

Kuitwa Training TAESA

Sawa mkuu,tayari nimehudhuria Training then next week kutakua na interview.Hivi baada ya Interview inachukua muda gani kupelekwa internship?pia academic certificates zinazohitajika kwenye interview inahusisha Transcript ya chuo?
Hawatabiriki mimi nilifanyaga interview mwaka jana December mpaka leo sijawahigi kuitwa for intern so inategemea na bahati yako si unajua corona iliingilia kati hpo so vingi vilikwama si ajabu ndo mana wengne hatukuitwa and transcript pia ni muhimu nenda nayo
 
Baada ya hapo utapigiwa simu kujulishwa kuhusu tarehe ya kufanya interview. Baada ya interview, ikitokea nafasi ya internship unayofit basi utaitwa kwa ajili ya orientation ambapo kubwa hasa huwa ni kuelekezwa ethics za kitumishi na baadaye utatajiwa kituo chako unachotakiwa kureport kwa ajili ya kuanza internship.
Ukifanikisha hatua hiyo utapewa contract ya posho ya laki na nusu kwa mwezi kwa ajili ya nauli na chakula,
Maisha haya daah!
 
Intern unapangiwa sehemu mbalimbali, na mkataba wa intern kikawaida ni mwaka mmoja. So sehemu ambayo unafanyia intern wakikupenda wanakuchukua moja kwa moja ndio mana unaweza sema wamepata intern toka TaESA.

Kumbuka hawatoi ajira permanent, hiyo kazi ni ya Utumishi. Ila CV yako itakuwa inabustiwa kupitia wao. Kuna jamaa zangu kadhaa waliingia intern shirika flani TaESA akiwa ndo kawaweka. Utendaji wao wa kazi ulipelekea mmoja kupewa mkataba wa kudumu.

Intern hizo unapangiwa sehemu yoyote tu ile yenye uhitaji ila sio pale kwao. Mfano unaweza pelekwa TRA, TANESCO, NGOs mbalimbali. Mfano kuna mwaka flani nilienda omba intern Red Cross nkaambiwa wao wanachukua watu kutoka TaESA, so nkajisajili kwanza kule.
Anhaa kumbe
 
Iyo training ni wanafundisha tu interview techniques na jinsi ya kuandika cv and cover letters basi usihisi ni kazi ushapata hapo ni unapigwa training kama kawaida then badae ndo wanaeza kukuita ufanye interview yao then utaingia kwenye system zao ikitokea kazi ya kada yako wanakupangia nafasi ya intern
Kuna kaposho kokote wanatoa? Au mtu unaishia kuchoma mafuta tu
 
Hawatabiriki mimi nilifanyaga interview mwaka jana December mpaka leo sijawahigi kuitwa for intern so inategemea na bahati yako si unajua corona iliingilia kati hpo so vingi vilikwama si ajabu ndo mana wengne hatukuitwa and transcript pia ni muhimu nenda nayo
Kweli mkuu Covid imevuruga mambo mengi sana,nakuja pm unisaidie maswali muhimu uliyoulizwa kwenye Interview.
 
Kuna kaposho kokote wanatoa? Au mtu unaishia kuchoma mafuta tu
Ukiitwa training, interview au orientation hupewi hata mia. Ukianza internship wanalipa laki na nusu kwa mwezi. So ukibahatika ofisi utakayopangiwa kufanya hiyo internship wakawa na huruma ndio utapona
 
Kweli mkuu Covid imevuruga mambo mengi sana,nakuja pm unisaidie maswali muhimu uliyoulizwa kwenye Interview.
Interview ya pale unategemea na taaluma uliyonayo pamoja na masuala mtambuka katika jamii
 
Ukiitwa training, interview au orientation hupewi hata mia. Ukianza internship wanalipa laki na nusu kwa mwezi. So ukibahatika ofisi utakayopangiwa kufanya hiyo internship wakawa na huruma ndio utapona
Iv hawawez wakakupeleka ata magogoni pale?
 
Hivi Hawa ofisi zao ziko maeneo gani? Na kwa mtu anayekaa Gongolamboto apande usafiri wa kwenda wapi
Panda gari za kwenda Postal/kivukoni omba kushukia CBE (nimesahau kituo kinaiwaje). Ukishuka vuka upande wa pili kisha uliza TAESA au Labour court(mahakama ya kazi) basi TAESA na hiyo labour court zimefuatana. Japo kwa nje ofisi ya TAESA inatia huruma kidogo.
Unapoenda kujisajiri mara ya kwanza hakikisha unabeba vyeti vyako ORIGINAL vya kitaaluma.
 
Sio tuu kutia huruma na kuvunjisha maini pia
 
Back
Top Bottom