Kuishi Duniani hakuhitaji Akili (Siri iliyojificha)

Huu uzi wakristo ndo watauelewa kdogo lakn wapagani sahau
Yah, ni wakristo ambao wamemfanya Mungu kuwa hana akili kuwapa wao akili.

Ila sisi wapagani ambao kitabu cha mwanzo kinatuambia binadamu alipoumbwa aliagizwa kutawala (mazingira, wanyama, ndege n.k) hatutaelewa.

Reff: mwanzo 1:26- na tumfanye mtu kwa mfano wetu, wakatawale....

Unatawalaje bila akili..!!!?? Wakati unavyovitawala vyenyewe (wanyama wa ardhini, majini, ndege n.k) vina akili.

Watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa.
 
Hakika umeifanya Jumapili yangu kuwa njema zaidi.

Nimefurahi kuona na kufahamu unavyoishi.
Nilivyosoma kichwa cha habari yako nilijua tu uliyoyaandika yatakuwa ndiyo niliyofikiria.

Hili somo tuliwahi kufundishwa Kanisani mwaka 2016.
Ni moja ya somo lililoniongoza vyema katika maisha ya imani yangu.

Ubarikiwe mtumishi kwa somo zuri.
 
Habari wakuu!

Bila shaka mada hii ni fikirishi sana hivyo nahitaji utulivu wako kwani utapata kitu muhimu katika maisha.

Ukitaka uishi vizuri bila shida yoyote hapa duniani basi usitumie akili yako. Huenda hujanielewa, ndio usitumie akili kabisa hapo ndipo utajua kuwa maisha ni matamu. Hilo nimeliona sana katika maisha yangu ya kawaida.

Turudi Edeni.
Edeni haikuhitajika akili yoyote ile isipokuwa ndio mkuu kama jeshini. Ijapokuwa kulikuwa na uhuru wa kusema hapana. Kilichohitajika pale edeni ni kusikia sauti ya Mungu Basi nakuitii. Suala la chakula, sijui mavazi sijui nini Jukumu hilo alilibeba Mungu mwenyewe. Kilichohitajika ni Adam na Hawa kutokula tunda basi.

Tuje kwenye maisha yetu:
Ili uishi katika dunia hii kama peponi basi sharti ni moja usitumie akili yako. Hii ndio kanuni namba moja. Ukitumia akili yako umeumia nakuhakikishia, utahangaika mpaka unakufa huna utakachokipata nafsi ikatulia. Utakuwa tajiri lakini utajiona masikini tuu. Utakuwa mashuhuri mbele za watu lakini utajiona duni. Utagangaika.

Ukitumia akili yako unaruhusu changamoto nyingi zikukabili. Unamruhusu roho hasi ishinde kwa urahisi kwani akili ya mwanadamu inamafungamano na roho hasi kwa kiasi kikubwa. Ukitumia akili unamfukuza Mungu na kujitukuza wewe mwenyewe na kujiona unajua kumbe hujui lolote.

Kuishi Duniani hakuhitaji akili yoyote isipokuwa kutii amri za Mungu. Maisha ya Dunia yapo kwa mfano huu:
Fikiria wewe ni mzazi unaweza kuwa Baba au Mama. Ukiwa na watoto wadogo nadhani unaona jinsi wanavyoishi. Hawahitaji akili kubwa kuendesha maisha yao zaidi ya kutii sheria zako wewe. Kama kusalimia, kusaidia kazi ndogo za nyumbani na kupumzika Basi.

Yesu alituambia huwezi kuurithi ufalme wa Mungu kama hutokuwa kama mtoto mdogo. Ndivyo maisha yalivyo. Lengo la Mungu si sisi kuhangaika na maisha bali kutii sheria zake na kuisikia sauti yake basi. Jinsi unavyotumia akili yako katika kutatua changamoto za maisha ndivyo unavyopoteza furaha yako kwa kiasi kikubwa. Inahitaji akili kunielewa lakini haihitaji akili kuishi duniani.

Siri hii imefichwa na inazidi kufichwa ili watu wataabike. Embu fikiria unaanzisha Mradi wa kuku, Unadhani kuku atahitaji akili gani kuishi kama si kukutegemea wewe.

Kuishi Duniani hakuhitaji akili yako bali utii wako kwa Mungu. Jaribu hii alafu nipe matokeo.

