Kuirudisha CCM madarakani ni maafa ~ Dr Slaa

napenda niwarejeshe kipindi cha kampen tulimsikia Dr slaa akisema kuichagua ccm kuongoza nch ni maafa, nilijua maafa yatatokana na uchumi kuwa mbaya au gharama za maisha kupanda kama tunavyoona hivi sasa, yote hayo ni indirect way hili la gongo la mboto lipo direct zaidi, je Dr slaa alijua mabomu yatalipuka na kuwa maafa?

Jino kwa Jino, sikio la kufa halisikii dawa ndugu yangu, maafa tumeyataka wenyewe, tulipewa nafasi ya kuyaepuka hatukuitumia vizuri, tukadanganywa na fulana na kofia, tukaruhusu wakachakachua na hii leo tunajionea kwa macho.
Mungu zilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amina.
 
Jino kwa Jino, sikio la kufa halisikii dawa ndugu yangu, maafa tumeyataka wenyewe, tulipewa nafasi ya kuyaepuka hatukuitumia vizuri, tukadanganywa na fulana na kofia, tukaruhusu wakachakachua na hii leo tunajionea kwa macho.
Mungu zilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amina.

kosa si kosa bali kurudia kosa ni kosa, MAISHA YANAZIDI KUWA MAGUMU SAMA KADRI SIKU ZINAVYOZIDI KWENDA
 
napenda niwarejeshe kipindi cha kampen tulimsikia Dr slaa akisema kuichagua ccm kuongoza nch ni maafa, nilijua maafa yatatokana na uchumi kuwa mbaya au gharama za maisha kupanda kama tunavyoona hivi sasa, yote hayo ni indirect way hili la gongo la mboto lipo direct zaidi, je Dr slaa alijua mabomu yatalipuka na kuwa maafa?[/QU

Kama alijua atakuwa alifanya makosa kutotuambia maake maafa haya ni makubwa.Je! amefurahishwa na vifo vya watu?Acha propaganda tuelekeze constructive ideas kwenye tukio na baada ya investigation huru hapo ndo tutarudi kwenye politics kujadili UCCM na UCHADEMA.
 
Angekuwa Slaa mabomu yasingelipuka au kama yangelipuka tungesema CCM wanahujumu serikali

Nimewasoma fanatics sijui lunatics wa CHADEMA
 
MAAFA YA GONGO LA MBOTO: WAZIRI WA ULINZI NA MKUU WA MAJESHI WAJIBIKE!

TAARIFA KWA UMMA
DODOMA, FEBRUARI 17, 2011

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeeleza kushtushwa na kusikitishwa na taarifa za milipuko ya mabomu katika Ghala la Kuhifadhi Silaha la Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana jioni.

Aidha, kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Tanzania kwa sababu ya maafa haya. Pia Kambi hiyo imezitaka mamlaka zote za umma zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi wote walioathirika na maafa haya wanapatiwa huduma zote wanazohitaji katika kipindi hiki cha msiba huu.

Hii ni pamoja na kuwapatia huduma za maziko wale wote waliofariki, matibabu kwa waliojeruhiwa na hifadhi kwa wale waliopoteza makazi yao. Aidha, ni muhimu kwa vyombo vya usalama kuhakikisha ulinzi wa mali za wananchi katika maeneo yote yaliyoathirika na ambazo zitakuwa hazina ulinzi baada ya wananchi kukimbia maeneo yao.

Taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kwamba tukio hili ni la kushtusha na kusikitisha hasa kwa kuzingatia kwamba haijapita miaka miwili tangu tukio la aina hiyo hiyo litokee katika Ghala ya Silaha ya Kambi nyingine ya JWTZ katika eneo la Mbagala, Dar es Salaam, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu thelathini na uharibifu mkubwa wa mali za umma na za wananchi binafsi. Aidha, milipuko ya Mbagala ilipelekea Serikali kutumia mabilioni ya fedha za umma kwa ajili ya malipo ya fidia kutokana na vifo, majeruhi na uharibifu wa mali binafsi za wananchi.

