Kuishi miaka mingi ni ishu ya Asili ya ukoo wenu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
Kwema Wakuu!

Kila ukoo unasifa zake. Unabaraka zake. Wapo waliobarikiwa Sura nzuri, wapo waliobarikiwa urefu, nguvu na wengine Akili.

Pia wapo waliobarikiwa kuwa na uzao mwingi.
Wapo waliobarikiwa asili ya Utajiri. Na wengi asili Yao ni umasikini.

Kila kitu kinaenda Kwa Mkondo.

Kitu pekee ambacho wengi hawakijui na ambacho ni muhimu ni kuwa,
Suala la umri Mkubwa pia ni ishu ya kijenetiki na kiroho.
Zipo koo ambazo watu wake Kupiga miaka 80-120 ni ishu ya kawaida. Kwao hilo sio ajabu.

Mjukuu anazaliwa anakuta Babu na Bibi zake wakutosha tuu tena wamepiga Age za maana.
Na wakati unakuta kop zengine mjukuu anazaliwa Kama atakuwa anabahati atakuta Babu au Bibi mmoja tuu ambaye ni Kati ya Babu Saba mpaka kumi waliomezwa na mauti. Tena Babu au Bibi mwenyewe hata miaka sabini haijui, Ni hawa Babu au Bibi Vijana.

Zipo koo ambazo watu wake hufa mapema hata kabla ya miaka sitini.

Kuishi miaka mingi ni baraka Kama Ilivyo baraka zingine.

Pia zipo familia zina Mkondo WA Mauti.
Ukioa au kuolewa nazo lazima uachwe mjane/mgane katika umri mdogo.

Unakuta umemuoa tuu mke wako, lakini kabla hamjafikisha hata miaka 40 Mkeo anakufa. Na kuacha watoto Yatima wa Mama.

Pia zipo familia ukiolewa nazo lazima mumeo afe kabla hajatimiza miaka 40.

Mambo haya hayatokei kibahati bahati, ni ishu zinazoenda na Mkondo.

Nafahamu Vijana wa siku hizi HAWAAMINI katika nature lakini hivyo ndivyo ilivyo.

Namna ya kuepuka na kujifuta katika Mkondo wa laana za mauti na kufikisha umri wako WA uzee uliopangiwa;

1. Jitakase na omba maombi ya kujitoa katika Mkondo WA mauti.

2. Tafuta mwenza mnayefanana Nyota/ubavu wako.

3. Takasa mwenza wako,jitakaseni pamoja na kuondoa laana za ukoo za Mkondo WA maiti.

4. Wajali na waheshimu wazazi wako iwe wakiwa hai au wakiwa wamekufa.
Kama wamekufa heshimu makazi Yao ambayo huitwa makaburi. Usiwatelekeze. Usije ukajidanganya mtu akifa ndio amekufa wakati ndiye aliyekuzaa.
Heshimu Baba na Mama yako iwe wakiwa hai au wamekufa.
Wakiwa hai wajali kwa kuwalisha vizuri, makazi mazuri, jitahidi hata Kama huna uwezo.

Wazazi hawakubariki upate riziki Ila wao wanauwezo wa kuongeza siku zako au kuzipunguza.

5. Jitakase kila mara karibu kila mwezi ikiwa wewe ni mlaji wa nyama.
Kila mwezi mwandamo jitakase na ondoa Mkondo WA mauti ikiwa kuna mnyama alikufa Kwa ajili ya wewe kumfanya chakula.

6. Lala masaa walau nane mpaka Tisa Kwa siku.
Kama hauoti ndoto jitakase ili walau Kwa siku uote ndoto moja.
Mtu asiyeota ndoto Nafsi yake IPO kizuizini au imekufa.

7. Kula chakula kingi ushibe.
Milo minne Kwa siku ukiwa na umri 20-34
Milo mitatu Kwa siku ukiwa na umri 35-45
Milo miwili Kwa siku ukiwa na umri 45- 65
Mlo mmoja Kwa siku ukiwa 66+
Kunywa maji mengi walau Lita tatu Kwa siku Kwa mwanaume mwenye umri kuanzia miaka 20.
Kwa mwanamke angalau Lita tatu.