Kuna wale wamama wanauzaga vitu vyao vyote vya ndani na kuenda kukesha kwa mchungaji.........nimegundua wewe ndo mmoja wapo mnaishiaga kuwaMIMBA tu af mnawafukura huku mkiwaacha wamekuwa wapweke na kukimbiwa na familia zao kwa maamuzi mliyowaambukiza.
 
wewe umetumia nn? mpaka now upo na Hali Gani????
The Greater Man
Mafanikio si mpaka mtu awe na miradi kama Bakhresa, sote hatuwezi kuwa na mafanikio ya hivyo. Ni kuridhika na hali halisi tu.

Chukua mfano wa Adam na Eva, pale Eden hawakuwa na majukum makubwa lakini waliishi good life.

Alafu angalia maisha yao baada ya kumkosea Mungu.
 
Mungu alituumba na kutupatia akili kututofautisha na wanyama ili tuitawale dunia. Anzisha wewe mradi wa kuku na usihangaike nao uone matokeo yake.
 
Habari wakuu!

Bila shaka mada hii ni fikirishi sana hivyo nahitaji utulivu wako kwani utapata kitu muhimu katika maisha.

Ukitaka uishi vizuri bila shida yoyote hapa duniani basi usitumie akili yako. Huenda hujanielewa, ndio usitumie akili kabisa hapo ndipo utajua kuwa maisha ni matamu. Hilo nimeliona sana katika maisha yangu ya kawaida.

Turudi Edeni.
Edeni haikuhitajika akili yoyote ile isipokuwa ndio mkuu kama jeshini. Ijapokuwa kulikuwa na uhuru wa kusema hapana. Kilichohitajika pale edeni ni kusikia sauti ya Mungu Basi nakuitii. Suala la chakula, sijui mavazi sijui nini Jukumu hilo alilibeba Mungu mwenyewe. Kilichohitajika ni Adam na Hawa kutokula tunda basi.

Tuje kwenye maisha yetu:
Ili uishi katika dunia hii kama peponi basi sharti ni moja usitumie akili yako. Hii ndio kanuni namba moja. Ukitumia akili yako umeumia nakuhakikishia, utahangaika mpaka unakufa huna utakachokipata nafsi ikatulia. Utakuwa tajiri lakini utajiona masikini tuu. Utakuwa mashuhuri mbele za watu lakini utajiona duni. Utagangaika.

Ukitumia akili yako unaruhusu changamoto nyingi zikukabili. Unamruhusu roho hasi ishinde kwa urahisi kwani akili ya mwanadamu inamafungamano na roho hasi kwa kiasi kikubwa. Ukitumia akili unamfukuza Mungu na kujitukuza wewe mwenyewe na kujiona unajua kumbe hujui lolote.

Kuishi Duniani hakuhitaji akili yoyote isipokuwa kutii amri za Mungu. Maisha ya Dunia yapo kwa mfano huu:
Fikiria wewe ni mzazi unaweza kuwa Baba au Mama. Ukiwa na watoto wadogo nadhani unaona jinsi wanavyoishi. Hawahitaji akili kubwa kuendesha maisha yao zaidi ya kutii sheria zako wewe. Kama kusalimia, kusaidia kazi ndogo za nyumbani na kupumzika Basi.

Yesu alituambia huwezi kuurithi ufalme wa Mungu kama hutokuwa kama mtoto mdogo. Ndivyo maisha yalivyo. Lengo la Mungu si sisi kuhangaika na maisha bali kutii sheria zake na kuisikia sauti yake basi. Jinsi unavyotumia akili yako katika kutatua changamoto za maisha ndivyo unavyopoteza furaha yako kwa kiasi kikubwa. Inahitaji akili kunielewa lakini haihitaji akili kuishi duniani.

Siri hii imefichwa na inazidi kufichwa ili watu wataabike. Embu fikiria unaanzisha Mradi wa kuku, Unadhani kuku atahitaji akili gani kuishi kama si kukutegemea wewe.

Kuishi Duniani hakuhitaji akili yako bali utii wako kwa Mungu. Jaribu hii alafu nipe matokeo.
Kuna wakati huwa najiuliza "hivi biblia yangu ina kasoro nini"

Mfano maarufu ni pale alipoagizwa mwanaume kuishi kwa akili. Huku tena jamaa anasema duniani hakuna kutumia akili.

Mithali 22:15 UJINGA umefungwa ndani ya moyo wa mtoto lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.

Mith 27:3 jiwe ni zito na mchanga hulemea, lakini ghadhabu ya MPUMBAVU ni nzito kuliko hivi vyote
 
Kwa hiyo maisha yako kuwa mazuri ndio kujali kwa mungu huko " vipi kuhusu wanaokufa kwa njaa somalia " Unalizungumziaje hilo na huyo mungu wako !?

