Kuiper Belt: Behind the certain

Zimbabwe huko walitua kwenye shule moja ya chekechea na wale watoto walisimulia hii kitu.Nilishawahi kuona documentary ya hili tukio siku za nyuma sana na nitaisaka hii kitu.....

Mkuu kwani unafahamu NWO ni kitu gani?
Kama una jina la hiyo documentary naomba unitajie tafadhali,
 
Kaka nimeisoma makala yako kwa umakini mkubwa kadiri ambavyo Mola wa ulimwengu amenijaalia.Mimi,wewe na wao sisi sote ni binadamu na hatujakamilika mkamilifu ni Mola peke yake,kwahiyo ukikuta kosa katika andiko langu ni sababu ya ubinadamu wangu.

Katika huu ulimwengu kuna jambo la umuhimu na umuhimu zaidi,na kuna kinyume chake pia.Kwa mujibu wa makala yako kama ulivyoeleza umesema ya kuwa umetoa ushahidi juu ya uwepo wa hao viumbe na ukanukuu ya kuwa wapo takribani sampuli 104,na ukatutajia chache miongoni mwazo.Kiukweli hata kwa mwenye akili ndogo na uelewa dhaifu kama wangu hatokububali kama wewe hapo umetuthibitishia uwepo wa hao viumbe.

MAELEZO MACHACHE JUU YA TAMKO "USHAHIDI"

Tamko ushahidi kiasili ni tamko la kiarabu lenye maana ya kushuhudia yaani kukiri.Ushahidi una mapito mengi sana mpaka ukafikia kiwango cha kuitwa ushahidi.Nataka nikupe mfano,kamwe kipofu hawezi kukupa ushahidi wa kuona,hapa nina maana pana sana,upofu upo wa kimaumbile na upofu wa kimaana.Mfano asie msomi ni muhali kukupa ushahidi wa kisomi na mfano wake.Ushahidi pia unapitia katika masimulizi kutoka kwa watu wenye kuaminika,wasomi,wenye ujuzi wa kupambanua jema kutokana na baya na mfano wake.Pia kuna ushahidi wa kuona,lakini ni ule ushahidi ambao nani ameona.Mfano wa tukio moja lililo ona na watu wanne kwa wakati mmoja na kila shuhuda kati yao akakupa maelezo tofauti juu ya kutokea kwa tukio hilo.Hapo ndipo utakapo staajabu suala zima la kuchukua habari na kuihakiki pia.Kwa ufupi hapa tunaona kuna ushahidi wa kuona,kusikia lakini kwa kukidhi vigezo.

SAYANSI NA VISASILI,PAUKA PAKAWA NA NGANO ZA KUSADIKIKA

Sayansi ya leo imekuwa kama hadithi na stori za vijiweni huku zikitiliwa nguvu na mapicha picha ya kubuni,kutilia nakshi dhana zao.Mimi baada ya kuupata ukweli juu ya suala la mtu kwenda mwezini,hapo ndipo nilipoinua kalamu yangu na kufumba macho yangu juu ya suala la kuamini tena mambo ya anga.Sijakuilia katika kukaririshwa,nimekulia katika uhakiki wa habari na wapi nikachukue habari.

Kuna ukweli ambao kila mtu mwenye akili timamu anapaswa kuujua ya kuwa si kila kinachezungumzwa na sayansi au wanasayansi kina ukweli,la hasha kufikiri kwa mtindo huo ni kufikiri kwa kitoto.Sayansi imekuwa yao kwa ajili yao wenyewe wanasayansi kufurahisha nafsi zao,kwani wanajua ya kuwa watu wa leo ni vigumu sana kuhoji na hata kama wakihoji hoja zao zitawafikia wakina nani na lini ? Kujadili ya maana muda huo hatuna tuna muda wa kusaka umbeya mitandaoni na kumsema fulani.Mwanachuoni mmoja alipata kusema "Itafikia zama jambo la kufanya kwa wiki moja litafanya kwa muda wa mwaka".Hakuziona zama zetu wala hakuiona kesho yake,bali elimu aliyopewa ikamuakisia ya mbeleni kwa idhini ya Mola aliye juu.Ukweli wa kauli yake uko wazi mithili ya tulionavyo jua la saa sita mchana.Leo tumeshughulishawa na mambo ya kijinga na kuacha kufanya mambo ya msingi,mwisho wake tunapotaka kufanya mambo ya msingi tunakuwa na uchache wa taarifa juu ya jambo husika,na tukianza kufanya basi nanga inapaa.

