The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,495
- 2,042
Ni aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kesho anatarajiwa kuzungumzia mgogoro unaoendelea ndani ya CUF kupitia kituo cha Clouds fm ktk kipindi kinachoruka asubuhi.
---------------------------
- Mbunge wa Kaliua Mh. Sakaya bado ni mwanachama na Mbunge, kikao kilichofanyika kumsimamisha uanachama hakina uhalali, Mh. Sakaya ilibidi awe kwenye Kikao hicho kama Naibu katibu Mkuu Bara ambaye ni msaidizi wa Katibu mkuu ndio alikuwa anahusika kuandaa kikao lakini hakuwa na taarifa mpaka siku moja kabla ya kikao ndio akajulishwa.
- Vikao vya CUF vina utaratibu, hiki hakikufuata utaratibu maana cha kimafia.
- Vyama vinavyounda UKAWA vilikubaliana kumsimamisha Mgombea mmoja kati ya Dr. Slaa, Prof. Lipumba na Dr. Kahangwa wa NCCR Mageuzi.
- Nilikaa kikao na Dr. Slaa na Dr. Kahangwa nyumbani kwangu na tukakubaliana kwakuwa wenzetu CHADEMA wamejiandaa na wana uwezo mkubwa basi wamsimamishe Mgombea wa Urais (Dr. Slaa), CUF hatukuwa na uwezo.
- Wakati tunapanga kumbe Mbowe na Seif walikuwa wanamshawishi Lowassa ahamie CHADEMA na awe mgombea Urais.Mh Mbowe na Maalim walikuwa wanawasiliana peke yao katika kuhakikisha EL anakuwa mgombea kwa bendera ya UKAWA bila kushirikisha kamati tendaji za vyama vyao.
- Tulikuwa tumekubaliana kutosimamisha mgombea wa makapi, tulitaka mgombea aliyetoka ukawa aliyekuwa anaunga mkono rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, Lowassa hakuwa anaunga katiba ya Jaji Warioba.
- Nilimshawishi Warioba agombee Urais kupitia UKAWA, Alikataa na kusema yeye bado ni mwanaCCM.
---------------------------
Updates Sept. 08, 2016
- Sikuwa na barua ya kusimamishwa uanachama mpaka waliposikia nitakuwa Clouds ndipo wakaniletea barua ya kunisimamisha. Barua ilikuwa ya tarehe 30 Agosti, 2016 na niliipata jana tarehe 7 Septemba.- Mbunge wa Kaliua Mh. Sakaya bado ni mwanachama na Mbunge, kikao kilichofanyika kumsimamisha uanachama hakina uhalali, Mh. Sakaya ilibidi awe kwenye Kikao hicho kama Naibu katibu Mkuu Bara ambaye ni msaidizi wa Katibu mkuu ndio alikuwa anahusika kuandaa kikao lakini hakuwa na taarifa mpaka siku moja kabla ya kikao ndio akajulishwa.
- Vikao vya CUF vina utaratibu, hiki hakikufuata utaratibu maana cha kimafia.
- Vyama vinavyounda UKAWA vilikubaliana kumsimamisha Mgombea mmoja kati ya Dr. Slaa, Prof. Lipumba na Dr. Kahangwa wa NCCR Mageuzi.
- Nilikaa kikao na Dr. Slaa na Dr. Kahangwa nyumbani kwangu na tukakubaliana kwakuwa wenzetu CHADEMA wamejiandaa na wana uwezo mkubwa basi wamsimamishe Mgombea wa Urais (Dr. Slaa), CUF hatukuwa na uwezo.
- Wakati tunapanga kumbe Mbowe na Seif walikuwa wanamshawishi Lowassa ahamie CHADEMA na awe mgombea Urais.Mh Mbowe na Maalim walikuwa wanawasiliana peke yao katika kuhakikisha EL anakuwa mgombea kwa bendera ya UKAWA bila kushirikisha kamati tendaji za vyama vyao.
- Tulikuwa tumekubaliana kutosimamisha mgombea wa makapi, tulitaka mgombea aliyetoka ukawa aliyekuwa anaunga mkono rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, Lowassa hakuwa anaunga katiba ya Jaji Warioba.
- Nilimshawishi Warioba agombee Urais kupitia UKAWA, Alikataa na kusema yeye bado ni mwanaCCM.
Lipumba: Seif anaiuza CUF bara kwa bei poa
Kufukuzwa kwa Wabunge ni kujenga misingi ya kuimaliza CUF Bara kuifanya isiwe na nguvu na hapa Maalim Sef anaiuza CUF Bara kwa bei poa. Haya sio maneno yangu, ni maneno ya Professa Lipumba wakati akiongea na Clouds FM katika kipindi cha Power Breakfast.
Kuhusu uwepo wa Lowassa ndani ya UKAWA Professa anasema, “Sababu za msingi za kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA, ni kwamba ukiwa katika siasa unahitaji uongozwe na misingi na 'principals' na hoja kwamba mnagombea kitu gani, na sisi tulianzisha UKAWA kwa kusema kwamba tutafute nchi, serikali na dola inayowajibika ambayo inatengeneza mambo vizuri, inatumia rasilimali vizuri itapambana na ufisadi na itajenga demokrasia ya kweli katika nchi yetu,
Ukiwa na misingi hiyo kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na tulikuwa wote kwenye bunge la katiba na Mh. Edward Lowassa alikuwepo kwenye bunge hilo hakuwa mmoja ya wabunge aliyeunga mkono rasimu ya Katiba" Ibrahim Lipumba
"Kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa na ile misingi iliyotuunganisha kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na ukumbuke Mh. Edward Lowassa alikuwepo katika bunge la katiba ya rasimu ya Jaji Warioba na hakuunga mkono rasimu hiyo kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa na ile misingi iliyotuunganisha na kuanzisha UKAWA kuja kumchukua Edward Lowassa ndiye awe mgombea urais wa watu wanaounga mkono rasimu ya Jaji Warioba" Ibrahim Lipumba