Brian Spilner
JF-Expert Member
- Aug 7, 2016
- 2,240
- 6,482
Nje ya box ndo nje ya dunia? Maana hapa duniani c ndo akili(hata hiyo yakuelewa) haihitajikiInaitaji uwe nje ya box ndio umuekewa mleta mada
Nje ya box ndo nje ya dunia? Maana hapa duniani c ndo akili(hata hiyo yakuelewa) haihitajikiInaitaji uwe nje ya box ndio umuekewa mleta mada
Labda najaribu kutotumia akili ndomana sielewi, ila nikitumia akili naona umeiripotisha kwa namna potoshi kdogo ambapo najua lengo ni kutaka binadamu asizitegemee akili zake (hii ni tofauti na kuto kuzitumia).
Tumtegemee Mungu (tusitegemee akili zetu).
Hivi mkuu, ni kweli kwamba Mungu alituumba na hizi akili kuwa luxury? Au zitakuja zitumike mbinguni?Kutozitegemea unajua maana yake? Yaani si lolote wala si chochote.
Hata biblia haijakanusha matumizi ya akili (as a matter of fact imehamasisha). Ila imekataza kuitegemea, maana akili ni zetu (ila Mungu nae hutusaidia kupitia hizo hizo).Ukimtegemea Mungu huwezi tumia akili yako. Mbona simple sana. Ukitumia akili zako ni wazi humtegemei Mungu.
tukutane wapi tena " Nyie vijana wa DAB ndio mitego yenu hii huwaga mnaanza hivi hivi" mwisho wa siku twasikia maiti imeokotwa mtoni ikieleaMkuu sijasema naishi maisha mazuri. Nimekuambia tukutane then utaona mwenyewe
Vip mkuu, Jemmy alisharudi kutoka kwa Tirampu au ulioa mwingine?Nina mtoto mmoja Mkuu. Karibu sana
Ndiyo hivyo mkuu, wengi binadamu hata bibilia hawasomi , hawajui vile mungu hupenda binadamu aishi, na vile umesema ni kweli wakipata matatizo mungu wanamulaumu, ila hali ni wao hawapendi kusoma na kutii mungu na neno lake, barikiwa sanaMkuu wengi hawezi elewa kwani wanadhani mafanikio wayapatayo ni matokeo ya akili zao lakini mabaya yakiwakumba humshtaki Mungu. Ndivyo akili ya mpumbavu ifanyavyo kazi
Hata biblia haijakanusha matumizi ya akili (as a matter of fact imehamasisha). Ila imekataza kuitegemea, maana akili ni zetu (ila Mungu nae hutusaidia kupitia hizo hizo).
Tunapozitegemea akili zetu tunaamini ni sisi tumefanya, ila tunapomtegemea Mungu tunajua ametenda kwa kutupa namna yakutumia akili (alizotuumba nazo) katika kufanya tuyafanyayo.
Kama hapa napo hujaelewa basi ni kweli wewe hutumii akili duniani. Zitunze zitakusaidia mbinguni hizo.
Umetoa ujumbe mzito lakini kwa vijana wa kisasa kwao si kitu,mawazo yao bado si komavu kuweza kuyaona yaliyomo ndani yake.Uwe na amani siku zote.
Ila waamini kuwa akiri za mwanadamu si kitu mbele za mweyezi Mungu.Yatupasa kujikana wenyewe na kumurudia muumba wetu.Pasipo kutegemea elimu zetu,kazi zetu ama vyeo vyetu ndo tutapata furaha katika maisha yetu,tena ni furaha idumuyo.
Sheria ya Mungu na kanuni zake ni nzuri na zinajitosheleza.Hii inafaa ieleweke kwa wale wenye imani na wanao tambua uwepo wa Muumba wetu,si kwa wapagani.
Hakuna kitu kizuri duniani kama kuishi katika misingi na kiimani na kumucha mwenyezi Mungu.mambo mengi tunayakosa kwa ajiri ya kutegemea akiri zetu binafsi.
