Kuirudisha CCM madarakani ni maafa ~ Dr Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuirudisha CCM madarakani ni maafa ~ Dr Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Not_Yet_Uhuru, Oct 26, 2010.

 1. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  WADAU...SIO VIBAYA KUKUMBUSHANA 'KAULI HII YA BUSARA ILIYOTOLEWA NA MWENYE KUONA MBALI!

  [h=2]Dr slaa aliposema kuchagua JK na CCM ni maafa kwa taifa, ni nini? Ni ukweli?[/h]

  Asilimia 85 ya Watanzania na hasa wale wanaoishabikia na kuichagua CCM wanaishi katika taabu, shaka na maisha magumu kuliko raia wowote wa nchi yetu hii ambayo Mungu amaibariki kuwa na kila aina ya neema. Ila tu wananchi wanashindwa kufikiria, au wanakuwa wavivu kufikiria na kuamua ili wawapate viongozi makini na wenye uchungu.

  Ikichukua mfano mdogo wa Majimbo yaliyo chini ya Vyama ambayo havina Serikali kwa sasa mfano Karatu na Moshi Mjini, Tarime (Chadema), na Bariadi (UDP) nk, utagundua kuwa wananchi wengi wana ufahamu mkubwa na wamejikwamiua sana kimaendeleo, mfano jimbo la Karatu pekee, wananchi karibu kila kona wana huduma za maji safi, afya, barabara, shule za hali ya juu achilia mbali vitega uchumi na kipato bora.

  Ukichukua Jimbo lolote la Wilaya ya Bagamoyo; and Mkoa wa Pwani - ambako ndio Kikwete amekuwa Mbunge kwa Miaka zaidi ya 20, utapata picha halisi ya ni kwa nini kuichagua tena CCM na JK ni maafa kwa taifa. Shule hakuna kitu, afya hakuna kitu, maji ndio usithubutu kutaja, Makazi ni nyasi na msonge kila kona, barabara ni ZERO, achilia mbali huduma nyingine za kijamii zilivyokufa.

  Mbali na Hayo yote na taabu ambazo ndiyo zimetapakaa tanzania nzima, CCM ikiongozwa na Wabunge wao wengi wajejipitishia maslahi na malipo yasiyokuwa na kifani, pasipo hata kufikiria lolote kuhusu taabu hizi za watanzania umati kwa umati waliowaweka madarakani . Kosa kubwa zaidi ni kwa Watanzania hawa hawa na taabu za kupumbazwa na CCM iyo hiyo, na kuendelea kuishi katika hali hii ya dhiki kuu, na kuendelea kuwachagua kwa kupewa vijizawadi vya T-shirt, khanga na labda sh 2000 au 5000 ili wawapigie kura, bila kujitambua kuwa wanarudishwa tena katika lindi na ukiwa ule-ule kwa miaka mingine mi-5 baada ya uchaguzi.

  Hii ni Laana na aibu, ba sasa watanzania wote tunatakiwa kusema sasa basi, kuendelea kuichagua CCM na JK ni maafa kwa Taifa letu ma Laana itatoka kwa Mungu kutuadhibu kwa kupenda wenyewe kuiangamiza nchi yetu mikononi mwa walafi, mafisadi, wabinafsi na watawala waovu wasioona mbali.

  Picha zifuatazo zinaonyesha ni kwa nini tusipoamua sasa tutaingia katika MAAFA mengine kitaifa kwa miaka mingine mi-5 ijayo, na historia itatuhukumu kwa matendo yetu na kushindwa kuchagua kwetu.

  View attachment 15738 View attachment 15734 View attachment 15739
  Wanafunzi wakiwa darasani, Madarasa ya nyasi yanaonekana na pia makazi ya dhiki ya mwanachi - Mtanzania

  Umaskini1.jpg umaskini2.jpg Umaskini5.jpg
  Haya ndio Maisha ya Wazazi wetu wapendwa waliotupigania Uhuru na kutulea??

  umaskini3.jpg View attachment 15736
  Wajawazito na Huduma za Hospitali, wagonjwa wetu wanalala chini au katika vitanda vya kamba. Huduma Bora??