SAYANSI HAINA UWEZO WA KUJIBU AU KUELEZEA SUALA LA UWEPO WA VIUMBE FULANI NA UHAI WAO

Sayansi haina uwezo kutuelezea juu ya uwepo wa maisha ya viumbe fulani na ukweli juu ya viumbe wao.Sayansi imejengeka katika misingi ya nadharia na kufanya majaribio,yaani aidha ianze nadharia lifate jaribio au lianze jaribio ifate nadharia.Sayansi inafanya na mwanadamu ambaye si mkamilifu,swali ni vipi upate ukamilifu kutoka kwa kisicho kikamilifu ? Swali hili ni jepesi mno.Sayansi haiamini mpaka kitu kionekane na nadra sana ukihisi.

Sitaki kujua walitumia nini au walitambua lini,sababu msingi ukianguka na jengo limeanguka.Picha wazitoazo wanasayansi juu ya masuala yote ya anga achilia mbali kuhusu hii ngano ya Aliens si halisi ni picha za kubuni.Hivi kwa maendeleo wayasemayo ni kweli wangekuwepo hao viumbe tungekosa picha zao halisi au hata video zao ?

Ukweli ni kwamba walijua jambo hilo halipo ndio maana wakaamua kummwagia sifa kiumbe huyo asiyekuwepo ya kuwa anaakili nyingi sana za kumzidi bina damu.Ili ukitokea kuhoji jambo hilo wasikupe jibu lenye kueweka.

Pindi wanasayansi walipojigonga juu ya swali je ni jua linazunguka dunia au dunia inazunguka jua ? Hapo ndipo utakapo ona makanjanja ya sayansi.

JE NI YUPI ADUI MKUBWA WA BINADAMU ?

Hili ni swali la msingi sana kujiuliza juu ya kile ulichokiwasilisha.Kutokana na ngano hii ya kisayansi inaonyesha kwa wazi ya kuwa hawa ndio maadui wakubwa sana wa binadamu,kitu ambacho si kweli.Adui mkubwa wa binadamu ni SHETANI kama vile Allah alivyotueleza katika Qur'an.(Natumia Qur'an sababu ndio kitabu ambacho nakisoma na ndio muongozo wangu).

Sasa labda waje hapo baadae wakanushe tafiti yao ya kuwa kiumbe walie mkusudia ni SHETANI wa kijini na sio hawa Aliens,hiyo ni baada ya kufanya utafiti zaidi ya miaka 100,hivi ndio wasemavyo waitwao wansayansi.Na kama wakiseama hivyo itabidi wajibu maswali haya.SHETANI wa kijini ni mmoja anaitwa ibilisi na yeye ndio ana kazi ya kuwaletea wasi wasi binadamu na kuwashawishi kufanya maovu.Zaidi ya hapo shetani ni sifa kwayo anaweza kuwa nayo binadamu na majini pia.

NI KWELI WAPO VIUMBE ZAIDI YA HIVI VILIVYOPO ULIMWENGUNI NA HATUVIJUI,TENA NAVYO VIPO VIWILI VIWILI

Huu ni ukweli mwingine ambao ni dharura mwanadamu kuujua.Mola mlezi anasema mwenyewe ya kuwa na katika viumbe msivyovijua viko viwili viwili,au kama alivyosema Allah.Na Allah anaendelea kuumba ila katika hao viumbe tusio wajua ni sisi hatuwajui na hatuwezi kuwaelezea sababu hatuwajui.Kwahiyo sual la ugunduzi juu ya viumbe tusivyovijua ni halipo sababu hatuvijui.Sasa hili suala la Aliens limetoka wapi ?

NGANO YA ALIENS IMEKOSA SIFA ZA KIELIMU NA UHAKIKI WA HABARI

Suala la Aliens limekosa sifa hizo hapo juu.Sababu watoaji habari hawana sifa ya kuaminiwa kutokana na misingi yao dhaifu walijijengea.

BINADAMU NDIO MMBORA WA VIUMBE

Kutokana na nususi za kiimani na ndizo nususi za kweli na zenye kuaminika sababu maandiko yaliitangulia sayansi kitambo sana.Nususi hizi zinasema hakuna kiumbe mmbora kuliko mwanadamu hata majini hawafikii ubora wa binadamu.

