mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 473
- 1,448
Kazi unazofanya ni miongoni mwa vitu ambavyo vinakuchagulia mahala pa kuishi. Nimeishi sehemu nyingi za mjini na kijijini, nilichokiona mimi maisha ya mjini ni mazuri ukiwa na pesa nyingi na maisha ya kuishi kwenye kijiji kilichochangamka ni mazuri zaidi hata ukiwa na pesa kiasi.
Nimechukua location ya shamba langu moja lilipo na mara nyingi huwa nikitoka mjini huwa napumzika hapo na kulala, nimejikuta napenda sana haya mazingira, pana maji, umeme, barabara ipo ya uhakika, soko dogo na sehemu za starehe zipo, network ipo, ni sehemu ambayo nikiwa hapo shamba napata utulivu sana wa akili, sisumbuliwi na mtu.
Hii ipo tofauti na kwangu mjini mara umelala unasikia geti linagongwa unatoka mtu anakwambia nilikuwa nauza icecream au nasajili line, mara usikie mke na mume wanagombana, ukitoka unyoshe miguu mara umekoswa na bodaboda, mara huyu kakusimamisha akupige mizinga nk full kero.
Kwa upande wako ni sehemu gani nzuri kuishi katikati ya mji au pembeni kidogo ya mji.