  Umaskini5.jpg
  Familia na watoto wanaishi maisha gani na wanapata lishe gani na katika mazingira gani??

  Udhoofu na Njaa_eti wao CCM damu.jpg
  Bado Watanzania wengi wamedoofika,hawajitambui, wamepoteza matumaini, Ni maafa haya yaliyowakumba lakini bado wanachagua CCM???

  View attachment 15737

  Watanzania wanapohangaika na kudhoofika kwa kiasi hiki, Je Wabunge (ambayo karibu wote ni CCM) wamejihalalishia marupurupu na malipo kiasi gani?? Rai ilitoa taarifa ya hali halisi. Na endapo ni ngumu kuifafanua hali hii, Tazama ufafanuzi unavyoweza kuonyesha Wabunge wanalipwa kiasi gani!


   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Unajua muda mwingine nafikilia kuwa watz hatufikilii saana but NAGUNDUA KUWA WATZ WENGI ELIMU HAWANA NI WAVIVU WAKUFIKIRI! kwa sasa ccm kila mtu ilitakiwa aichukie toka Moyoni!
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Kusema kweli nakubaliana na maoni yako Msaki001 kuhusu jimbo la jk, hususan maeneo ya kutokea Chalinze mpaka inapoanzia Wilaya ya Handeni. Mara nyingi husafiri kwa gari kwenye barabara ya Chalinze-Segera.

  Mwaka 2005 nilikuwa na baba yangu kwenye moja ya safari hizo. Tulipofika maeneo ya Msata tukiwa tunaelekea Chalinze, baba ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu, akauliza, "hivi hawa watu wamekosa nini? Maeneo mazuri haya wameshindwa hata kulima? Hapa mahindi yatastawi sana. Ardhi ina rutuba, lakini watu wamekaa pembeni wanauza mkaa, wamebeba kuku wa kienyeji wanatafuta soko. Nyumba nzuri hakuna, kila kilometa chache tunaona watu wamebeba ndoo na madumu ya maji. Hivi ni kweli hapa hakuna maji safi? Mbona kuna mto Wami mkubwa unapita karibu na mto Ruvu hauko mbali. Kweli serikali imeshindwa kuwapatia hawa watu maji safi na salama bila ya wao kusumbuka kiasi hiki?"

  Nilimtazama mzee wangu kwa butwaa. Ameweza kutazama na kufanya tathmini yake ya hali ya maisha ya watu hawa kwa kuwaangalia kwa muda mfupi tu. Baba yangu hakuwa msomi, lakini aliweza kuona kuwa hapa kuna tatizo. Nina hakika maji hata ya kuchimba visima ardhini yanaweza kupatikana, pale sio jangwa. Ardhi ina rutuba wakati wa mvua majani ni marefu na mazuri sana. Lakini watu wake wanaishi katika hali duni sana. Siku hizi za karibuni kumeibuka Palace upande wa kulia ukiwa unatokea Segera, limeota kama uyoga. Limezungukwa na vibanda vya wenyeji wa eneo hilo. Na bado wao wanaona fahari kuwa mbunge wao ni mkuu wa nchi, pamoja na kwamba hali zao ni bora maisha.

  Kuendelea na hali hii ni kujitakia maafa makubwa, sio kwao tu bali kwa Taifa zima.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nakubaliana na ww mkuu kwa kweli mkoa wa pwani umebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba ni uongozi mbovu tuu!
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Uzuri Slaa posho lake anatumia kuhadaa na kupora wake za watu
   
 6. Profesy

  Profesy Verified User

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe unajuaje? Umemrekodi? Maana siku hizi mafisadi wameshindwa kujibu maswali kuhusu hela iliopotea lakini wanajibu kwa kusema flani kaiba mke wa mtu.

  Hivi kuiba mke wa mtu na kuwaibia wananchi ipi mbaya zaidi? tangu lini kupora mke wa mtu imekufanya usijenge barabara au zahanati? Tangu lini jibu sahihi ukiulizwa hela zimeenda wapi ni eti uko na mke wa mtu.