Akielezea tukio la milipuko ya Gongo la Mboto, Msemaji wa Ulinzi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Joseph Selasini alisema: "Milipuko ya Gongo la Mboto inaonyesha dhahiri kwamba Serikali ya Awamu ya Nne ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haijajifunza lolote kutokana na maafa yaliyotokea Mbagala mwaka juzi. Maana kama Serikali ingejifunza kutokana na maafa hayo ingeshachukua hatua za dharura na za haraka kuhakikisha kwamba maafa ya aina hii hayatokei tena." Mh. Selasini alizitaja baadhi ya hatua hizo kama ni pamoja na kuhamisha maghala yote ya silaha na mabomu yaliyo karibu na maeneo wanayoishi raia na kuyapeleka katika Kambi za JWTZ zilizoko mbali kabisa na maeneo ya raia. "Haiwezekani kwa Serikali kuendelea kuweka maghala ya silaha katika Kambi za Jeshi zilizo karibu na wananchi na hivyo kuhatarisha maisha yao namna hii", alisema Mh. Selasini.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewataka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kujiuzulu mara moja ili kuwajibika kisiasa kutokana na maafa ya Gongo la Mboto na ili kupisha uchunguzi huru na wa kina wa chanzo na/au sababu za milipuko hiyo. Mh. Selasini alisema: "Dr. Hussein Mwinyi alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati wa maafa ya Mbagala; na Jenerali Mwamunyange alikuwa Mkuu wa Majeshi. Maafa ya Mbagala yalitokea chini ya dhamana na/au usimamizi wao. Na mara baada ya maafa hayo, Waziri Mwinyi na Jenerali Mwamunyange waliliahidi taifa kwamba maafa ya aina hii hayatatokea tena. Sasa yametokea. Inaelekea, kwa hiyo, kwamba ahadi yao ilikuwa sio ya kweli na/au hawakuhakikisha kwamba inafanyiwa kazi ili iwe ya kweli. Viongozi hawa hawana budi kuwajibika kwa hiari yao wenyewe au kuwajibishwa kama itahitajika."

Mh. Selasini aliongeza kusema kwamba hadi leo hakuna taarifa yoyote rasmi iliyowahi kutolewa hadharani kwa wananchi na/au kwa wawakilishi wao Bungeni ya chanzo na/au sababu za maafa hayo. "Hadi leo hii wananchi na/au wawakilishi wao Bungeni hawajaambiwa kama kulikuwa na makosa ya makusudi na/au ya uzembe na/au kama hatua zozote za kinidhamu na/au za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya mtu yeyote kutokana na kusababisha na/au kuwajibika kwa maafa hayo. Jana maafa mengine ya aina hiyo hiyo yametokea tena na kwa kadri ya taarifa rasmi ya Serikali watu wengi wameuawa na wengi wengine kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa. Kwa sababu hizo, huu ni wakati muafaka kwa Dr. Mwinyi na Jenerali Mwamunyange kuonyesha uadilifu wao kwa kujiuzulu nafasi zao ili kuwajibika kwa maafa haya."

Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imependekeza iundwe Tume Huru ya Uchunguzi na/au Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchunguza kwa kina chanzo, sababu na madhara yote yaliyosababishwa na milipuko ya Gongo la Mboto. "Kwa kuzingatia historia ya uchunguzi wa milipuko iliyotokea Mbagala mwezi Aprili 2009, Tume Huru na/au Kamati Teule ya Bunge lazima itoe taarifa yake hadharani kwa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", alishauri Mh. Selasini.
 
Baada ya gadhabu yote hii ya Mungu hakuna aliyewajibika wala kuwajibishwa?tutegemee kichapo kingine kutoka kwa Mungu. bado niponiposana. wazushi watasema uchuro.poa tu nshakata tamaa mie.afadhali mabomu yatulipukie kuliko kutawaliwa na viongozi wala rushwa wasio na huruma.
 