Mkuu una bonge la ujumbe ila nakukosoa kwenye uwasilishaji, nafikiri lengo lako kuu ni kutaka kutuambia tumtegemee Mungu na kumtii yeye kwa kila jambo, ni kweli kabisa, so nafikiri ungesema tusizitegemee akili zetu bali tutegemee mwongozo wa Mungu katika maisha yetu, means kwamba akili zetu ziendeshwe na mapenzi ya Mungu, kwahiyo kwa kila tutakachokifanya basi lazima kiwe katika mapenzi ya Mungu.
hahaa hujaniteka kiboya badoHahahah!! Mkuu acha hizo. Njoo tuu usiogope. Nipo Sinza Kwaremi Mkuu
Habari wakuu!
Bila shaka mada hii ni fikirishi sana hivyo nahitaji utulivu wako kwani utapata kitu muhimu katika maisha.
Ukitaka uishi vizuri bila shida yoyote hapa duniani basi usitumie akili yako. Huenda hujanielewa, ndio usitumie akili kabisa hapo ndipo utajua kuwa maisha ni matamu. Hilo nimeliona sana katika maisha yangu ya kawaida.
Turudi Edeni.
Edeni haikuhitajika akili yoyote ile isipokuwa ndio mkuu kama jeshini. Ijapokuwa kulikuwa na uhuru wa kusema hapana. Kilichohitajika pale edeni ni kusikia sauti ya Mungu Basi nakuitii. Suala la chakula, sijui mavazi sijui nini Jukumu hilo alilibeba Mungu mwenyewe. Kilichohitajika ni Adam na Hawa kutokula tunda basi.
Tuje kwenye maisha yetu:
Ili uishi katika dunia hii kama peponi basi sharti ni moja usitumie akili yako. Hii ndio kanuni namba moja. Ukitumia akili yako umeumia nakuhakikishia, utahangaika mpaka unakufa huna utakachokipata nafsi ikatulia. Utakuwa tajiri lakini utajiona masikini tuu. Utakuwa mashuhuri mbele za watu lakini utajiona duni. Utagangaika.
Ukitumia akili yako unaruhusu changamoto nyingi zikukabili. Unamruhusu roho hasi ishinde kwa urahisi kwani akili ya mwanadamu inamafungamano na roho hasi kwa kiasi kikubwa. Ukitumia akili unamfukuza Mungu na kujitukuza wewe mwenyewe na kujiona unajua kumbe hujui lolote.
Kuishi Duniani hakuhitaji akili yoyote isipokuwa kutii amri za Mungu. Maisha ya Dunia yapo kwa mfano huu:
Fikiria wewe ni mzazi unaweza kuwa Baba au Mama. Ukiwa na watoto wadogo nadhani unaona jinsi wanavyoishi. Hawahitaji akili kubwa kuendesha maisha yao zaidi ya kutii sheria zako wewe. Kama kusalimia, kusaidia kazi ndogo za nyumbani na kupumzika Basi.
Yesu alituambia huwezi kuurithi ufalme wa Mungu kama hutokuwa kama mtoto mdogo. Ndivyo maisha yalivyo. Lengo la Mungu si sisi kuhangaika na maisha bali kutii sheria zake na kuisikia sauti yake basi. Jinsi unavyotumia akili yako katika kutatua changamoto za maisha ndivyo unavyopoteza furaha yako kwa kiasi kikubwa. Inahitaji akili kunielewa lakini haihitaji akili kuishi duniani.
Siri hii imefichwa na inazidi kufichwa ili watu wataabike. Embu fikiria unaanzisha Mradi wa kuku, Unadhani kuku atahitaji akili gani kuishi kama si kukutegemea wewe.
Kuishi Duniani hakuhitaji akili yako bali utii wako kwa Mungu. Jaribu hii alafu nipe matokeo.