  USE YOUR BRAIN BEFORE TYPING... (kumbuka ni home of great thinkers):nono:
   
 7. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu Kibunango; Maneno yako ni huzuri kwa jinsi ulivyo na mawazo dhaifu!
  Mgonjwa akikaribia kututoka, hata akipewa dawa anaitema, na hata akiambiwa awaishwe hospitali anasema 'niacheni humuhumu ndani' ndiyo wewe , na wenzako mnaokuwa wavivu kuufikiria udhoofu wa kifikra na ki-saikolojia mliokuwa nao kwa kuiogopa na kuiabudu CCM bila kujua kuwa saa ya kufa msaada ni muhimu saana!

  Na msaada wenyewe ndio Dr Slaa, ndio mwenye dawa halisi unayotakiwa uipokee katika ulimi, unatakiwa ufungue tu mdomo upokee dawa ya kukuponya. Bado unabaki katika mawazo yaliyokufa ya kujadili personal issues badala ya substances au logical na materials ambayo Tanzania inahitaji kwa karne mpya na kizazi kinachoona mbali! Aibu!
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Heshima mbele Mkuu, mbona hili suala la mke limekukuna sana?
   
 9. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kilaza wewe, na sijui kwann wanarusu comment zako na ilo lipicha la bendera
   
 10. A

  Awo JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Labda ndie Mahimbo mwenyewe! Tena acha kuwafananisha wake za watu na bidhaa, inayoweza kuibiwa. Hiyo ni dharau kubwa kwa mama yako na dada zako!!
   
 11. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ufinyu wa fikra na ukiritimba wa kuona mbali kama walivyo wanaokuongoza!

  Ila hao hao wanasahau matendo yao machafu! Kibunango; unaweza kutufahamisha vyema mateso wanayopata Babu Seya na watoto wake yametokana na nini au na uchafu wa nani?? Kama ujalo jibu sahihi, hapa wana-JF wataweza kukufikiria kuwa fikra zako zinaelekea kwenye mwanga angalau kidogo!
   
 12. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kibunango,na mm ntapora mkeo tu we subiri
   
 13. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Jamani eeh, mke wa mtu anaibiwaje? Kwani huyo mke wa mtu sio mtu, naye si anao uamuzi na atashi wake? Mbona mnaangaika kuusemea moyo wake? Yeye kama kaibwa mbona anaona ni shwari tu?

  Leteni mada za kubadili taswira ya taifa kwa ujumla na si mada au hoja dhaifu ya kujadili vitu visivyojadilika. Mtu unaweza kuiba mali na kuificha au kuuza ili unufaike zaidi, sasa ukiiba mke wa mtu utamuuza wapi au utam-invest wapi ili upate faida. Acheni mambo ya Kikwere... Wakwere wamezoea kushinda ngomani na wakifanikiwa kulala na mke wa mtu au kumchukua huwa wanaona ni ufahari. Lakini hawajui kuwa hata huyo mwanamke kumkubali lazima kuna vitu alikuwa anavikosa huko alikokuwa.

  Naomba mada ya mke wa mtu ife, na ikome kutokezea katika mada muhimu za maendeleo. Badilikeni kama mnapenda maendeleo. Huu sio uwanja wa taarabu. Ebo!
   
 14. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  YUSUFU MAKAMBA..!:tape:
   
 15. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Penetrations ..................either by willingly or by force,
  no way
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  huyu kibunango nilidhani ana busara sana kumbe bureeeeeee, wewe km humkuni mkeo unadhani atakuganda wewe tu, lzm akipata mkunaji wewe utaonekana km kaka yake tu. Slaa amekuna pande zote kuanzia mke wa mtu hadi waTANGANYIKA.
   
 17. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  hivi bado unatumia bangi?au kale kaugonjwa ka kili bado kanakusumbua? nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri unaonekana kama dakika tano mbele
   
 18. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  jeykey na mabinti wadogo(viky kamata,stella mwaibale,....)ongezea pls
   
 19. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  wa kwake aliporwa na jeykey
   
 20. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Roho yako ya kifisadi. Inaelekea umekunwa sana kuliko mwenye mke. Kwetu tuna msemo kwamba anayelia sana kwenye msiba ndiye mchawi

  Baada ya ilo nasisitiza kwamba kumchagua JK (PhD fake) ni janga la kitaifa!
   
Loading...