Ralphryder
JF-Expert Member
- Nov 16, 2011
- 5,599
- 1,798
Chadema ni watu wa
ajabu sana. Kwa wasioijua hebu tafakari!!
1. Wako tayari hata kuua ili waingie ikulu. Kumetokea vifo vingi vya
vijana wetu wakiwa mikononi mwao au ktk mazingira ambayo yanatiliwa
shaka kama walikuwa na dhamira ya dhati ya kuleta amani. Mfano mauaji ya
kijana wa Morogoro ktk maandamano yao ilihali maandamano yalizuiwa.,
mauaji ya Chacha Wangwe ni mfano wa nyongeza.
2. Viongozi wa CHADEMA wameifanya CHADEMA kama SUCCOS yao. Mfano Dr.
Slaa(babu) kukwapua viroba vya manoti na kujikopesha. Sidhani kama
Chadema wamegeuza maudhui ya Chama chao kuwa SUCCOS.
3. Chadema imegeuka ni kama "vikundi vya kusaidiana". Kwa wasiojua
vizuri kule uchagani kuna vikundi vya kusaidiana wakati wa shida ktk
ukoo. Chadema wameamua kuigeuza Chadema kama KIKUNDI CHA KUSAIDIANA
kwani hata "population ya wanachama, wabunge wa viti maalumu na wa
kuchaguliwa" inatia shaka. Na wengine wameamua kuleta WAKE ZAO ili
kusaidiana kula pesa ya chama.
4. Hakuna demokrasia ya kutosha. Chadema imekuwa na kawaida ya kufukuza
wanachama wake pale "wakubwa" wanapohisi watu hao wanahatarisha amani na
uhai wao wa ndani ya chama.
5. Chadema ni wanafiki. Walitangaza kuwa hawatopokea posho lakini
wakaendelea na wanaendelea kupokea na kula posho hadi kesho. Na Mbowe
alitangaza kuwa hatochukua gari la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani
lakini alichukua na anatanua nalo.
6. Walitangaza kuwa hawamtambui Mh. Kikwete kama rais lakini sote
tukiona jinsi Mbowe alivyokuwa anammwagia sifa rais Kikwete pale
alipotembelea HAI jimboni kwake. Na si ndo yeye aliyeongoza wenzake
"kwenda IKULU kwenda kukutana na rais Kikwete". Walinusa kaubaridi ka
pale "kwetu" huku wakifurahia na kujichekelea JUISI ya ukwaju.
7. Wanamtega na kupinga chini chini ili tu "mtu wao asije akakosa
nafasi ya kugombea urais, au isije akagombea tena uenyekiti". Si ndo
Zitto Kabwe "aliyeombwa" na akina mtei aondoe jina lake ktk
kinyang'anyiro cha uenyekiti ili "mkwe" wake apite bila kupingwa?
Je kwa haya machache unaweza kulazimika kuipenda CHADEMA? Kwa lipi jema?
Kupayuka kwenye majukwaa? Kuleta vurugu? Kuonesha ukanda na kugawa
kanda?
Nimeng'amua!!!
CHAGADEMAAAAAAA! hao ndio eti wanataka kutawala nchi! bora waumbuke!