Mkuu sijasema naishi maisha mazuri. Nimekuambia tukutane then utaona mwenyewe
 
Yah, ni wakristo ambao wamemfanya Mungu kuwa hana akili kuwapa wao akili.

Ila sisi wapagani ambao kitabu cha mwanzo kinatuambia binadamu alipoumbwa aliagizwa kutawala (mazingira, wanyama, ndege n.k) hatutaelewa.

Reff: mwanzo 1:26- na tumfanye mtu kwa mfano wetu, wakatawale....

Unatawalaje bila akili..!!!?? Wakati unavyovitawala vyenyewe (wanyama wa ardhini, majini, ndege n.k) vina akili.

Watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa.

Kumcha Bwana ni chanzo cha Akili. Mbona mada ipo uchi kabisa. Usichoelewa ni nini Mkuu
 
Hakika umeifanya Jumapili yangu kuwa njema zaidi.

Nimefurahi kuona na kufahamu unavyoishi.
Nilivyosoma kichwa cha habari yako nilijua tu uliyoyaandika yatakuwa ndiyo niliyofikiria.

Hili somo tuliwahi kufundishwa Kanisani mwaka 2016.
Ni moja ya somo lililoniongoza vyema katika maisha ya imani yangu.

Ubarikiwe mtumishi kwa somo zuri.

Hhahah!! Nimecheka ulivyoniita Mtumishi. Ahsante sana
 
Falsafa iko mbinguni? Au ni huku duniani ambako hakuhitaji akili? Nyinyi wenye akili kubwa ni zanini hizo, maana hapa duniani c ndo akili haitakiwi, au?

Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa
 
Kuna wale wamama wanauzaga vitu vyao vyote vya ndani na kuenda kukesha kwa mchungaji.........nimegundua wewe ndo mmoja wapo mnaishiaga kuwaMIMBA tu af mnawafukura huku mkiwaacha wamekuwa wapweke na kukimbiwa na familia zao kwa maamuzi mliyowaambukiza.

Hahahah! Mkuu hao wamama wanatumia akili ndio maana wanafanya hayo. Mungu anasemaje kuhusu jambo hilo
 
Mungu alituumba na kutupatia akili kututofautisha na wanyama ili tuitawale dunia. Anzisha wewe mradi wa kuku na usihangaike nao uone matokeo yake.

Anzisha mradi afu tumia akili zako uone utafika popote. Bila Mungu huna utakachofanya Mkuu
 
Kuna wakati huwa najiuliza "hivi biblia yangu ina kasoro nini"

Mfano maarufu ni pale alipoagizwa mwanaume kuishi kwa akili. Huku tena jamaa anasema duniani hakuna kutumia akili.

Mithali 22:15 UJINGA umefungwa ndani ya moyo wa mtoto lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.

Mith 27:3 jiwe ni zito na mchanga hulemea, lakini ghadhabu ya MPUMBAVU ni nzito kuliko hivi vyote

Akili ya mwanadamu kwa Mungu ni upumbavu. Bila Mungu huwezi fanya lolote. Kumcha Bwana ni chanzo cha akili. Sasa umeelewa watu hupaswa kufanya nini ili waishi vyema duniani
 
Kumcha Bwana ni chanzo cha Akili. Mbona mada ipo uchi kabisa. Usichoelewa ni nini Mkuu
Labda najaribu kutotumia akili ndomana sielewi, ila nikitumia akili naona umeiripotisha kwa namna potoshi kdogo ambapo najua lengo ni kutaka binadamu asizitegemee akili zake (hii ni tofauti na kuto kuzitumia).

Tumtegemee Mungu (tusitegemee akili zetu).
 
Inaitaji uwe nje ya box ndio umuekewa mleta mada

Pia inahitaji uwe na uzoefu wa maisha ndipo uielewe mada. Watu wazima wengi watanielewa lakini sijategemea vijana wa umri chini ya 35
 
Labda najaribu kutotumia akili ndomana sielewi, ila nikitumia akili naona umeiripotisha kwa namna potoshi kdogo ambapo najua lengo ni kutaka binadamu asizitegemee akili zake (hii ni tofauti na kuto kuzitumia).

Tumtegemee Mungu (tusitegemee akili zetu).

Kutozitegemea unajua maana yake? Yaani si lolote wala si chochote.
 
Back
Top Bottom