Asilimia 85 ya Watanzania na hasa wale wanaoishabikia na kuichagua CCM wanaishi katika taabu, shaka na maisha magumu kuliko raia wowote wa nchi yetu hii ambayo Mungu amaibariki kuwa na kila aina ya neema. Ila tu wananchi wanashindwa kufikiria, au wanakuwa wavivu kufikiria na kuamua ili wawapate viongozi makini na wenye uchungu.

Ikichukua mfano mdogo wa Majimbo yaliyo chini ya Vyama ambayo havina Serikali kwa sasa mfano Karatu na Moshi Mjini, Tarime (Chadema), na Bariadi (UDP) nk, utagundua kuwa wananchi wengi wana ufahamu mkubwa na wamejikwamiua sana kimaendeleo, mfano jimbo la Karatu pekee, wananchi karibu kila kona wana huduma za maji safi, afya, barabara, shule za hali ya juu achilia mbali vitega uchumi na kipato bora.

Ukichukua Jimbo lolote la Wilaya ya Bagamoyo; and Mkoa wa Pwani - ambako ndio Kikwete amekuwa Mbunge kwa Miaka zaidi ya 20, utapata picha halisi ya ni kwa nini kuichagua tena CCM na JK ni maafa kwa taifa. Shule hakuna kitu, afya hakuna kitu, maji ndio usithubutu kutaja, Makazi ni nyasi na msonge kila kona, barabara ni ZERO, achilia mbali huduma nyingine za kijamii zilivyokufa.

Mbali na Hayo yote na taabu ambazo ndiyo zimetapakaa tanzania nzima, CCM ikiongozwa na Wabunge wao wengi wajejipitishia maslahi na malipo yasiyokuwa na kifani, pasipo hata kufikiria lolote kuhusu taabu hizi za watanzania umati kwa umati waliowaweka madarakani . Kosa kubwa zaidi ni kwa Watanzania hawa hawa na taabu za kupumbazwa na CCM iyo hiyo, na kuendelea kuishi katika hali hii ya dhiki kuu, na kuendelea kuwachagua kwa kupewa vijizawadi vya T-shirt, khanga na labda sh 2000 au 5000 ili wawapigie kura, bila kujitambua kuwa wanarudishwa tena katika lindi na ukiwa ule-ule kwa miaka mingine mi-5 baada ya uchaguzi.

Hii ni Laana na aibu, ba sasa watanzania wote tunatakiwa kusema sasa basi, kuendelea kuichagua CCM na JK ni maafa kwa Taifa letu ma Laana itatoka kwa Mungu kutuadhibu kwa kupenda wenyewe kuiangamiza nchi yetu mikononi mwa walafi, mafisadi, wabinafsi na watawala waovu wasioona mbali.

Picha zifuatazo zinaonyesha ni kwa nini tusipoamua sasa tutaingia katika MAAFA mengine kitaifa kwa miaka mingine mi-5 ijayo, na historia itatuhukumu kwa matendo yetu na kushindwa kuchagua kwetu.

View attachment 15738 View attachment 15734 View attachment 15739
Wanafunzi wakiwa darasani, Madarasa ya nyasi yanaonekana na pia makazi ya dhiki ya mwanachi - Mtanzania

View attachment 15730 View attachment 15732 View attachment 15731
Haya ndio Maisha ya Wazazi wetu wapendwa waliotupigania Uhuru na kutulea??

View attachment 15735 View attachment 15736
Wajawazito na Huduma za Hospitali, wagonjwa wetu wanalala chini au katika vitanda vya kamba. Huduma Bora??

View attachment 15731
Familia na watoto wanaishi maisha gani na wanapata lishe gani na katika mazingira gani??

View attachment 15733
Bado Watanzania wengi wamedoofika,hawajitambui, wamepoteza matumaini, Ni maafa haya yaliyowakumba lakini bado wanachagua CCM???

View attachment 15737

Watanzania wanapohangaika na kudhoofika kwa kiasi hiki, Je Wabunge (ambayo karibu wote ni CCM) wamejihalalishia marupurupu na malipo kiasi gani?? Rai ilitoa taarifa ya hali halisi. Na endapo ni ngumu kuifafanua hali hii, Tazama ufafanuzi unavyoweza kuonyesha Wabunge wanalipwa kiasi gani!

