Kuiponya UKAWA, hawa lazima wakatwe

Kuiponya UKAWA, hawa lazima wakatwe

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,006
Nashauri tu watani zangu wa UKAWA. Nawashauri kuwakata wawili wanaotajwatajwa kuwa wana mvutano usio na mfano na kusababisha mkwamo. Saa 11 za jana zilishindwa kumaliza VUTA-NKUVUTE hiyo. Wanapaswa kukatwa au wao wenyewe wajitoe kugombea Urais kwa bendera ya UKAWA. Hata CCM yetu ilipoona Lowassa na Membe wamepania,wakakatwa. Wote walipoondolewa kwa kukatwa,mambo yakatulia.

UKAWA wanapaswa kuwakata wawili hawa. Ni mafahari katika vyama vyao na hivyo hawawezi kuishi kwenye zizi moja. Hakuna atakayekubali kushindwa hivihivi tu. Patachimbika na UKAWA kusambaratika. Maneno ya Mbatia ya jana kuwa mambo yanakwnda sawia na mgombea ameshapatikana hayana tofauti na yale ya Nape Nnauye baada ya kikao cha CC. Baadaye wakaibuka akina Nchimbi. Maneno ya Mbatia ni ya kisiasa na kidiplomasia.

Nawashauri UKAWA mambo mawili. La kwanza,kuwakata Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na Dr. Wibrod Peter Slaa katika orodha ya wanaotaka ugombea. La pili, wamsimamishe Tundu Antipas Mughwai Lissu kupeperusha bendera UKAWA. Dr. John Pombe Magufuli,mgombea mteule wa CCM, ni heavyweight. Wa level yake ni Lissu tu wakishakatwa hao wawili. Nanyamaza nitazame na kusikia mlivyonielewa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Hawa wanaofikiriwa bado wana kesi mahakamani.
UKAWA wasije wakakosea wakapendekeza yeyote mwenye kesi maana watalia kilio cha mbwa pindi kesi za wagombea wao zitakapoamuliwa na wa kuchukua fomu utakuwa umekwisha.
Labda wampe Kafulila.
 
Mgombea ameshapatikana na wameshakubaliana. Sasa hivi ni CUF, inawaweka sawa wafuasi wake ili wakubaliane na maafikiano ya UKAWA wasije kubaki nje, wakapotea.

Hoja ya kukatwa wala kusukwa, sasa haipo!
 
Natamani kuona mpambano wa Lissu Vs Magufuli.

Yoyote atakayeshinda serikali ijayo itakuwa na vionjo vipya. Labda itokee tu.

Naunga mkono hoja.
 
mkuu sisi huku ukawa refa hajapoteza kipenga wala kadi...anasaidiwa kwa ukaribu na washika vibendera....mchezo unaendelea vyema...hakuna kukatana mitama na mpaka sas hakuna hata mmoja aliyeonyeshwa kadi ya njano achilia mbali nyekundu...mchezo utakwisha salama
 
Tatizo mashabiki wa Chadema wengi mawazo yao ni mgando, wao wanajua anayefaa kugombea urais ni Dr. Wilbroad Slaa tu kumbe hawajui kuna vichwa vingine vingi ambavyo vinaweza kupeperusha bendera vizuri kabisa.
 
watakutukana wenye chama chao shauri yako ngoja waje.
 
VUTA-NKUVUTE

wewe bavicha unakazi kweli wambie wewe ni wazee wako.
 
Last edited by a moderator:
VUTA-NKUVUTE figisu zinazoendelea ndani ya UKAWA sio kati ya mtu na mtu bali ni masrahi ya chama na chama plus uchumia tumbo!!
Tunaimani haya yote yatapita bila kukatwa mtu labda chama chenye uroho wa pesa.
 
Last edited by a moderator:
Mgombea ameshapatikana na wameshakubaliana. Sasa hivi ni CUF, inawaweka sawa wafuasi wake ili wakubaliane na maafikiano ya UKAWA wasije kubaki nje, wakapotea.

Hoja ya kukatwa wala kusukwa, sasa haipo!

Mbona Chadema hawajaenda waweka sawa hao wananchi wao??

Why CUF na Sio vyama vingine?
 
Tatizo mashabiki wa Chadema wengi mawazo yao ni mgando, wao wanajua anayefaa kugombea urais ni Dr. Wilbroad Slaa tu kumbe hawajui kuna vichwa vingine vingi ambavyo vinaweza kupeperusha bendera vizuri kabisa.

Hata CCM walikuwa na vigezo muhimu vya kuzingatia kabla ya kupata tano bora. Tatizo la UKAWA ni ubinafsi wa baadhi ya Vyama vya siasa vinavyounda UKAWA.

Kila mwenye analysis mind hawezi kupinga ukweli kuwa Dk Slaa anafaa kuliko wagombea wengine kwa nafasi ya Urais ndani ya UKAWA.

Ikiwa UKAWA watasamvaratika ktk hili la Urais, chama ambacho kitajitoa au kutengwa kitadidimia zaidi.

Mwaka 2000, Chadema walikuwa walikuwa radhi na walimwachia Prof. Lipumba na CUF kusimamisha mgombea Urais, lkn pamoja na kauli ya karibuni ya Prof. Lipumba baada ya kupitishwa na CUF kuwa atamuunga mkono mgombea yoyote atayepitishwa na UKAWA, naona kuna uzito wa CUF kukubali mgombea mwingine nje ta Prof. Lipumba.

Vv
 
Back
Top Bottom