Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,336
- 10,910
Habari wakuu!
Bila shaka mada hii ni fikirishi sana hivyo nahitaji utulivu wako kwani utapata kitu muhimu katika maisha.
Ukitaka uishi vizuri bila shida yoyote hapa duniani basi usitumie akili yako. Huenda hujanielewa, ndio usitumie akili kabisa hapo ndipo utajua kuwa maisha ni matamu. Hilo nimeliona sana katika maisha yangu ya kawaida.
Turudi Edeni.
Edeni haikuhitajika akili yoyote ile isipokuwa ndio mkuu kama jeshini. Ijapokuwa kulikuwa na uhuru wa kusema hapana. Kilichohitajika pale edeni ni kusikia sauti ya Mungu Basi nakuitii. Suala la chakula, sijui mavazi sijui nini Jukumu hilo alilibeba Mungu mwenyewe. Kilichohitajika ni Adam na Hawa kutokula tunda basi.
Tuje kwenye maisha yetu:
Ili uishi katika dunia hii kama peponi basi sharti ni moja usitumie akili yako. Hii ndio kanuni namba moja. Ukitumia akili yako umeumia nakuhakikishia, utahangaika mpaka unakufa huna utakachokipata nafsi ikatulia. Utakuwa tajiri lakini utajiona masikini tuu. Utakuwa mashuhuri mbele za watu lakini utajiona duni. Utagangaika.
Ukitumia akili yako unaruhusu changamoto nyingi zikukabili. Unamruhusu roho hasi ishinde kwa urahisi kwani akili ya mwanadamu inamafungamano na roho hasi kwa kiasi kikubwa. Ukitumia akili unamfukuza Mungu na kujitukuza wewe mwenyewe na kujiona unajua kumbe hujui lolote.
Kuishi Duniani hakuhitaji akili yoyote isipokuwa kutii amri za Mungu. Maisha ya Dunia yapo kwa mfano huu:
Fikiria wewe ni mzazi unaweza kuwa Baba au Mama. Ukiwa na watoto wadogo nadhani unaona jinsi wanavyoishi. Hawahitaji akili kubwa kuendesha maisha yao zaidi ya kutii sheria zako wewe. Kama kusalimia, kusaidia kazi ndogo za nyumbani na kupumzika Basi.
Yesu alituambia huwezi kuurithi ufalme wa Mungu kama hutokuwa kama mtoto mdogo. Ndivyo maisha yalivyo. Lengo la Mungu si sisi kuhangaika na maisha bali kutii sheria zake na kuisikia sauti yake basi. Jinsi unavyotumia akili yako katika kutatua changamoto za maisha ndivyo unavyopoteza furaha yako kwa kiasi kikubwa. Inahitaji akili kunielewa lakini haihitaji akili kuishi duniani.
Siri hii imefichwa na inazidi kufichwa ili watu wataabike. Embu fikiria unaanzisha Mradi wa kuku, Unadhani kuku atahitaji akili gani kuishi kama si kukutegemea wewe.
Kuishi Duniani hakuhitaji akili yako bali utii wako kwa Mungu. Jaribu hii alafu nipe matokeo.