ZIADA

Maelezo hayo ni maoni machache katika yale niliyotaka kuyatoa,na wakati mwingine nikipata muda nitakuja na maswali juu ya kile ulichokiwasilisha.

SIKU NYINGINE KIONGOZI TUELETEE USHAHIDI JUU YA UWEPO WA HAO VIUMBE.NAJUA USHAHIDI HAUNA WALA HAUTAKUWA NAO.

HITIMISHO

Hakuna viumbe viitwavyo Aliens kwa sifa hizo na maelezo hayo na sayansi haina uwezo wa kuelezea uwepo wa kiumbe chochote na chenye kuishi bila kukidhi vigezo vya uhakiki wa habari.Bali kuna majini,na watakuja kudhihiri viumbe viitwavyo YAAJUJ WA MAAJUJ navyo ni katika uzao wa Adamu,yaani binadamu kama sisi sema wanasifa z uharibifu na mfano wake.
 
Mkuu

Kwenye makala yangu kwanza nimeanza kuzungumzia kuhusu uwepo wa aneo ambalo kisayansi lina ushahidi wake....

Ninafahamu kwamba hakuna picha halisi za Aliens na jambo hili haliwezi kufanya wasiwepo.Sijasema kwamba picha nilizoweka ni halisi......

Sijui kama unaelewa kuwa hadi kitu kikubalike au kiwe kimethibitishwa ni mpaka taasisi zilinazokubalika na serikali duniani kukubaliana na suala husika.Mfano ni kwamba kama kitengo cha sayansi ya anga cha Marekani ambacho kinakubaliwa na serikali ya Marekani na dunia kwa ujumla kikikubaliana na uwepo wa sayari fulani basi jambo hilo hukubaliwa ramsi na kuanza kufundishwa mashuleni.Suala hili la Aliens halijakubaliwa na hao wanasayansi isipokuwa wanasayansi binafsi na walioamua kufanya utafiti wao binafsi ndiyo wanakubaliana na suala hili...

Unapaswa ulielewe jambo hilo kwasababu inaonekana unadhani kuwa jambo hili linakubalika rasmi duniani.Pamoja na hayo kuna watu wengi tu ambao wamehojiwa na kusema wameshawaona hao Aliens,huo ni ushahidi labda uwe hauukubali.....

Kwasababu hii hoja yako ya kulikataa jambo hili kwa kuegemea dhana yako ya kutokukubaliana na wanasayansi linakosa mashiko kwasababu uwepo wake hauegemei kauli za wanasayansi pekee kwani wapo mashuhuda pia....

Suala lako la kufikiri kuwa binadamu hawezi kujua uwepo wa viumbe wengine mahali pengine sijalielewa vizuri hasa limesimamia wapi.Kujua ni kufanya nini kwani? Naona hapo umesema kuwa ukamilifu hauwezi kutoka kwenye kutokukamilika,kwani kujua jambo ni ukamilifu?

kuwepo kwa Aliens na kuonekana kuwa adui ya binadamu hakumuondoi Shetani kuwa adui wa binadamu .Naona wengi wanachanganya jambo hili kwa kudhani kuwa uwepo wa Aliens unamfanya Shetani asiwepo....

Hao Aliens wanaweza kuwa ni product ya huyo huyo Shetani vile vile mkuu hivyo usidhani kuwa uwepo wa Shetani kunaondoa uwepo wa Aliens na kinyume chake....

Hivi mkuu ubora wa binadamu ni nini au uko wapi?

Msingi wa makala hii naona hujauelewa kabisa ndiyo maana unaendelea kudai ushahidi.Unaweza kuisoma upya ukaelewa zaidi mkuu....
 
Kiongozi ninapo sema misingi ya sayansi ndio kikwazo cha kufikia ukweli muhimili namaanisha mzee.Unaposema ya kuwa kutokuwepo picha za Aliens hakuondoi uwepo wa Aliens.Kauli hii si yakisomi na niayakukata tamaa,rejea katika misingi ya sayansi ndio ujibu hoja yangu.Kielimu kama huna ushahidi wa unachokiegemea hauna ruhusa ya kuongea.Kama picha picha halisi ya Aliens haipo kwanini wanatuchorea picha za kufirika ?