Zingatia mambo ya kwanza zaidi kuliko haya ya chakula na mazoezi.
Unaweza Kula vizuri na ukafanya mazoezi lakini bado roho yako ikawa dhaifu kukabiliana na Mkondo WA mauti.

Taikon huwa naongea Kama naota lakini ndivyo ilivyo. Mwenye kusikia na asikie.
Hata hivyo wote tutakufa na Hilo hakuna anayeogopa lakini hofu kubwa ni kuondoka tukiwa hatujajiandaa na kifo chenyewe.

Unakufa ukiwa na deni Kwa watoto.
Unawaachaje watoto na wajukuu zako?
Umri mrefu unasaidia kiasi kukabiliana na matatizo na kuisaidia familia.

Mtu ukifa na miaka 40 ukaicha familia yako na watoto wadogo inauma na kutesa zaidi ya mtu aliyekufa akiwa na miaka 80+
Ambaye atakuwa kasaidia watoto ikiwezekana na wajukuu zake.

Matatizo la kuishi miaka mingi ni Kama ifuatavyo;

1. Kushuhudia vifo vya watu uwapendao Kama watoto au wajukuu walioshindwa kukabiliana na Mkondo WA Nauru.
Inasemakana inauma kumzika mtoto uliyemzaa.

2. Upweke.
Umri mrefu Kama miaka 80 utakabiliwa na upweke Mkuu. Wenye umri Kama wako watakuwa wachache au wasiwepo kabisa. Hii itakufa uishi Kama maiti.

3. Magonjwa na Huduma kuwa mbovu.
Magonjwa ya uzee ni sehemu ya changamoto kubwa Kwa Wazee.

4. Kutoa laana Kama hautakuwa makini.
Umri huu Kama hukujipanga ujanani ni rahisi kuwalaani watoto wako endapo watashindwa kukuhudumia.
Mara nyingi familia Masikini hujikuta katika wakati mgumu zikiwa na Wazee WA umri mkubwa.

Umri saa hii wa kufa ni upi?
Uzi unakuja sasa hivi.

Ni Yule Taikon Mtibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kuna mzee mmoja kaishi miaka 80 ila watoto wake wanne wakafa kabla ya Babu na bibi.wawili walikuwa wanywa gongo wazuri...
Asante Sana kwenye ishu ya chakula nimekubali ngoja nianze kula dona asubuhi na Milo minne na matunda ya kutosha maji lita nne nakubaliana na wewe..of course maada NI nzuri na ila 60%
 
Kuna mzee mmoja kaishi miaka 80 ila watoto wake wanne wakafa kabla ya Babu na bibi.wawili walikuwa wanywa gongo wazuri...
Asante Sana kwenye ishu ya chakula nimekubali ngoja nianze kula dona asubuhi na Milo minne na matunda ya kutosha maji lita nne nakubaliana na wewe..of course maada NI nzuri na ila 60%


Hapo kwenye Dona naomba ule zaidi vyakula vya protein na vitamin Kama mbogamboga na matunda.

Wanga Kula kidogo Sana.
Iwe ni wali, ugali,mandazi, chapati, mihogo, n.k.
 
💯 ukweli mtupu , babu amekufa akiwa na 96,Bibi 94 , Mzee anaelekea 80 ,

Hapo wewe kupiga 70 ni constant
Ukifa ni bahati mbaya tuu.
Lakini wengine kufika tu hamsini ni mbinde.
Unakuta ukoo mzima, mwenye umri mkubwa ati ana 65.

Hawa wengi wao wakijitahidi Sana ni 55-60 Ila wengi watapotea chini ya 50.
 
Taikon wa fasihi umefululiza sana machapisho hatimaye umeanza kuandika mada zisizo na ubunifu.

Yaani mambo ambayo ni ya kawaida kabisa na jamii inayafahamu ata sayansi imethibitisha habari ya vinasaba, mbona iko wazi.
 
Hapo kwenye Dona naomba ule zaidi vyakula vya protein na vitamin Kama mbogamboga na matunda.

Wanga Kula kidogo Sana.
Iwe ni wali, ugali,mandazi, chapati, mihogo, n.k.
Vipi kuhusu pombe na athari zake juu ya miaka ya kuishi.hasa TUnaokunywa pombe aina yoyote
 
Back
Top Bottom