HALI HALISI

Sasa tucheze na hesabu 6,900,000/= kwa mbunge mmoja,zidisha mara miezi 12 then zidisha kwa miaka 5 = 414,000,000/= jumlisha 50,000,000/= anayopewa mara baada ya kumaliza miaka 5 = 464,000,000/= kwa mbunge mmoja.


464,000,000/= siko tayari kuzidisha fedha hii mara wabunge wote kwa miaka 5,calculator yangu itachanganyikiwa alafu niingie gharama ya kununua nyingine.


TATIZO NI CCM; HAYA NI MAAFA, NA TAIFA LINAANGAMIA WATU WAKE KWA KUKOSA MAARIFA na KUKOSA KUCHAGUA VIONGOZI SAHIHI NA MAKINI, WENYE UCHUNGU NA NCHI YETU.


WOTE TUSEME, HAPANA! PAMOJA TUNAWEZA! SASA BASI. TUIKOMBOE NCHI YETU. TUPIGE KURA MOJA, KURA YA NDIO KWA MABADILIKO KWA RAIS MAKINI KABISA!



DR W. P. SLAA NDIYO CHAGUO LA KULITOA TAIFA KATIKA HALI HII YA MAAFA NA KUFANI. YES WE CAN!



Asante kwa kwa kutukumbusha kule tulikopita na yale tuliyoyaona kipindi cha mzunguko,Najaribu kuvuta picha watu wale na maeneo yao hali ikoje sasa.Tunamshukuru Mungu kutupa uzima na kuendelea kujifunza mengi tuliyoyaotea.
Nashukuru sana nimesoma kwa uchungu mkubwa kwani mengi tuliyashuudia,watu wengi wanaitazama Tanzania katika miji,sina uhakika kama wengi wamefika ndani ya miisho ya Tanzania na kushuhudia miaka takribani 50 watanganyika wanaishi vipi,wapo wengiine hawajua hata kama Nyerere ni marehemu wanaelewa bado anapambana kuleta muelekeo.
 
Asante kwa kwa kutukumbusha kule tulikopita na yale tuliyoyaona kipindi cha mzunguko,Najaribu kuvuta picha watu wale na maeneo yao hali ikoje sasa.Tunamshukuru Mungu kutupa uzima na kuendelea kujifunza mengi tuliyoyaotea.
Nashukuru sana nimesoma kwa uchungu mkubwa kwani mengi tuliyashuudia,watu wengi wanaitazama Tanzania katika miji,sina uhakika kama wengi wamefika ndani ya miisho ya Tanzania na kushuhudia miaka takribani 50 watanganyika wanaishi vipi,wapo wengiine hawajua hata kama Nyerere ni marehemu wanaelewa bado anapambana kuleta muelekeo.
Hongera kwa kuzunguka Tanganyika yote na kujifunza maisha halisi ya Wadanganyika. nilikuwepo pale Mwembeyanga Dr Slaa alipozungumzia maafa kwa kuichagua CCM. Tulionywa hautkusikia, tuliweka pamba masikioni mwetu, tukamezwa na propaganda za udini na mambo binafsi ya Dr Slaa. Leo ni majuto pande zote. hakuna mishahara, mfumuko wa bei, mabomu, mgao wa umeeme, dowans, wabunge wetu wanapiga porojo na majungu bungeni, kila mtu afe kivyake. Full stop
 
kweli ni maafa na tunaendelea kuyapata hayo maafa...
Tutakukumbuka Dr.Slaa daima
 
Watu kama kibunango inatakiwa wafungwe jiwe shingoni na kutupwa baharini. Ni mkosi na laana kubwa kuwa na watu wenye upeo na mawazo mfu, finyu kama Kibunango. Umelaaniwa wewe!! kwa kutetea uovu wa hilo pepo baya linaloitwa CCM linalowatesa watoto wa Mungu(watanzania).
 
Back
Top Bottom