Mzee tabia ya ukweli unamea popote.Leo kuna mifano mingi ya juu ya mengi tusiyoyaona na wala hatujawi kupewa mfano wa picha za hayo mengi lakini tunayaamini na kuyashikilia kwa meno ya magego.Sababu kuna ushahidi makini juu ya hayo mambo mpaka umepelekea tukayaamini.

Na suala lako la wewe kusema ya kuwa yawezekana ya kuwa hao Aliens wanaweza kuwa majini ni uvivu wa kufikiri,ina maana ni jinsi gani unajaribu kuihujumu elimu na ukweli halisi,kama jambo hulijui kwanini usiulize au usiwaulize hao wanaoandika habari za Aliens ?

Swali litakuja Je unaweza kutupa uhusiano uliopo kati ya majini na hao Aliens,kama utakuja au unadhani ya kuwa hao Aliens wanaweza kuwa Majini.

Msingi wa ELIMU,ni kujifunza kwanza kabla ya kutenda na kusema.

Ukija kutaka kujua ubora wa binadamu hapa nakupa hoja za kiakili wala si hoja za kiufunuo hoja ambazo ni za hakika.Binadamu ndio viumbe waliopewa akili,na utambuzi wa kung'amua mambo na ubora wa binadamu unakuja kutokana na mambo anayayafanya na majuto anayokuja kujutia baada ya kufanya uzembe fulani.

Binadamu ndio aliepewa dhamana ya Elimu kuitumikia na kuifanyia kazi.Bibadamu ndio amepewa uwezo wa kuwatawala viumbe wengine,viumbe ambao kwa ukubwa ni zaidi ya mara hamsini kuliko mwanadamu mwenyewe.Mifano juu ya hili iko mingi na ukikataa itabidi uituhumu akili yako mzee.

Kuhusu kutokuielewa makala yako,maneno hayo si sahihi sababu,nimegusia mambo muhimu juu ya udhaifu wa sayansi na nikakupa maana ya tamko ushahidi.Jaribu kuiweka huru akili yako pia ujenge hoja kwa umakini,tuendelee kupeana faida....
 
Kaka msingi wa hoja zangu umemili kuwajibu wale wanaokubaliana na jambo hilo hasa hao wanasayansi.Suala la kusema kuna watu wamehojiwa na wameshawahi kuwaona ndio ikawa hoja juu yako juu ya kuthibitisha uwepo wa viumbe hao ? Huo ni uchache wa maarifa ya uhakiki wa Habari mzee.Uliza kwa sababu gani ? Jibu ni rahisi sana.Mathalani tukio la Zimbabwe linazungumzia juu ya ushahidi wao ya kuwa waliowaona hao viumbe ni watoto ? Swali la msingi kwanini wamehusishwa watoto na watu wa sehemu hiyo ? Pili,mtoto ni mtu na ni binadamu,pia,je mtoto ana nafasi gani juu ya kufanyiwa kazi kile anachokisema ? Katika masharti juu ya ushahidi wa mtu kuwa na nguvu na kufata hatua ya piliya kufanyiwa kazi,ni lazima huyo anayetoa ushahidi awe ni baleghe yaani amepevuka na sharti la ziada ni awe na uwezo wa kupambanua mambo kwa lugha za uhakiki wa habari tunasema awe na uwezo kumaizi mambo.

Sasa unapoleta ushahidi uliotokana na watoto unatakiwa kuangalia ndani zaidi ya utoto wao.Mara ngapi watoto waliona paka pori wakasema yule ni simba ? Na suala la wao kuchora walichokisema eti ukakijengea hoja ? Ajabu ilioje juu ya dunia hii.
 
Kaka niliandika katika hoja zangu ya kuwa misingi ya kisayansi ina udhaifu mkubwa sana katika kufikia hitimisho la jambo fulani ndio maana leo akisema A kesho watasema B.

Kwahiyo mimi najadili misingi ya kisayansi na matokeao yake na wewe unajadili matokeo ya sayansi bila kuijua misingi yao,hili ndio tatizo lililopo kati yetu.

Tengeneza kiti chako kwako ndio ukipambe mzee.
 
Mi natupenda tu alien tuje tu ni kama tu midoli twa kuchezea
 
Kwenye kufikiri kuwa hoja yangu msingi wake ni sayansi tu ndipo penye tatizo na kwasababu hii nakuambia hujaelewa nilichokisema na hata ulichokinunuu ...

