Baada ya kuona hali inakuwa ngumu kila kukicha nimeamua kutangaza kuuza nyumba. Na wakati huu nimehamia hapa mbezi tangi bovu.
Mbezi kimara sitaki tena hata unipe kiwanja bure sijengi. Nilikata tamaa siku nilipotoka mwenge saa 11 jioni nikafika nyumbani saa sita usiku!!!!
Wachaga endeleeni kukaa huko na mkiendelea kupambana na laana hiyo.
Hapo kwenye bold naona unawatafuta maneno hawa jamaa zangu. ANYWAY.
Morogoro road ndio major road IN and OUT of Dar to almost all upcountry regions and neighbouring countries (Rwanda, Burundi, Congo, Kenya, Uganda, Zambia and Malawi). Hii ndio barabara inayobeba 99% ya malori na mabasi yote yaendayo mokoani na nchi za jirani.
Huwezi ukategemea barabara ya namna hiyo, hata ikiwa imekamilika ikawa sawa na barabara ya Mbagala ambayo ina DCM peke yake. Hii inatosaha kuonyesha kwamba Moro road haifai kutumiwa na watumiaji wa kawaida wa kila siku, ama wakitumia watapata kero ya malori na mabasi, ama wasitumie kabisa watafutiwe njia nyingine.
Lakini ujenzi unaoendelea, ambao huu lazima Magufuli na TANROAD wabebe lawama, umekuwa mradi wa kishenzi sana. Mradi usiojali environmental, social and economic impact kwa watumizi wengine wa barabara wala waishio pembezoni mwa barabara hiyo. Mradi hauna diversions wala nini, ukiingia pale Kimara kuelekea Ubungo, huwezi kuchepuka popote, mpaka ufike Ubungo, sawasawa na reli, Upuuzi mkubwa huu.
Kwa sasa, njia za kuchepuka kama Bahama mama to Chuo Kikuu, au Msewe to Chuo kikuu ni ndoto kupitika, kwasababu ukikaa kushoto kwa barabara, basi huwezi kuingia kulia, ukikaa kulia, huwezi kuingia kulia...TANROAD na Magufuli watueleze, huu ndio ujenzi wa aina gani.
:suspicious::suspicious::suspicious::suspicious:Ipo rushwa hapo...