Kuishi Duniani hakuhitaji Akili (Siri iliyojificha)

Kuishi Duniani hakuhitaji Akili (Siri iliyojificha)

ili umuelewe mtoa mada inabidi ufikilie kiundani zaid na sio juu juu tu kamwe hautamuelewa.

mtoa mada ili somo lako lieleweke zaidi jaribu kutumia neno lingine badala ya akili huwenda watakuelewa.


Wachache wataelewa
 
Nimekuelewa sana mleta mada


Mtu akishakuwa mtu mzima huanza kuelewa mambo ya msingi katika maisha.

Nafahamu kwa uzoefu wako ni kuwa yale mambo uliyotumia akili nyingi ndio ulifeli na yale ambayo hata hukutumia akili wala kupanga ndio mengi yamefanikiwa
 
Sawa we lala kutwa nzima utii amri za mungu usipo geuka amba rutty


Unaoenekana umri mdogo na umemaliza chuo juzi. Kaa kitaa utaelewa mada hii vizuri. Kila unapotumia nguvu na akili zako ndipo unapopotea katika ramani ya maisha. Amini usiamini.

Dunia hii ni Mungu au shetani. Ukiwa neutral lazima uteteseke
 
Umetolea mfano wa kuku hapo juu..ukasema hawatumiaa akili basi wanakutegema wewe, ukaweka mfano wa watoto pia (ukiwa mzazi) ukasema nao hawatumii akili wanafata amri zako! Sasa mkuu mbona hujasema sisi (wafuga kuku/wazazi) tusitumie akili tumfate nani??
Na je,kuhusu hao wanaotutegemea na kufata akili zetu (kuku/watoto) huoni kuwa wanafanya hivyo kwa sababu sisi tuna akili zaidi labda kuliko wao? sasa unataka na sisi tuache kutumia akili zetu hao wanaoishi kwa kutegemea akili zetu wataishije tena?


Umewaza vyema Mkuu. Mtegemee Mungu hutojuta Maisha yako yote. Maisha ni uji ukimtegemea Mungu. Utakapo tumia akili yako ndio mwanzo wa kuthibitisha ugumu wa maisha. Bila akili huwezi nielewa lakini usitumie akili kwenye maisha. Tumia akili kujifunza tabia ya Mungu ambayo hudhihirishwa na sheria zake
 
Kwa hiyo tuwe mazwazwa??


Ukitumia akili kumjua Mungu huwezi kuwa zwazwa lakini ukitumia akili kuijua dunia lazima utakuwa zwazwa. Angalia wote wanaopinga sheria za Mungu na uwepo wake. Angalia maisha yao utaelewa nazungumzia nini.
 
Tatizo kachanganya imani na maisha
Amri kumi za mungu hazitoi ugali usipotumia akili ugali utapataje?


Akili haikupi ugali bali kushika sheria za Mungu ndio kunakupa ugali na maisha mazuri. Sheria haihitaji utumie akili bali inahitaji utii tuu basi nenda jeshini utaelewa
 
Kuishi bila kutumia akili labda uwe tegemezi wa kutupwa.
Maandiko hayohayo yanasema asiyefanya kazi na asile.

Kijana! Kama unamwamini Mungu wako, basi fanya kazi huku ukimwimbia Mungu moyoni mwako

Je, waweza kufanya kazi pasipo kutumia akili? Wewe mleta mada hela ya kuweka bando na kununulia simu ulihongwa?

Kwahiyo tukubali wewe ni tegemezi kwa ndugu zako, jamaa na marafiki sio?

Hebu tuambie mwenzetu wewe unaishije hapa mjini bila kipato [emoji23]

KWANZA UNA FAMILIA?

Unajua hizi dini zimewaharibu akili sana


Huwezi elewa kwa ubongo wa Mende.

Huenda unauelewa mdogo kuhusu maisha. Maisha yanahitaji utii kuliko akili. Ninaposema utii tayari nimezungumzia sheria, amri na maagizo. Mungu ndiye aliyeweka sheria mama ambazo mwanadamu anapaswa kuzifuata pasipo kutumia akili yake.

Kufanya kazi ni sehemu ya utii wa sheria za Mungu na za nchi.

Tukija kwenye ishu ya mambo yangu binafsi. Maana naona umeniuliza maswali, sijui nina familia, naishije hapa mjini, na mambo kadha wa kadha.

Ndio nina familia ya mke na mtoto mmoja.
Ninafanya kazi inayoniingizia kipato.
Nina elimu ya kidunia ambayo bila shaka kwenye ukoo wenu wote hakuna aliyeipata.
Kwa elimu ya kidini ndio usiguse kabisa.

Siku nyingine ujadili mada na si kutaka taarifa za watu ambazo hazitakusaidia kitu
 
Mi naamini mtoa mada ana ujumbe mzuri na sahihi kabisa,ila maneno aliyoyatumia yanawa mis-lead baadhi ya watu.

"Kuisikiliza sauti ya Mungu ni salama zaidi kuliko logic"


Mkuu wachache wataelewa ila wengi hawataelewa. Na wengi wasioelewa ni wale wanaojitia wamesoma na wanatafuta maisha. Wengi ni wale wenye ndoto kubwa lakini kuna umri wataelewa kuwa maisha sivyo wadhaniavyo
 
Back
Top Bottom