Mkuu kwanini usirudie kusoma huenda ukaelewa?

By the way,sayansi inadanganya wenye mambo yote au baadhi tu?
 
1;Unachokifanya hapa ni kutaka kuonesha kuwa wanasayansi ni watu waongo na ambao hawajawahi kufanya jambo lolote la maana kiasi kwamba ni wa kupuuzwa sana.hii siyo kweli hata kidogo na inawezekana labda kwako ni waongokwa kiwango hiki.Unaweza kutueleza kuwa ni waongo kwenye mambo yote?

2;Kimsingi watoto huwa wanasema kweli kabisa na ushahidi wao huwa unakubalika sana mahakamani hadi ithibitishwe walirubuniwa au kulazimishwa kwa njia mbali mbali kusema waliyosema.Dhana yako ya ushahidi wa mtu hadi abalehe ni dhana ya wapi sijui....

Bado sijaona sababu ya kufuatilia maelezo yako kwa kina hadi sana labda ukinipa maelezo ya kueleweka....
 
Unaniambiaje nirejee misingi ya sayansi wakati wewe huitaki hiyo sayansi?

Sina ushahidi namna gani?
Haya maelezo yako yanakinzana na maelezo yako hapo juu,hebu rejea uone namna unavyo0jikinza....
Nani amesema kuwa hao Aliens wanawezekana kuwa ni majini?

Unasoma ninachoandika vizuri mkuu?
Swali litakuja Je unaweza kutupa uhusiano uliopo kati ya majini na hao Aliens,kama utakuja au unadhani ya kuwa hao Aliens wanaweza kuwa Majini.
Hili swali lako halina mashiko kutokana na msingi wa swali hili ambalo ni hiyo kauli yako hapo juu kuwa siyo ya kweli...
Kutawala maana yake nini kwa namna unavyoelewa wewe?

tuanzie hapo halafu uone namna unavyokuna kushindwa kutetea hiki unachoandika hapa...
Kuhusu kutokuielewa makala yako,maneno hayo si sahihi sababu,nimegusia mambo muhimu juu ya udhaifu wa sayansi na nikakupa maana ya tamko ushahidi.Jaribu kuiweka huru akili yako pia ujenge hoja kwa umakini,tuendelee kupeana faida....
Akili yangu iko huru sana,tatizo ni kwamba matatizo yako unayaonea kwangu kitu ambacho ni tatizo zaidi....

Wewe peke yako ndiye unasema umegusa mambo muhimu bila kujua kuwa unaweza kuona ni muhimu wakati kiuhalisia ikawa siyo....
 
Kiongozi twende taratibu sasa,naona unaelekea kunielewa.Nimekwambia urejee misingi ya sayansi ili ujue ni yapi mapungufu ya sayansi na usiendelee kujadili matokeo ya sayansi sababu mafikio yako yatakuwa ni kubebeshwa uongo ulio mwepesi na kushindwa kuujua uongo huo.Misingi ndio asasi ya kujua hatima ya jambo husika,misingi imara huleta natija madhubuti.Sayansi siikubali hasa sayansi ya mambo ya anga kutokana na misingi yake.Natilia mkazo urejeetena na tena kwenye misingi ya sayansi ili ujue uozo wa sayansi.

Maelezo yangu kamwe hayapingani na ukiona yanapingana basi tambua kuna mambo mawili juu yako.

1.Kwanza ituhumu akili ya kuwa imeshindwa kuyadiriki mawazo na kuyaelewa ndio maana ukafikia hitimisho la kusema ya kuwa yana kinzana.Hapa naweza kukupa mfano juu ya kauli kwayo kwa uelewa mdogo utaweza kusema ya kuwa kauli hizi zina kinzana.Tazama kwa makini kauli hizi.

a) Nilijifunza shari niijue ili nisifanye shari na

b) Haifai mtu kujifunza kufanya mambo maovu.

Mwenye uchache wa kufikiri na kung'amua mambo hapo lazima atasema kauli hizi mbili zinakinzana.Swali la msingi litakuja ni wapi zinakinzana kauli hizo.Tusipende mteremko lazima tuzishughulishe kauli zetu.

2.Pili kuona kwako kauli zangu kama zinakinzana,lazima uituhumu elimu yako kuwa haina uwezo kung'amua mawazo yangu au hoja nilizo zihudhurisha hapo juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