Chadema ni watu wa ajabu sana. Kwa wasioijua hebu tafakari!!
1. Wako tayari hata kuua ili waingie ikulu. Kumetokea vifo vingi vya vijana wetu wakiwa mikononi mwao au ktk mazingira ambayo yanatiliwa shaka kama walikuwa na dhamira ya dhati ya kuleta amani. Mfano mauaji ya kijana wa Morogoro ktk maandamano yao ilihali maandamano yalizuiwa., mauaji ya Chacha Wangwe ni mfano wa nyongeza.
2. Viongozi wa CHADEMA wameifanya CHADEMA kama SUCCOS yao. Mfano Dr. Slaa(babu) kukwapua viroba vya manoti na kujikopesha. Sidhani kama Chadema wamegeuza maudhui ya Chama chao kuwa SUCCOS.
3. Chadema imegeuka ni kama "vikundi vya kusaidiana". Kwa wasiojua vizuri kule uchagani kuna vikundi vya kusaidiana wakati wa shida ktk ukoo. Chadema wameamua kuigeuza Chadema kama KIKUNDI CHA KUSAIDIANA kwani hata "population ya wanachama, wabunge wa viti maalumu na wa kuchaguliwa" inatia shaka. Na wengine wameamua kuleta WAKE ZAO ili kusaidiana kula pesa ya chama.
4. Hakuna demokrasia ya kutosha. Chadema imekuwa na kawaida ya kufukuza wanachama wake pale "wakubwa" wanapohisi watu hao wanahatarisha amani na uhai wao wa ndani ya chama.
5. Chadema ni wanafiki. Walitangaza kuwa hawatopokea posho lakini wakaendelea na wanaendelea kupokea na kula posho hadi kesho. Na Mbowe alitangaza kuwa hatochukua gari la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani lakini alichukua na anatanua nalo.
6. Walitangaza kuwa hawamtambui Mh. Kikwete kama rais lakini sote tukiona jinsi Mbowe alivyokuwa anammwagia sifa rais Kikwete pale alipotembelea HAI jimboni kwake. Na si ndo yeye aliyeongoza wenzake "kwenda IKULU kwenda kukutana na rais Kikwete". Walinusa kaubaridi ka pale "kwetu" huku wakifurahia na kujichekelea JUISI ya ukwaju.
7. Wanamtega na kupinga chini chini ili tu "mtu wao asije akakosa nafasi ya kugombea urais, au isije akagombea tena uenyekiti". Si ndo Zitto Kabwe "aliyeombwa" na akina mtei aondoe jina lake ktk kinyang'anyiro cha uenyekiti ili "mkwe" wake apite bila kupingwa?
Je kwa haya machache unaweza kulazimika kuipenda CHADEMA? Kwa lipi jema? Kupayuka kwenye majukwaa? Kuleta vurugu? Kuonesha ukanda na kugawa kanda?
Nimeng'amua!!!